Feb 24, 2012

EAST AFRICAN GOSPEL STAR ROSE MUHANDO SIGNS MULTI-RECORD DEAL WITH SONY MUSIC

Global recording company Sony Music Entertainment is proud to announce the signing of East African Gospel Star Rose Muhando to its roster of artists, which includes some of the most important recordings in history. The signing was announced at a press conference in Dares Salaam, Tanzania on the 9th February 2011, and is the first deal of its kind for East Africa.

Rose Muhando is undoubtedly one of Africa’s biggest selling and most acclaimed gospel artists, with millions of fans throughout East Africa and her home country Tanzania. The gospel diva has now been signed to a multi-album recording deal with Sony Music, and a fullservices management deal with Sony Music and ROCKSTAR4000.

Sony Music Entertainment Africa views the continent of Africa as a highly important music development frontier and believes that some of the best talent in theWorld is currently creating and performing music across the continent. Sony has set its sights on becoming the primary partner of the best Africa has to offer and has high hopes that with its assistance, African musicians can achieve new Pan African and Global success.

“We’re so excited about the wealth of talent we are discovering literally daily inAfrica.” says Managing Director of Sony Music Entertainment Africa Sean Watson. “Rose is a magnificent example of the level of talent we mean to invest in. Her gift is quite extraordinary and we are very proud to be her partner. We count her alongside us as a pioneer of a new era in African music.”

'Its a new and exciting time for amazing talent and music from Africa to shine and we are thrilled to have a star like Rose as part of the family and to represent Rose through the next chapter of her very successful career' said Jandre Louw, CEO of ROCKSTAR4000 Music Entertainment.

‘I am thrilled and honored to be working with great African talents. Rose Mhando is a new addition to this roaster of clients that embodies what Rockstar 4000 believes and stands for. She is an Iconic local Tanzanian brand that we will develop to become an International brand’ added Christine Seven Mosha, Music and New business of ROCKSTAR4000

Rose was so excited and thanked God for all he has blessed her with.Rose Muhando was born in 1976 and was raised in Dodoma, Tanzania. On being deathly ill, Rose converted to Christianity and it was this move, her leading the choir at her local church and her meeting Nassan Wami that prompted her first album recording.

Today Rose lives in Dar Es Salaam where her career has flourished over the last 10 years. To date, Rose's first album shattered sales records, selling over 5 million copies. She currently has her second album (JipangeSawaSawa) out, which has already sold well over 1.3 million copies. The magical voice has not been restricted to Tanzania and she has toured extensively across the African continent, covering cities in Kenya, Mozambique, South Africa, Malawi. Congo, Uganda. Rose has also been well received in the United States.

For more information contact:

Tabasamu Pr Consultancy

+255 754 602674

tabasamupr@gmail.com

ROCKSTAR4000 MEDIA & PRESS:

media@rockstar4000.com

Follow us on:

www.facebook.com/sonymusicafrica

www.rockstar4000.com

www.facebook.com/i.am.rockstar.4000

www.twitter.com/rockstar4000

www.facebook.com/rose_muhando

www.youtube.com/iamrockstar4000

Feb 15, 2012

BINTI WA WHITNEY HOUSTON ATAKA KUJINYONGA

WHITNEY HOUSTON

BOBBI KRISTINA

BAADA ya kutokea kwa kifo cha mwimbaji, Whitney Houston kumeibuka kwa taarifa mbalimbali huku nyingine ambazo zimeendelea kuchukua nafasi ni binti yake Bobbi Kristina (18), ambaye amekimbizwa hospitalini mara mbili tangu kufariki kwa mama yake.

Kifo cha mwanamama huyo kimeishtua dunia na kuwa gumzo kimehusishwa na kutumia dawa za usingizi kupita kiasi na pombe.

Sababu ya kusema hivyo imeelezwa kwamba amekutwa amefariki ndani ya maji wakati akiwa anaoga kwenye bafu la hoteli ya Beverly Hilton chumba cha kifahari namba 434 aliyokuwa anaishi kabla ya kupatwa na umauti.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanasema kwamba wakati alipoingia bafuni kuoga walishangaa amekaa kwa muda mrefu na ndipo walipoanza kugonga lakini bila majibu, ikambidi mtengenezaji wake wa nywele afungue mlango na kumkuta akiwa amelala kifudifudi juu ya maji.

Ndipo alimuita mlinzi wa mwanamama huyo akaingia na kumvuta ambako walimpeleka hospitali wakamchukulia vipimo na kugundua tayari alikuwa ameshafariki.

Kuna taarifa nyingine zinazosema kwamba siku moja kabla ya kifo alionekana akiwa kwenye baa ya hoteli hiyo akinywa kinywaji huku wengine wakimuhusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Kifo cha mwanamama huyo kimesababisha binti yake mwenye miaka 18, Bobbi Kristina kuchungwa kwa makini akihofiwa huenda anaweza kuchukua uamuzi wa kujingonga.

Houston (48) kabla ya kifo chake amekuwa akisemwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambako inadaiwa inawezekana atakuwa ametumia dawa hizo wakati akiwa amelewa.

Baada ya msako chumbani mwake zilikutwa chupa za Lorazepam, Valium, Xanax na dawa nyingine za usingizi ambazo wakati mwingine hutumiwa na mateja kama kilevi halim inayowasababisha wengi kuamini kwamba inawezekana baada ya kunywa pombe alichukua dawa hizo na kutumia.

Pamoja na maneno hayo yote ofisa wa Los Angeles alikana taarifa zilizokuwa zikimuhusisha mwanamama huyo na kufariki kutokana na maji aliyokuwa akioga kudaiwa kuingia kwenye mapafu yake.

Alisema kwamba taarifa zote zimebaki kuwa fununu ila ukweli kamili utaelezwa hapo baadaye baada ya polisi kumaliza upelelezi wake, ambao utachukua zaidi ya mwezi mmoja au miwili hivi, na mpaka sasa bado upo chini ya uchunguzi wa polisi na hakuna anayeruhusiwa kuutembelea na kuutazama mpaka pale watakapowaruhusu kuuondoa.

Baada ya kutangazwa kwa kifo chake aliyekuwa mumewe, Bobby Brown (43) ameripotiwa kuchanganyikiwa na kujikuta akitokwa machozi muda wote baada ya kupokea taarifa za kifo hicho alijikuta akiwaliza mashabiki waliokuwa wamehudhulia onesho lake la huko Mississippi, Marekani, alilokuwa akipiga na bendi yake ya New Edition ambako alisikika akilia kwa sauti akisema “nakupenda Whitney” huku akipiga busu hewani.

Baada ya kifo chake kilichotokea muda mchache kabla ya kufanyika kwa tuzo za Grammy mwimbaji Jennifer Hudson aliimba nyimbo ya heshima kwa ajili ya gwiji huyo wa muziki.

Naye rafiki wake wa karibu na mwimbaji huyo Mariah Carey aliongoza kutoa rambirambi kwa kusema “Nimevunjika moyo na machozi yananitoka kwa kifo cha rafiki yangu mpenzi Whitney Houston, hatatokea mwanamuziki mwingine mwenye sauti nzuri kama yake duniani."

Naye mwimbaji Christina Aguilera aliandika kwenye Twitter akisema “Tumepoteza gwiji mwingine. Tuwaombee familia ya Whitney kwa kumpoteza mtu muhimu."

Gwiji wa miondoko wa Aretha Franklin, alisema ameshtushwa na habari hizo na kuongeza “Siwezi kusema lolote kwa sasa ila bado siamini nilichokisikia. Sikuamini maneno yaliyokuwa yakipita kwenye kioo cha TV yangu niliposoma na moyo wangu ukaanza kuwaonea huruma Cissy, binti yake Bobbi Kris, familia yake na Bobby."

Kuna taarifa zinasema kuwa mwaka 2001 baada ya kifo cha mfalme wa Pop kuliibuka uzushi uliokuwa ukimuhusisha na kufariki siku ya pili.

Mahusiano

Mwaka 1980 mwimbaji huyo akiwa maarufu alianza kujihusisha katika mahusiano na mchezaji wa soka ya Marekani, Randall Cunningham na mwigizaji Eddie Murphy. Mwaka 1989 alikutana na mwimbaji wa R&B, Bobby Brown katika sherehe za utoaji wa tuzo za Soul Train Music na hapo walianza mahusiano rasmi yaliyodumu kwa miaka mitatu na Julai 18, 1992 kutangaza ndoa.

Machi 4, 1993 wawili hao walipata binti yao wa kwanza, Bobbi Kristina Houston Brown.

Mahusiano ya wawili hao yalikuwa katika wakati mgumu baada ya kubanwa na kashfa za kutumia dawa za kulevya kwa kila chombo cha habari.

Pamoja na mara kadhaa kugoma kukubali hilo ila mwaka 2009, Whitney alikiri kwenye kipindi cha TV cha Oprah Winfrey alikiri na kusema kwamba walianza kwa na mumewe wa zamani Bobby Brown, kuvuta bangi na baadaye kokeini.

Katika kipindi hicho alibainisha kwamba sababu kubwa ya kutumia dawa za kulevya ilichangiwa na kutaka kumfurahisi mumewe huyo aliyekuwa akimpenda ambaye alikuwa amethirika na dawa hizo za kulevya.

Akasema “kuna wakati ulifikika dawa za kulevya zilikuwa ndio kila kitu katika maisha yake, na nisipotumia sipati furaha na nilipotumia kuna wakati nilijikuta napoteza njia."

Oktoba 1994, Houston alipiga muziki katika sherehe ya chakula cha usiku katika Ikulu ya Afrika Kusini wakiwa wamearikwa na rais wa nchi hiyo, Nelson Mandela ambaye alimpigia debe na kumuwezesha kushinda uchaguzi wa kwanza wa kuondoka kwa ubaguzi wa rangi.

Mwigizaji huyo baada ya kupata matatizo hayo yaliyoonekana kuchangiwa zaidi na dawa za kulevya alichukua uamuzi wa kutengana na Boby mwaka 2007 aliyemuona kama mtu aliyechangia kuharibu maisha yake kwa kumsababishia kuwa teja na pia alimlaumu kwa kumpatia kipigo kila wakati.

Muda mfupi baada ya kutangaza kutengana na Boby aliripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mdogo wa mwaimbaji, Brandy anayekwenda kwa jina la Ray-J ambaye kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 17 hiyo ilikuwa mwaka 2007 na 2009.

Jambo hilo lilisemwa kila kona hali iliyosababisha hata Bobby Brown, kumtishia kijana huyo akifikiria sababu kubwa ya kutengana na mkewe huyo ilichangiwa na mahusiano hayo.

Unapozungumzia mwaka 1980 hadi 1990 mwimbaji huyo alikuwa mwimbaji anayeongoza kimauzo, mwenye sauti ya mvuto na yenye nguvuna mwigizaji aliyetamba na filamu kama vile ‘The Bodyguard’ na ‘Waiting to Exhale.’

Uwezo wake wa kuimba ulichangia kwa kiasi kikubwa kuibua vipaji vya waimbaji ambao nao wamekuwa moto kama vile Christina Aguilera, Mariah Carey.

HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA HUKOOOO DOM KATIBA MPYA YA CHAMA VS KATIBA MPYA YA NCHI TEH TEH TEH TEH TEH CCM WOYEE!!!!!

Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha NEC mjini Dodoma jana. Kushoto ni Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Wanzibar Dk. Ali Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Amani Abeid Karume. Kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akisisitiza jambo kwenye kikao hicho. Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dk. Sheni na Makamu Mkt (Zanzibar) Amani Abeid Karume
Kicheko: Rais Kikwete, Mukama na Msekwa wakicheka baada ya kufurahishwa na hoja za wajumbe wakati wa mjadala wa marekebisho ya Katiba ya CCM
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Ali Hassan Mwinyi akifurahia jambo wakati wa kikao cha NEC mjini Dodoma juzi.
Rais Kikwete akijenga hoja katika mkutano huo
Wajumbe wa NEC kutoka Tanzania Bara wakinyoosha mikono kuunga mkono marekebisho ya katiba ya CCM ambayo yalipitishwa na kikao hicho
Rais Kikwete, Mukana na Msekwa wakiongoza kunyoosha mikono kuunga hoja hiyo
Wajumbe wa NEC Zanzibar wakinyoosha mikono kuunga mkono kupitishwa kwa marekebisho ya Katiba ya CCM

JIKUMBUSHE WATEULE KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2012

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe (Pichani) alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri na zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2011”.

Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George Kavishe aliongeza “Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo zitaendeshwa kisasa na kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki nchini. Tunaendeleza ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi hili la Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.”

Kura za wana Academy ni siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro hubaki siri ya INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi za washindi.

Hatua zifwatazo:
1. Semina ya Wasanii:
Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina elekezi kuhusu tuzo hizi na kupata nafasi kuuliza maswali juu ya mchakato mzima wa kupata wateule na taratibu zitakazofwata.

2. Kura.
Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb - 06/ Apr Maelekezo ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro www.kilitimetz.com na mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya magazeti na vipindi mbali mbali ya redio na TV.

3. Usiku wa utoaji Tuzo.
Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012 katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na TV mbali mbali.

Walioteuliwa majina na kundi la Mtumbuizaji Bora wa Kike Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Queen Darleen, Dayna na Shaa.Mtumbuizaji Bora wa Kiume, Diamond, Ally Kiba, Bob Junior, Dully Sykes na Mzee Yussuf.

Mwimbaji Bora wa Kiume Ally Kiba, Diamond ,Barnaba, Belle 9 na Mzee Yussuf. Mwimbaji Bora wa Kike Lady Jaydee, Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Dayna na Linah.

Wimbo Bora wa Taarab Full Stop ulioimbwa na Khadija Kopa, Mamaa Mashauzi wa Isha Mashauzi,Hakuna Mkamilifu wa Jahazi, Nilijua Mtasema, Wimbo Bora wa Mwaka jina na aliyeucheza katika mabano ni Hakuna (Suma Lee), Dushelele (Ally Kiba), Moyo Wangu (Diamond), Mathematics (Roma), Nilipe Nisepe (Belle 9) na Riz One (Izzo B).

Katika kundi la kuwania tuzo ya Wimbo Bora ya Kiswahili uliopigwa na bendi unawaniwa na Dunia Daraja (The Africa Stars), Hukumu ya Mnafiki (Mashujaa Band), Falsafa ya Mapenzi na Mtenda zote (Extra Bongo) na Usia wa Babu (Mapacha Watatu).

Wimbo Bora wa R&B unawaniwa na nyimbo za My Number One Fan (Ben Pol), Maumivu (Ben Pol ft One), Nilipe Nisepe(Belle 9), Napta Raha (Jux) na Usiniache (Hemed). Wimbo Bora wa Hip Hop wanaowania ni Famous (Jay Mo ft P Funk), King Zila (Godzilla ft Marco Chali), Mathematics (Roma), Riz One (Izzo B), Kilimanjaro (Joh Makini ft Lady Jaydee, G Nako),Wimbo Bora wa Reggae Mazingira (Malfred ft Lutan Fyah),Arusha Gold (Worrior from the East), Give it Up to me(Delyla Princess), Nia Yao (20%), Ni Wewe (Nakaaya).

Wimbo Bora wa Ragga/Dancehall unawania wan a Goo Look (A.Y ft Miss Trinity), Maneno Maneno (Queen Darleen ft Dully Sykes), Ganja Man (Dabo), Kudadeki na Poyoyo (Malfred). Rapa Bora wa mwaka bendi wamo Kalidjo Kitokololo, Khalid Chokoraa, Msafiri Diouf na Totoo Ze Bingwa, Msanii Bora wa Hip Hop ni Godzilla, Roma, Izzo B, Joh Makini na Fid Q.

Kwa upande wa tuzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki inawaniwa na Kigeugeu (Jaguar)Chokoza (Avrill na Marya), Mulika Mwizi (Kidumu ft Sana), Coming Home (Nameless) , 4sho4shizzle (Prezzo) na Valuvalu (Jose Chameleon).

Tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka inawaniwa na Diamond, Ali Kiba, Mzee Yussuf, Barnaba na Belle 9. Huku tuzo ya Mtayarishaji Bora (Producer) wa mwaka inawaniwa na Marco Chali,Pancho Latino, Bob Junior Maneck na Man Walter.

Video Bora ya Muziki ya Mwaka zinazochuana ni Moyo Wangu (Diamond), Hakunaga (Suma Lee), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Ndoa Ndoana (Kassim Mganga ft Mr. Blue) na Bongo Fleva (Dully Sykes).

Wimbo Bora wa Afro PopHakunaga (Suma Lee),Bongo Fleva (Dully Sykes), Moyo Wangu na Mawazo (Diamond) na Nai Nai (Ommy Dimples).Wimbo Bora wa Zouk/ Rhumba Daima Milele (Barbanaba), Dushelele (Ally Kiba), Nivute Kwako (Dyna ft Barbanaba),Wangu Lady Jaydee ft Mr. Blue) na Kizunguzungu (Recho).

Wimbo Bora wenye vionjo vya Kiasili unawaniwa na Bao la Kete (AT),Kidudu Mtu (Offside Trick ft Baby J), Vifuu Tundu (A.T ft Mwanne), Mwanadamu (Ashimba) na Tunapeta (Young Dee ft Kitokololo na Mataluma).Msanii Bora Anayechipukia Ommy Dimpoz, Darasa, Recho, Abdul Kiba na Beatrice a.k.a Nabisha. Wimbo Bora wa Kushirikiana ni Famous (Jay Moe ft P-Funk Majani), King Zilla (Godzilla ft Marco Chali), Wangu (Lady Jaydee ft Mr. Blue), Kama ni Ganster (Chegge, Tembaft Ferouz) na Nai Nai (Ommy Dimpoz ft Ally Kiba).

JK KUPANGUA BARAZA LA MAWAZIRI



















PANGA pangua ya Baraza la Mawaziri imewadia. Imeelezwa kwamba Rais Jakaya Kikwete anajipanga kufanya mabadiliko makubwa katika baraza lake, Tanzania Daima Jumatano limedokezwa.

Taarifa za Rais Kikwete kutaka kufanya mabadiliko hayo, zilizagaa mjini Dodoma wakati alipowasili kutoka mjini Mwanza alikokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Baadhi ya mawaziri ambao hawakupenda majina yao yatajwe, waliliambia gazeti hili kwamba Rais Kikwete anatarajia kufanya mabadiliko makubwa ya baraza lake mara baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, (NEC), kilichomalizika mjini Dodoma juzi.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema mabadiliko hayo ambayo yatakuwa ya kwanza tangu Rais Kikwete alipochaguliwa kwa mara ya pili kumalizia awamu ya mwisho ya uongozi wake, yametokana na sababu kubwa tatu.

Mosi, yanatokana na baadhi ya mawaziri kuugua kwa muda mrefu na hivyo kulazimika kuwapa nafasi ya kupumzika, huku wakiendelea kujiuguza.

Mawaziri wanaougua na huenda wakaachwa ili kupumzisha afya zao ni pamoja na Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye kuugua kwake kumeibua tuhuma nzito kwamba huenda kiongozi huyo amelishwa sumu.

Hivi sasa umeanzishwa uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo ambazo kwa mara ya kwanza ziliibuliwa hadharani na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kati, Samuel Sitta.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, naye huenda akakumbwa na mabadiliko hayo kwani licha ya kurejea nchini na kuanza kuingia ofisini, afya yake imezidi kuzorota.

Sababu ya pili ya mabadiliko hayo inaelezwa kuwa inatokana na utekelezaji wa maazimio ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii iliyokuwa inachunguza mgogoro wa serikali na madaktari.

Katika mapendekezo yake, kamati hiyo inayoongozwa na Magareth Sitta ilipendekeza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, na Naibu wake, Dk Lucy Nkya, wawajibishwe kwa madai ya kuhusika na uzembe uliosababisha mgomo huo ambao umeleta athari kubwa nchini.

Wengine waliopaswa kuwajibishwa kutokana na mgomo huo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu, Dk. Deo Mtasiwa.

Tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametangaza kuwasimamishwa kazi Nyoni na Dk. Mtasiwa ili kupitisha uchunguzi dhidi yao.

Sababu ya tatu, inaelezwa kuwa ni uzembe wa baadhi ya mawaziri, huku panga pangua hiyo, ikitarajiwa kuwakumba pia mawaziri ambao kwa muda mrefu wizara zao zimekuwa zikituhumiwa kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa katika mabadiliko hayo yanayotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia sasa, Rais Kikwete ameingiza sura mpya, kuwabadilishia baadhi yao wizara, huku wengine wakitupwa nje kusubiri wapangiwa kazi zingine.

Shinikizo la Rais kutaka afanye mabadiliko katika baraza lake, limekuwa likitolewa na watu wa kada mbalimbali nchini, wakiwemo wabunge wa CCM.

Alipokuwa akizungumza na wabunge wa CCM mjini Dodoma, baadhi ya wabunge walimtaka Rais Kikwete kufumua Baraza lake la Mawaziri kwani baadhi yao wamechoka na hawana ubunifu tena.
Chanzo; gazeti la Tanzania Da
ima

MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA UZINI ZANZIBAR YATHIBITISHA MWISHO WA CUF UMEFIKA

Mshindi wa Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Uzini, kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mohammed Raza, akiwaonesha waandishi na wananchi cheti cha kuthibitishwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

MATOKEO ya uchaguzi mdogo wa uwakilishi wa Jimbo la Uzini, Dunga, Wilaya ya Kati, Unguja, uliofanyika Jumapili ya Februari 12, 2012, yametangazwa na Mohammed Raza mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuibuka mshindi wa kishindo huku yakituachia mafunzo kibao.

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na msimamizi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Wilaya ya Kati, Mussa Ali Juma, Raza alizoa kura 5,377 akifuatiwa na mgombea wa CHADEMA, Ali Mbarouk Mshimba (281), Salma Hussein Zaral wa CUF (223), Khamis Khatib Vuai wa Tadea (14) na Rashid Yussuf Mchenga wa AFP kura nane.

Wapiga kura waliojiandikisha katika uchaguzi huo walikuwa 8,743, lakini waliojitokeza ni 5,903 na kura zilizoharibika 28, na kwa maana hiyo wapiga kura ambao hawakujitokeza kupiga kura walikuwa 2,852.

Kwangu mimi matokeo hayo yametoa mafunzo, kwanza kutokana na kura nyingi alizopata Raza ni dhahiri kwamba wananchi wa jimbo hilo wamethibitisha kuwa wameridhishwa na utawala wa CCM, hivyo wapinzani waangalie vema sera zao kama wanatamani kulitwaa jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

Pili, na ambalo ni kubwa kabisa ni kwamba, CUF wanapaswa kuketi haraka kujiangalia walipofikia, ni dhahiri mvutano baina ya Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed na Katibu Mkuu wao Maalim Seif Hamad unakimaliza chama hicho na kama hawatajifunza kwa hili, basi tusubiri kuona kinavyosambaratika.

Naamini kwa kulisema hili watu wengi wa CUF hasa upande wa Maalim Seif watanichukia na kukereka na pengine kuniona kama adui kwa kuwa wao wanaamini Maalim Seif ndiye yuko sahihi na Hamad Rashid si kitu na hana athari yoyote ndani ya chama.

Lakini binafsi nimeona bora niseme hili kwa kuwapa huu Muarobaini ili waunywe kwa kuwa ndio utakaowaponya vinginevyo nisipofanya hivyo nitalazimika kuungana na wengine wanaosubiri kuona jinsi chama hiki ambacho awali kilionekana ndicho pekee chenye nguvu katika upinzani Zanzibar na hata Tanzania bara pia kinavyosambaratika.

Sijui ndugu zetu wa CUF wanasubiri alama gani itokee ndipo wakubali kuwa panahitajika suluhu ya haraka baina ya pande zinazohasimiana ndani ya chama hicho, ikiwa kura 223 alizopata Salma Hussein Zaral, zimefunikwa hata na zile za Ali Mbarouk Mshimba wa CHADEMA aliyepata kura 281.

CHADEMA ambayo hakuna aliyekuwa akiitazamia kupata walau robo ya kura achilia mbali kuzifikia kura za CUF, imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili na kuipiku CUF.

Sitaki kuamini kuwa CHADEMA kina wanachama wengi kuliko CUF katika jimbo la Uzini, bali ninachokiamini ni kwamba mgogoro baina ya Hamad Rashid Mohamed na Maalim Seif sasa unahitimisha utawala wa CUF katika siasa za upinzani Tanzania Visiwani na Bara pia.

Kwa wale tuliokuwa tukifuatilia kwa karibu majibizano yalivyokuwa ndani ya CUF tangu hali ya kutoelewana baina ya wawili hawa ilipoanza hadi kuvuliwa uanachama kwa Hamad Rashid na washirika wake na jinsi ambavyo baadhi ya wananchama walivyoanza kujiengua, sasa tunathibitisha kuwa mgogoro huo unaathari kubwa.

Wale waliokuwa wakimbeza Hamad Rashid kwa sababu mbalimbali wanazozijua na kumuona Maalim Seif kuwa mtu asiyekosea au kustahili kuonywa, kukumbushwa ndani ya chama hicho, naamini kwa hili watabadili mtizamo wao.

Wakati baadhi ya watu kutoka maeneo mbalimbali ya bara walipoanza kurudisha kadi baada ya Hamad Rashid na wenzake kuvuliwa uanachama, uongozi wa CUF ulijaribu kuwaaminisha watu kwamba hao ni mamluki lakini kwa uchaguzi huu wa Uzini ni wazi wameumbuka.

Kwa hili walilolionyesha wananchi wa Uzini kuacha kumpigia kura mgombea wa CUF badala yake wakaamua kuzipeleka kwa mgombea wa chama kingine cha upinzani cha CHADEMA na kumfanya Ali Mbarouk Mshimba, kumfunika Salma Hussein Zaral wa CUF kinathibitisha hilo.

Lakini pia wananchi wa Uzini wamethibitisha na kutoa funzo kwamba, hakuna chama chenye hati miliki ya kuongoza, kwamba chama chochote kitakachoamua kuwapigania katika kusaka maendeleo yao watakiunga mkono kama walivyofanya kwa CHADEMA.

Aidha, kwa matokeo haya, wametufunza pia kwamba kila chama kinaposimamisha mgombea kihakikishe kuwa ni mtu anayekubalika mbele ya jamii na si kutokana na sababu nyingine zozote zile kwani pasipo kufanya hivyo kitaadhirika.

Pia matokeo hayo yamethibitisha kuwa, kila chama kinapaswa kufanya uchambuzi wa kina kuhusu kukubalika kwake na kwamba si lazima kusimamisha mgombea pale ambapo kinaamini hakina uungwaji mkono wa kutosha.

Sidhani kama viongozi wa chama makini watakuwa tayari kutumia mamilioni ya fedha kumsimamisha mgombea ili tu kuonekana nacho kimeshiriki uchaguzi, wakati mwisho wa siku mgombea anapata kura zisizofika kumi.

Nimalize kwa kukumbushia hoja yangu kwamba uchaguzi huu mdogo wa Uzini umetuthibitishia pasipo shaka kwamba kama CUF hawatachukua tahadhari basi mwisho wao umefika.
Chanzo;Tanzania Daima

TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MPANGO WA UENDESHAJI WA SHUGHULI ZA SERIKALI KWA UWAZI (OPEN GOVRNMENT PARTNERSHIP-OGP)

Tanzania imeridhia kujiunga na Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi (Open Government Partnership - OGP). Mpango huu ni juhudi za kimataifa katika kuhimiza uendeshaji wa Serikali kwa uwazi zaidi, ushirikishwaji mkubwa wa wananchi, kudhibiti rushwa katika jamii na kuimarisha utoaji wa huduma bora.

Mpango huu ulizinduliwa rasmi na Viongozi wa Nchi za Marekani, Mexico, Norway, Afrika ya Kusini, Indonesia na Uingereza tarehe 20 Septemba, 2011 wakati wa Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, Marekani. Kwa kutambua umuhimu wa Mpango huu, Tanzania imeridhia kujiunga nao. Hadi sasa nchi nyingine 37 zimeridhia kujiunga zikiwemo nchi nne (4) kutoka Bara la Afrika ambazo ni Afrika ya Kusini, Ghana, Kenya na Liberia.

Vigezo vya nchi kuwa mwanachama wa Mpango huu ni pamoja na kuandaa Mpango Kazi wa Kitaifa (Country Action Plan) kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi na wananchi. Mambo muhimu yanayosisitizwa ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Serikali, kuwawezesha wananchi kupata taarifa kutoka Serikalini kwa urahisi zaidi, kuzuia na kupambana na rushwa na kusisitiza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi katika uimarishaji wa utawala bora.

Serikali imeanza mchakato wa kutayarisha Mpango Kazi wa Kitaifa. Katika kuandaa mpango huo wananchi watashirikishwa kikamilifu ili kutoa maoni yao kuhusu maeneo yatakayozingatiwa kwenye Mpango. Njia mbalimbali za mawasiliano zitatumika kukusanya maoni ya Wananchi. Njia hizo ni pamoja na tovuti ya wananchi (www.wananchi.go.tz), barua za kawaida kupitia posta (Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Ikulu, S.L.P. 9120, Dar es Salaam), ujumbe bila malipo kupitia simu ya mkononi (SMS) namba 0658-999222, barua pepe: ogp@ikulu.go.tz na mikutano ya majadiliano na wadau mbalimbali.

Mkutano wa kwanza wa kukusanya maoni ya wadau ulifanyika tarehe 15 Novemba, 2011 na uliwashirikisha wawakilishi kutoka Taasisi za Kiraia, Sekta Binafsi, Mashirika ya Kidini, Vyombo vya Habari na Serikali.

Kwa kuanzia, uandaaji na utekelezaji wa Mpango huo utahusisha vipaumbele vya sekta tatu za Afya, Elimu na Maji ili kuimarisha uwazi, uadilifu na uwajibikaji katika utoaji wa huduma. Mpango utaendelea kuongeza wigo wa utekelezaji kwa kujumuisha sekta zote kadri uzoefu utakavyopatikana.

Serikali iko tayari na imedhamiria kutekeleza Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa uwazi na inaamini kuwa Mpango huo utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi. Hivyo, Serikali inatoa wito na kuwakaribisha wananchi wote kutoa maoni yatakayosaidia kuandaa mpango wa kitaifa utakaosaidia kuongeza uwajibikaji, uwazi na uadilifu katika utendaji wa kazi kwenye sekta za Afya, Elimu na Maji. Muda wa kutoa maoni ni kuanzia sasa hadi tarehe 25 Machi, 2012. Tunawaomba Wananchi, washiriki kikamilifu katika maandalizi ya Mpango Kazi wa Kitaifa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

IMETOLEWA NA OFISI YA RAIS

IKULU- DAR ES SALAAM.

Waume walalamikia kipigo Kenya - mwananchi

Februari tarehe kumi na nne ni siku ya wapendanao au Valentine, lakini siku hii ikiadhimishwa kote duniani kwa raha, baadhi ya waume nchini kenya hawaifurahi kwani wanapigwa na kunyanyaswa na wake zao.

Kulingana na mwenyekiti wa chama cha kutetea haki za wanaume nchini humo Nderitu Njogu, idadi ya wanaume wanaopigwa na wake zao imeongezeka mno.

Bw Nderitu anasema utafiti wa chama chake umeonyesha kuwa harakati za kumpa uwezo mwanamke zimeathiri maadili na kuwasabibisha kuwadharau wanaume.

Mwanaharakati huyo anadai kuwa tatizo hilo limechochewa zaidi na hali ya kuwa wanawake wengi sasa wana kipato kikubwa kuliko waume zao.

Mwishoni mwa wiki Polisi walimtia mbaroni mwanamke mmoja mjini Nyeri huko mkoa wa kati, baada ya kumshambulia mumewe na kumjeruhi vibaya kwa panga.

Mwanamume huyo bado anapokea matibabu hospitalini baada ya kukatwa katwa usoni. uchunguzi kuhusu tukio hilo bado unaendelea.

Bw Nderitu anadai kuwa zaidi ya wanaume 460,000 walinyanyaswa na wake zao mwaka jana. Anasema utafiti wa shirika lake unaonyesha kesi nyingi za waume kuteswa na wake zao zinaripotiwa katika mkoa wa kati.

"Siku hii ya Valentine na washauri wanaume wasikubali kudhalalishwa na wake zao, kwa kufanya matumizi makubwa kuliko na wanayoweza kumudu" alisema Bw Nderitu.

REDD’S ORIGINAL MDHAMINI MKUU WA MISS TANZANIA 2012.

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega akiongea na waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya JB Belmonte jijini Dar es salaam wakati alipotangaza udhamini wa Miss Tanzania 2012 ambapo Redds imedhamini mashindano hayo mwaka huu kwa milioni 700, katika picha kutoka kulia ni Miss Tanzania Salha Israel, Vick Kimaro Meneja wa Redds na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala. wakijiandaa kukabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na Vick Kimaro Meneja wa kinywaji cha Redds.
Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega na Meneja Masoko wa TBL Fimbo Butala. wakikabidhiana hati mara baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa mashindano ya Redds Miss Tanzania, wanaoshuhudia ni Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Patel kushoto nyuma na Vick Kimaro Meneja wa kinywaji cha Redds.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original leo imetangaza rasmi kuchukua nafasi ya “Mdhamini Mkuu” wa shindano kubwa kabisa la urembo hapa nchini lijulikanalo kama “Miss Tanzania”.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, meneja masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah alisema; Redds Original, leo inatangaza kuwa ndio wadhamini wakuu wa mashindano ya urembo Tanzania, yanayojulikana kama “Miss Tanzania”. Kwa udhamini huu, mashindano haya sasa yatajulikana kama “REDDS MISS TANZANIA 2012”. Kwa miaka kadhaa sasa Redds Original imekuwa ikishiriki katika mashindano haya kama mdhamini mwenza, yaani “Kinywaji rasmi cha Miss Tanzania”. Hivyo leo tunapiga hatua nyingine kubwa katika historia ya tasnia hii ya urembo hapa nchini kwa kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Miss Tanzania.

Katika kuonesha kuwa Redds Original, imedhamiria kwa dhati kuendeleza tasnia hii, leo tumesaini mkataba wa udhamini wa mashindano haya kwa kipindi cha miaka mitatu, yaani 2012 hadi 2014. Hii inawahakikishia wapenzi na mashabiki wa mashindano haya kuwa wataendelea kushuhudia mashindano haya na kuburudika na kinywaji cha Redds Original kwa kipindi chote hiki. Alisema Butallah.

Nae Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Bi. Victoria Kimaro alisisitiza juu ya udhamini wa mashindano haya kuanzia ngazi za chini hadi ngazi ya Taifa. Udhamini huu mkubwa wa mashindano ya Miss Tanzania unajumuisha udhamini tutakaotoa katika maeneo mbali mbali kwa ngazi za vitongoji hadi Taifa. Tunawaahidi mashabiki wote wa mashindano haya na wadau wa tasnia ya urembo kujiandaa kwa burudani ya hali ya juu.

Akizungumzia udhamini huo, Mkurugenzi wa LINO Agency waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Bw. Hasim Lundenga alisema; Kwa niaba ya kamati ya Miss Tanzania napenda kutoa shukurani za dhati kwa TBL kupitia kinywaji chake cha Redds Original kwa udhamini huu, na tunatangaza rasmi kuwa mashindano haya sasa yataitwa “Redds Miss Tanzania’. Kitu kikubwa tunachowashukuru wadhamini wetu ni mkataba ambao tumesaini hii leo, ukituhakikishia udhamini wa mashindano haya kwa miaka mitatu.

Kwa mara nyingine tunawapongeza zaidi Redds original kwa kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza tasnia hii ya urembo hapa nchini. Tumekuwa nao bega kwa bega kwa miaka kadhaa sasa, na haiwezekani ukazungumzia tasnia ya urembo hapa nchini bila kuitaja Redds Original.
Alisema Lundenga.
kwa msaada wa blog rafiki

Feb 5, 2012

SHEREHE ZA MAULID YA KUZALIWA BWANA MTUME MUHAMMAD S.A.W

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,(kushoto) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa kwanza kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji. (05/02/2012) (PICHA NA RAMADHAN OTHMAN IKULU)
Ustadhi Salum Rashid wa Madrsa Qadiria ya Amani akisoma Maulid Barzanji Mlango wa nne,ambao Waislamu husimama na kumswalia Bwana Mtume,S.A.W,wakati wa sherehe za Maulid zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,( katikati wakiitikia Dua katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume S.A.W zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Zanzibar,ikiombwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabbi,(wa pili kushoto)(wa kwanza kulia) Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu,na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji,Wazri wa Katiba na Sheria Sheikh Abuu Bakar Khamis,(kushoto). (05/02/2012)
Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi Seif,pamoja na viongozi wengine ni miongoni mwa waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume S.A.W. zilizofanyika katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Unguja.
Baadhi ya Waumini wa mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na viongozi wa Dini wakiwa katika kiwanja cha Maisara Suleiman,katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa kwa Bwana Mtume S.A.W. yaliyofanyika jana.
kwa msaada wa blog jirani

JK AONGOZA MATEMBEZI YA MIAKA 35 YA CCM JIJINI MWANZA

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza kuongoza matembezi ya mshikamano kwa ajili ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM leo asubuhi. Anayempokea ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wengine ni Spika wa Bunge Anna Makinda ambaye ni mlezi wa mkoa huo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. Pamoja na Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilllo. (Picxha zote na Bashir Nkoromo)
. Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu Yussuf Makamba.
Rais Kikwete akimsalimia Nape Nnauye Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya matembezi hayo.
Wananchi kutroka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo tayari kushiriki matembezi hayo.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM. Kutoka Ofisi hiyo hadi kwenye viwanja ni umbali wa kilometa tatu.
Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akiwa na Makatibu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza.
Kijana Mussa aliyemwagiwa tindikali wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga mwaka jana, akishiriki matembezi hayo. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Wananchi wakiushangilia msafara wa matembezi hayo ulipopita eneo la mtaa wao.
Sungusungu wakionyesha ukakamavu wao baada ya Kikwete kuwasili nba matembezi hayo kwenye viwanja vya Furahisha.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kiwkete akiwasalimu wananchi baada ya kufika mwisho wa matembezi hayo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
(kwa msaada wa blog rafiki)

Feb 3, 2012

JK launcehs First National Bank Tanzania

A round of applause rings after President Jakaya Mrisho Kikwete has officially launched the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania) yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam. Others from left are the High Commissioner of South Africa to Tanzania, Mr Thanduyise Henry Chiliza, the CEO of FirstRand, Mr Sizwe Nxasana and the Deputy Permanent Secretary in the Ministry of Finance Ms Elizabeth Nyambibo. (Photo by State House)
President Jakaya Mrisho Kikwete makes his keynote speech during the official launch of the First National Bank Tanzania (FNB-Tanzania) yesterday at the Kilimanjaro Grand Hyatt hotel in Dar es salaam today February 2, 2012.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA