Nov 3, 2010

Mathias Chikawe ahutubia mkutano wa AALCO, New York Marekani

Waziri wa Katiba na sheria na Rais wa Jumuiya ya Mashauriano ya Kisheria kati ya Nchi za Afrika na Asia (AALCO), Bw. Mathias Chikawe alihutubia mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika kando ya vikao vya 65 vya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa vinavyoendelea mjini New York, Marekani tarehe 02 Novemba 2010.

Kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Ombeni Sefue, Bw. Chikawe aliwaeleza wajumbe wa mkutano huo baadhi ya masuala muhimu yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa 49 wa mwaka wa AALCO uliofanyika Dar es Salaam kuanzia Tarehe 05 hadi 08 Agosti, 2010.

Baadhi ya masuala hayo ni pamoja na urejeshwaji wa Wapalestina katika maeneo yao na vitendo vya Israel vya kuyakalia kwa nguvu maeneo ya Wapelestina pamoja na changamoto za kupambana na ufisadi.

Kuhusu suala la Palestina, Waziri Chikawe alieleza kuwa nchi wanachama zililaani vikwazo vilivyowekwa na Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza kwa kusema kuwa vikwazo hivyo ni ukiukwaji wa sheria za kimataifa, ikiwa ni pamoja na Mkataba wa nne wa Geneva wa mwaka 1949.

Kuhusu suala la ufisadi, Waziri Chikawe alibainisha kuwa nchi zote wanachama zilikubaliana kuwa, Azimio la Umoja wa Mataifa la kupambana na ufisadi (UNCAC) ni silaha pekee ya kukabiliana na tatizo hilo. Nchi zilishauriwa kutunga sheria na vyombo husika kwa ajili ya utekelezaji wa Azimio hilo.

Aidha, Waziri Chikawe alieleza mikakati AALCO inayokusudia kuchukua kuongeza ushiriki wake kwenye Tume ya Kimataifa ya Sheria (ILC). Alieleza kuwa, katika mkutano wa Dar es Salaam nchi wanachama zilikubaliana kuwa AALCO iendelea kuzitupia jicho mada ambazo ILC inazipa kipaumbele.

Jambo lingine ambalo Waziri Chikawe alilizungumzia na pia lilijadiliwa kwenye mkutano wa Dar es Salaam ni suala la Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC). Alieleza kuwa, AALCO inafuatilia kwa karibu masuala yanayogusa Mahakama hiyo. Alisema kuwa, mkutano wa Dar es Salaam uliangalia masuala yaliyojadiliwa kwenye mkutano wa kwanza wa kupitia Mkataba wa Rome uliofanyika Kampala, Uganda kuanzia tarehe 31 Mei hadi tarehe 11 Juni 2010.

Alieleza kuwa, mkutano huo ulitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwa ni pamoja na tafsiri ya kosa la uchokozi (crime of aggression). Maelezo yaliyotolewa na wataalamu kuhusu kosa hilo ni mazuri na yanajitosheleza. Aidha, nchi nyingi wanachama wa AALCO zilionesha wasiwasi kuhusu uhuru wa Mahakama hiyo na kwamba waliweka msisitizo kuwa mahakama hiyo lazima iwe huru na isiyumbishwe na msukumo wowote wa kisiasa.

Mwisho, Waziri Chikawe aligusia suala la mazingira na maendeleo endelevu. Suala hili lilijadiliwa pia katika mkutano wa Dar es Salaam kama maandalizi kwa ajili ya mkutano wa mabadiliko ya tabianchi unaotarajiwa kufanyika Cancun, Mexico mwishoni mwa mwaka 2010. Mkutano ulisisitiza umuhimu wa nchi wanachama kuwa na utashi wa kisiasa katika kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi kwa kufuata kanuni za rasimu ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya Tabianchi (UNFCCC).

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilijiunga na AALCO mwaka 1973 na tangu wakati huo inajihusisha na shughuli za jumuiya hiyo kikamilifu. Vile vile, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilishakuwa mwenyeji wa mikutano miwili ya mwaka ya AALCO. Mkutano wa 25 wa mwaka uliofanyika Arusha mwaka 1986 na mkutano wa 49 wa mwaka uliofanyika Dar es Salaam Agosti 2010.

WAANGALIZI WA UCHAGUZI KUTOKA EU NA AU WASEMA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA WA AMANI

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO

WAANGALIZI wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu uliofanyika Oktoba 31,kutoka Jumuiya ya Ulaya ( EU EOM) na Umoja wa Afrika wamesema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa huru na haki, utulivu na amani.

Waangalizi hao walitoa kauli hizo kwa nyakati tofauti wakati walipofanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana(leo) kuhusu taarifa ya awali ya uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, David Martin alisema uchaguzi huo ambao ni wa nne kufanyika nchini tangu mfumo wa vyama vingi kuanzishwa Tanzania, hadi sasa kwa ujumla umefanyika kwa amani na mpangilio mzuri.

“ Siku ya Uchaguzi Mkuu ilijitokeza kwa utulivu mkubwa na kwa ujuml a waangalizi wa uchaguzi wa Ujumbe Maaalumu wa Jumuiya ya Ulaya(EU EOM) ulikadria mchakato mzima wa uchaguzi huo kuwa ama ulikuwa ‘mzuri’ au ‘ kuridhisha’ katika asilimia 95 ya vituo vyote vya kupigia kura walivyovitembelea upande wa Tanzania Bara na upande wa Zanzibar,” alisema Martin.

Aliongeza kuwa kwa ujumla taratibu muhimu katika vituo vya kupigia kura zilitumwa kwa ulinganifu kwa kila kituo cha kupigia kura nchini kote, licha kuwepo mapungufu machache.

Martin alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) zilisimamia chaguzi kwa namna ya kitaalamu, hivyo kwa sehemu kubwa ziliwapatia watu watu wote haki ya kupiga kura.

Aliongeza kuwa ujumbe huo utabakia nchini kuzidi kufuatilia kwa karibu zaidi zoezi la kuhesabu matokeo ya uchaguzi, utangazaji wa matokeo na matukio yoyote yatakayojitokeza baada ya uchaguzi.

“Taarifa hii ni ya awali .Taarifa ya kina ya mwisho itatolewa baina ya miezi miwili na miezi mitatu baada ya mchakato mzima wa uchaguzi kukamilika,” alisema.

Kwa upande wake Kiongozi wa waangalizi hao, kutoka AU, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Sierra Leone, Dk. Ahmad Tejan Kabbah alisema uchaguzi huo umefanyika wa amani na umefanyika kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa Tanzania .

Aliongeza kuwa umefanyika kwa kuzingatia Azimia la Durban Demorasia katika Chaguzi za Afrika la Julai mwaka 2002.

“ Waangalizi wa Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi umefanyika kwa huru, haki , uwazi na uadilifu(Credible) .

Waangalizi hao ,waliwapongeza wananchi wa Tanzania, Vyama vya Siasa, wagombea , NEC, ZEC na vyombo vya usalama kwa kuwezesha uchaguzi huo ufanyike kwa amani na kuwashauri wagombea kukubali matokeo yanayotangazwa na NEC.

MPIGIE KURA LEAH MUDY ASITOKE TUSKER PROJECT FAME.








Wafuatao ni washiriki wa TUSKER PROJECT FAME 2010 4 na anayetakiwa kipigiwa kura nyingi ni Leah mwenye namba 3 hivyo watanzania tunaomba mumpigie kura nyingi Leah Mud na kumpa kwa kuandika Tusker 3 kwenda 15522 mara nyingi zaidi kadiri iwezekanzavyo jitahidini kupiga kura kwa mtanzania mwenzetu ili asitoke kwenye nyumba ya Project Fame. wiki hii.

Tusker 1 – Atete Gaelle

Tusker 2 – Thomas

Tusker 3 – Leah

Tusker 4 – Amileena

Tusker 5 – Davis

Tusker 6 – Kuonck Deng

Tusker 7 – Rachel

Tusker 8 – Elizabeth Gaga

Tusker 9 – Msechu

Tusker 10 – Steve

Tusker 12 – Aneth

Tusker 13 – Paleki

Tusker 14 – Prudence

Tusker 15 – Gabiro

BAADHI YA MAJIMBO AMBAYO TAYARI YAMESHATANGAZWA

Ubunge Tanga - Omar Noor Rashid/CCM Ubunge Busanda - Bi. Lawrencia Bukwimba/CCM Ubunge Geita - MacDonald/CCM Ubunge Nyang'wale - Hussein Nassoro/CCM Ubunge Ruangwa - Kassim Majaliwa/CCM Ubunge Lulindi - Jerome Bwanaus/CCM Ubunge Serengeti - Kebwe Stephen Kebwe/CCM Ubunge Mwibara - Alfax Lugora/CCM Ubunge Masasi - Mariam Kasembe/CCM Ubunge Makete - Dk. Binilith Mahende/CCM Ubunge Manyoni - John Chiligati/CCM Ubunge Bunda - Stephen Wassira/CCM Ubunge Morogoro Kusini Mashariki - Lucy Nkya/CCM Ubunge Bukoba Mjini - Khamis Kagasheki/CCM Ubunge Njombe Kaskazini - Deo Sanga/CCM Ubunge Njombe Magharibi - Grayson Lwenge/CCM Ubunge Morogoro Kusini - Innocent Karogoresi /CCM Ubunge Nyang'wale - Hussein Amary/CCM Ubunge Urambo Mashariki - Samwel Sitta/CCM Ubunge Kyela - Harrison Mwakyembe/CCM Ubunge Morogoro Mjini - Aziz Abood/CCM Ubunge Manyoni Mashariki - Lwanji/CCM Ubunge Mkinga - CCM Ubunge Kilosa - Mustapha Mkullo/CCM Ubunge Namtumbo - Vita Kawawa/CCM Ubunge Longido - Michael Lekule Laizer/CCM Ubunge Moshi Vijijini - Cyril Chami/CCM Ubunge Mtwara Mjini - Murji Hasinen Mohamed/CCM Ubunge Tabora Mjini - Ismal Aden Rage/CCM Ubunge Arumeru Mashariki - Jeremia Sumari/CCM Ubunge Mwanga - Jumanne Maghembe/CCM Ubunge Siha (Kilimanjaro) - Aggrey Mwanri/CCM Ubunge Chato - John Magufuli/CCM Ubunge Songea - Dk. Emmanuel Nchimbi/CCM Ubunge Bukoba Vijijini - Jasson Rweikiza/CCM Ubunge Mvomero - Amos Makalla/CCM Ubunge Kigoma Mjini - Peter Serukamba/CCM Ubunge Tarime - Nyambari Nyangweni/CCM Ubunge Babati Mjini - Chambiri Werema/CCM Ubunge Singida Mjini - Mohamed Dewji/CCM Ubunge Peramiho - Jenista Mhagama/CCM Ubunge Mpwapwa - George Tau/CCM Ubunge Mbarali - Dickson Kiruvi/CCM Ubunge Korogwe - Yusuf Nassir/CCM Ubunge Kongwa - John Ndugai/CCM Ubunge Mtwara Vijijini - Hawa Ghasia/CCM Ubunge Tandahimba - Juma Njwayo/CCM Ubunge Urambo Magharibi - Prof. Juma Kapuya/CCM Ubunge Bumbuli - January Makamba/CCM Ubunge Rorya - Lameck Airo/CCM Ubunge Sumbawanga Mjini - Aeshi Khalfan Hilal/CCM Ubunge Manyovu (zamani likijulikana kwa jina la Kasulu Magharibi) - Albert F. Ntaliba/CCM Ubunge Kwimba - Mansour/CCM Ubunge Ukerewe - Salvatory Naluyaga/CHADEMA (mshindani wa karibu Gertrude Mongella) Ubunge Ukerewe - Salvatory Naluyege/CHADEMA CHADEMA Ubunge Mbeya Mjini - Joseph Mbilinyi (Mr. II aka Sugu)/CHADEMA Ubunge Moshi Mjini - Philemon Ndesamburo Kiwelu/CHADEMA Ubunge Biharamulo Magharibi - Dk Antony Mbasa/CHADEMA Ubunge Rombo - Julius Selasini/CHADEMA (mshindani wa karibu Basil Mramba/CCM) Ubunge Nyamagana - Hezekiah Wenje/CHADEMA (mshindani wa karibu Lawrence Masha/CCM) Ubunge Iringa Mjini - Mchungaji Peter Msigwa/CHADEMA (mshindani wa karibu Monica Mbega/CCM) Ubunge Hai - Freeman Mbowe/CHADEMA Ubunge Musoma Mjini - Vincent Nyerere/CHADEMA Ubunge Arusha Mjini - Godbless Lema/CHADEMA Ubunge Kigoma Kaskazini - Zitto Kabwe/CHADEMA Ubunge Ilemela - Hayness Samson/CHADEMA Ubunge Maswa Magharibi - John Shibuda/CHADEMA Ubunge Meatu - Meshack Opulukwa/CHADEMA Ubunge Maswa Mashariki - Sylvester Kasulimbayi Mhoja/CHADEMA Ubunge Ubungo - John Mnyika/CHADEMA Ubunge Mbulu - Mustapha Quorro Akonay/CHADEMA Ubunge Karatu - Israel Yohana/CHADEMA Ubunge Lindi - Salum Barwani/CUF Ubunge Kasulu Vijijini - Zaituni Buyogela/NCCR-Mageuzi Ubunge Kasulu Mjini - Machali Moses/NCCR Mageuzi Ubunge Vunjo (Kilimanjaro) - Augustine Lyatonga Mrema/TLP UBUNGE JIMBO LA KAWE- HALIMA MDEE /CHADEMA

KURA ZA URAIS ZA BAADHI YA MAJIMBO LEO.

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: IGUNGA

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 9 0.11%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 6,111 72.88%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 112 1.34%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 1,978 23.59%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 22 0.26%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 15 0.18%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 7 0.08%

SPOILT VOTES 131 1.56%

TOTALS 8,385 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: CHONGA

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 34 0.37%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 5,731 61.94%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 204 2.20%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 2,901 31.35%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 46 0.50%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 26 0.28%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 36 0.39%

SPOILT VOTES 275 2.97%

TOTALS 9,253 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: CHAMBANI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 20 0.30%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 2,271 34.01%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 90 1.35%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 3,806 57.00%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 101 1.51%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 25 0.37%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 31 0.46%

SPOILT VOTES 333 4.99%

TOTALS 6,677 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: BUMBWINI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 9 0.18%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 624 12.79%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 49 1.00%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 3,981 81.61%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 60 1.23%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 28 0.57%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 14 0.29%

SPOILT VOTES 113 2.32%

TOTALS 4,878 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: BUBUBU

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 24 0.36%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 3,941 58.94%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 110 1.64%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 2,205 32.97%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 68 1.02%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 41 0.61%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 27 0.40%

SPOILT VOTES 271 4.05%

TOTALS 6,687 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: BAGAMOYO

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 22 0.24%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 4,720 52.06%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 88 0.97%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 3,995 44.07%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 38 0.42%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 21 0.23%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 14 0.15%

SPOILT VOTES 168 1.85%

TOTALS 9,066 100.00%

MATOKEO YA UCHAGUZI WA RAIS KWA JIMBO

JIMBO: AMANI

KUGA PETER MZIRAY APPT - MAENDELEO 203 0.97%

KIKWETE JAKAYA MRISHO CCM 15,829 75.69%

SLAA WILLIBROD PETER CHADEMA 2,364 11.30%

LIPUMBA IBRAHIM HARUNA CUF 1,861 8.90%

RUNGWE HASHIM SPUNDA NCCR-MAGEUZI 32 0.15%

MGAYWA MUTTAMWEGA BHATT TLP 18 0.09%

DOVUTWA YAHMI NASSORO DOVUTWA UPDP 29 0.14%

SPOILT VOTES 576 2.75%

TOTALS 20,912 100.00%

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA