Oct 6, 2010

VING'AMUZI VYA STAR MEDIA SASA NI SHILINGI ELFU 60.000!!

Mkurugezni Mtendaji wa Star Media Tanzania Limited akionyesha kwa waandishi wa habari kipeperushi kinachoonyesha ofa maalum iliyotolewa na kampuni hiyo ambapo ving'amuzi wa vya Star Media sasa vinapatikana kwa shilingi elfu 60.000 huku ukiunganishwa moja kwa moja na matangazo ya kituo hicho. Bw. Charles Liu amesema wana mpango wa kuongeza vituo vitatu vya hapa nyumbani kwenye mtandao wa ving'amuzi vyao ambapo wataongeza chaneli mbili za dini ya Kiislamu na ya Kikristo na nyingine ya habari za Kijamii ili kuwavutia zaidi watanzania wengi kujiunga nha kampuni yao. Kampuni hiyo ina wateja elfu 60.000 mpaka sasa toka ilipoanzishwa na inaendelea kuigiza wateja zaidi kwa ajili ya kujipatia huduma yao, katika picha kushoto ni Meneja Masoko Msaidizi wa kampuni hiyo David Mwijage.

Amesema hili ni tamasha ambalo huwa linafanywa na kampuni yetu kama sehemu ya utamaduni, na huwa inaambatana na mambo mengi sana yatayo mfanya mteja wetu kuwa karibu na Star Times.

Mwezi huu wa October tumeandaa promotion kubwa sana ambayo ina mambo yatakayo mfaidisha mteja kwa namna moja au nyingine. .

Baadhi ya mambo hayo ni:

1.Kwanza kwa kutaka kukidhi kiu ya burudani na habari mbalimbali kwa wateja wetu tumeongeza channel mpya ikiwemo BOLLYWOOD TV kwa wale ambao ni wa wapenzi wa filamu za kihindi, stori za maisha yao na tamaduni zao kwa ujumla huu ndo wakati wa kufurahia channel hii.

Pia tumeongeza chanell za E-star na Real star ambazo nazo pia zinaonesha burudani mbalimbali ikiwemo filamu kutoka afrika kama Nigeria na sehemu nyingine.. na channel nyingine ni MSNBC ambayo ni channel ya kimarekani hii inaonesha zaidi habari mbalimbali na matukio yanayoendelea kutoka sehem mbalimbali.

2. Pili Star Times imetoa punguzo kubwa la bei ndani ya mwezi huu wa kumi ambapo

Dikoda/ king’amuzi kilichokuwa kikiuzwa kwa 70000/= tsh sasa kinapatikana kwa

60000/= unaweza ukaona ni karibia 14% iliyopunguzwa hapo.

Pia digital TV zitauzwa kwa bei pungufu ukilinganisha na wakati mwingine ambapo bei imeshushwa kwa 12%.

NO BIDHAA BEI YA KAWAIDA BEIYA PROMOSHENI
1. Digital TV 21 inch 250,000/= tsh 220,000/= tsh
2. Digital Tv 26 inch 570,000/= tsh 500,000/= tshs
3. Digital Tv 32 inch 800,000/= 700,000/= tshs

3. Tatu ili kuepusha usumbufu kwa wateja wetu Star Times imeamua kuanza kuuza vocha zake za kulipia bill ya mwezi katika maduka madogo madogo yatayokuwa yanapatikana kila sehemu ili kumfanya mteja awe karibu na huduma zetu. Kwahiyo hii ni mojawapo ya ajira ambayo Star Times itatoa kwa vijana wengi wataokuwa tayari kuwa ma delers au wawakilishi wa kampuni yetu katika sehemu mbalimbali.

4. Na mwisho tuna mkakati wa kuandaa tamasha litalokutanisha watu mbalimbali wakiwemo wajasiriamali, wanamichezo na watu wa tasnia mbalimbali kuwa pamoja katika Star Times DIGITAL FESTIVAL..hili tutawajulisha litakapokuwa limekamilika..

MAHALI: TBCI Star Times Shop.

Injinia Aisha Masoud Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akiendelea na kazi yake kwenye mitambo ya kampuni hiyo inayorusha matangazo ya vituo mbalimbali duniani kwa kutumia ving'amuzi vya kulipia.
Hawa ni baazi wa wateja wakipata hudumaza kulipia ving'amuzi vyao katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo kwenye ofisi za TBC1 Mikocheni.
Mkurugenzi mtendaji wa Star Media Tanzania Limited Bw. Charles Liu akiwaonyesha waandishi wa habari mitambo mbalimbali ya kampuni hiyo inayorusha matangazo wakati wanahabari walipotembelea kituo hicho kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kituo hicho.
Mkurugenzi wa kampuni ya Star Media Tanzania Limited Bw. Charles Liu akionyesha kifaa mtambo wa kurushia matangazo ya kituo hicho kinachojihusha na kurusha matangazo kwa kutumia Ving'amuzi nchini kwa kulipia. kulia ni Meneja masoko msaidizi wa kampuni hiyo David Mwijage.
Waandishi wa habari wakipewa viatu maalum vya kuzuia vumbi na mfanyakazi wa kampuni hiyo Inijinia Aisha Masoud wakati walipokuwa wakitembelea katika chumba cha kuongozea matangazo.
Wafanyakazi wa Star Media Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja ofisini kwao leo.

DK GHALIB BILAL AUNGURUMA MKOANI TANGA

Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya Tanga mjini, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Tangamano jana, uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote. (Picha na Muhidin Sufiani)
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na mkewe Bi Asha Bilal, wakati wakiwa ndani ya Kivuko cha Pangani walipokuwa wakivuka kutoka Kijiji cha Mwela kuelekea Pangani mjini jana okt 5.
Wananchi wa Manispaa ya Tanga mjini, wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Tangamano jana okt 5.
Wananchi wa Manispaa ya Tanga mjini, wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi hao katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Tangamano jana okt 5.

WAZIRI MKUU AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO UGANDA!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya watanzania wanaosomama kwenye Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala wakati alipozungumza na watanzania waishio Uganda kwenuye Ubalozi wa Tanzania Mjini Kampala Oktoba 6 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pindana Mkewe Tunu wakisalimiana na baadhi ya watanzania waishio nchini Uganda kabla ya kuzungumza nao kwenye ubalozi wa Tanzani Mjini Kampala
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda akizungumza katika Mkutano wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) na Watanzania waishio nchini Uganda uliofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania Mjini Kampala Oktoba 5, 2010. Kushoto ni Mke wa Kaimu Balozi wa Tanzani nchini Uganda, Naomi Ndatta.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANGAZO LA KAZI

JAMHURI YA MUUNGANO TANZANIA

WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII

Serikali inaendelea kufanya maboresho ya Sekta ya Afya kupitia Mpango wa Maendeleo ya Afya ya Msingi (MMAM) ikiwa ni pamoja na kuongeza vituo vya kutolea huduma, kuongeza idadi ya watumishi pamoja na kuboresha maslahi ya watumishi. Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ametoa Kibali cha Ajira kwa Wataalam wa Kada za Afya 7,471 kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ili kutekeleza azima hii; Katibu Mkuu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, anapenda kuwatangazia wale wote wenye taaluma zifuatazo:-

Madaktari, Wafamasia, Maafisa Wauguzi, Wauguzi, Maafisa Afya, Wateknolojia wa Maabara/Mionzi/Dawa, Maafisa Tabibu na Matabibu Wasaidizi kwamba, Wizara ipo tayari kuwapangia kazi.

Wahitimu waliofuzu Mafunzo ya Afya, katika mwezi Julai, 2010 pamoja na Matabibu Wasaidizi waliohitimu Oktoba, 2009 watapangiwa kazi moja kwa moja na hawatalazimika kutuma maombi. Majina ya waliopangiwa vituo vya kazi yatatangazwa kwenye Magazeti na Tovuti ya Wizara www.moh.go.tz. Pia Wahusika watatumiwa barua za kupangiwa kazi katika anuani zao za posta, na kwa waajiri wao watakakopangiwa.

Aidha, Waombaji wengine wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu kwa kutumia Anuani iliyotajwa hapa chini. Muombaji anatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:-

    1. Awe ni raia wa Tanzania.
    2. Awe na umri usiozidi miaka 45.
    3. Wale wenye umri wa miaka zaidi ya 45 wataajiriwa kwa Mkataba baada ya kuombewa Kibali kutoka kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.

Waombaji wanashauriwa kupendekeza Halmashauri tatu ambazo wangependa kupangiwa kazi. Hata hivyo Wizara itatoa kipaumbele zaidi kwa Halmashauri zilizopo nje ya Dar es Salaam, na upangiwaji wa vituo utategemea uwepo wa nafasi wazi katika Halmashauri hizo.

Maombi yote yaambatanishwe na:-

  1. Nakala ya Cheti cha Taaluma
  2. Nakala ya Cheti cha Kidato cha nne/sita
  1. Maelezo binafsi (CV) ikijumuisha anuani kamili, umri na namba ya simu ya kiganjani.
  2. Picha (Passport size mbili) za hivi karibuni
  3. Nakala ya Cheti cha usajili kutoka baraza la taaluma husika.

Vyeti vyote vya Taaluma na Kidato cha nne/sita vithibitishwe na Hakimu au Wakili.

Barua zote zitumwe kwa:-

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

S.L.P. 9083,

DAR ES SALAAM.

Tangazo hili linapatikana katika tovuti yetu

www.moh.go.tz

R.I.P dada yetu leticia kaijage



Marehemu Leticia Kaijage enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa katika Msiba Tabata Segerea nyumbani kwa kaka wa marehemu.
Waombolezaji ambao baadhi yao walifanya kazi pamoja na Marehemu katika Kampuni za PR wakiwa msibani.
Jamaa na marafiki wa marehemu
Sanduku lililouhifadhi mwili wa Marehemu Leticia likiwa tayari kwa misa maalum ya kumuombea.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Marafiki wa marehemu,Celine Njuju na Betrice Singano walishindwa kujizua na kujikuta wakibubujikwa na machozi kwa huzuni ya kuondokewa na mwenzi wao.
waombolezaji wakibeba sanduku tayari kwa safari ya kwenda Kijiji cha Nyakigando Kata ya Kaibanja Wilaya ya Bukoba Vijijni ambako mwili wa marehemu utahifadhiwa katika nyumba yake ya Milele Oktoba 7,2010.
Mwili ukiingizwa katika gari na baadhi ya waombolezaji tayari kwa safari ya kwenda uwanja wa ndege ili kuweza kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kijijini kwao Nyakigando Kata ya Kaibanja Wilaya ya Bukoba Vijijni kwa mazishi.
Gari likiwa tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Amina.picha zimepigwa na mdau Father Kidevu aliekuwepo bega kwa bega katika msiba huo.

StarTimes yapunguza gharama za ving'amuzi vyao


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Charles Liu(kushoto) akionyesha mitambo inayotumiwa na kampuni hiyo kurusha matangazo kwa njia ya dijitali ili kuwawezesha wananchi wengi kuachana na teknolojia ya kale ya analogia. Kushoto ni Afisa Masoko Davis Mwijage.


Kampuni inayotamba kwa ving’amuzi vya bei rahisi na iliyosambaa ulimwenguni na Africa kwa ujumla (Star Times) imezindua tamasha la uuzaji wa ving’amuzi vyake leo jijini Dar-es-salaam sambamba na kutangaza kuwa wameongeza channel zaidi kukidhi haja ya watanzania.

Akizindua tamasha hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo bwana Charles Liu amesema kampuni yao imesambaa kwenye nchi 9 za Africa zikiwema Tanzania, Uganda, Rwanda, Guinea, Cote de voire na nyinginezo .

Tamasha hilo limeambatana na punguzo la bei kwa 14% kwa king’amuzi kija na pia punguzo kubwa kwa television za kisasa ambazo zimeunganishwa moja kwa moja na king’amuzi hicho.

‘Tumetoa punguzo kubwa la bei ndani ya mwezi huu wa kumi na pia tumeongeza chanel za E-star na Real ambazo zinaonesha burudani mbalimbali ikiwemo filamu kutoka Nigeria na sehemu nyingine” Aliongeza Liu.

Mbali na hayo pia kampuni hiyo imepanua huduma zake katika mikoa mingi ya Tanzania ambapo vituo vimefunguliwa Dodoma, Mwanza,Arusha , Mbeya na Moshi pia kuepusha usumbufu kwa wateja, wameamua kuuza vocha zake za kulipia bili ya mwezikatika maduka madogo yatakayopatokana kila sehemu.

Bwana Liu alizitaja baadhi ya chanel zinazopatikana kuwa ni MSNBC,Nood Tv,Fashion Tv, Discovery world,Nickeledeon kwa ajili ya watoto, MTV base, ANIMAX, Kidsco na nyingine nyingi. Pia wameanzisha utaratibu wa kutoa huduma kwa wateja kwa njia ya simu kwa masaa 24.

WASANII WATAKIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU YA KAZI ZAO

Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego yeye alisema kwamba uhifadhi wa kazi za sanaa ni muhimu kwa wasanii kwani ni nyenzo ya kurithisha sanaa kwa vizazi vijavyo na kujua maendeleo ya tasnia hii.

Wasanii wa Muziki Kizazi kipya wakifurahia jambo baada ya kuahirishwa kwa Jukwaa la Sanaa.Kutoka Kulia ni Dar Shopper,Mzee Nkwama Bhalanga,Mtoto wa Kitaa,Gheto King na Yuda Skills.

Wasanii wametakiwa kutunza kumbukumbu ya kazi zote wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za kazi za sanaa za kale ili kuchota ujuzi wa kale na kuboresha sanaa wanazozifanya.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa,Dkt Paul Msemwa wakati akiwasilisha mada yake kuhusu ‘Uhifadhi wa Sanaa za Asili na Changamoto Zake’ kwenye Jukwaa la Sanaa, linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kukutanisha wadau wengi wa sanaa.

Alisema kwamba uhifadhi wa kazi za sanaa ni muhimu sana kwani ndiyo chanzo kikubwa cha kujua ni kwa kiwango gani sanaa imebadilika na ni kwa jinsi gani wasanii wataweza kutumia kazi za kale za sanaa katika kuboresha zile wanazozizalisha sasa.

Aliongeza kwamba, sanaa haiwezi kukua kama wasanii watakuwa ni wa kujifungia ndani ya boksi na kubuni vitu vyao bila kutaka kutafiti na kujifunza sanaa za kale zilivyokuwa ili nao waweze kuboresha na kuongeza vionjo kulingana na nyakati tulizonazo sana.

“Ukuzaji wa Sanaa huanza na kujua wengine wanafanya nini halafu ukishajua sasa unaweza kuongeza vionjo na ubunifu kulingana na nyakati zilizopo lakini pia uhitaji wa soko la kazi za sanaa” Alisisitiza Dkt.Msemwa.

Aliyataja matatizo ambayo yanasababishwa na wasanii kutokutunza kumbukumbu ya kazi zao kuwa ni pamoja na kazi zao kutokuthaminiwa,kuuzwa kwa bei za chini,kuibiwa hakimiliki, kuharibiwa, kutoroshwa nje ya nchi pasi na mtu kujali na wasanii kushindwa kujua tarehe na muda kazi zao ziliozalishwa.

Sakata la wasanii hususan wa muziki kupuuzia kutunza kumbukumbu ya kazi zao liliibuka Kwenye Jukwa la Sanaa mwezi mmoja uliopita wakati Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akiwasilisha mada yake Kuhusu ‘Mwelekeo wa Tunzo za Muziki Tanzania na Changamoto Zake’ ambapo alisema kwamba, wasanii wamekuwa hawatunzi kumbukumbu za kazi zao hali ambayo imekuwa ni changamoto katika uingizaji wa nyimbo zao kwenye tunzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Music Awards).

Mbali na kuwashauri wasanii kujenga utamaduni wa kuhifadhi kazi zao, aliwashauri kutembela hifadhi za sanaa za kale na kazi zingine za utamaduni ili kujijenga kisanii na kupata kujifunza sanaa za kale zilivyokuwa zinaendeshwa ili sasa waweze kupata pa kuanzia.

Kwa uapande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, utunzaji wa kazi za sanaa ni muhimu sana kwani ndiyo njia pekee ya kuirithisha sanaa kwa vizazi vijavyo.Aliongeza kwamba, lazima kuwepo na utaratibu wa wasanii kuhifadhi kazi zao ili kuhakikisha hazipotei na kusahaulika.

Wadau wengi waliochangia kwenye Jukwa la Sanaa waliishauri serikali kuanzisha Hifadhi za Kazi za Sanaa na Utamaduni katika ngazi mbalimbali za wilaya na mikoa badala ya ilivyo sasa ambapo hupatikana katika maeneo machache.Walisema kwamba, maafisa utamaduni wapewe kazi ya kuratibu zoezi hili ili kufufua utamaduni.

Jukwaa la Sanaa litaendelea tena wiki ijayo na wadau wa sanaa kama kawaida watakuwepo kujadili masuala mbalimbali yahusuyo tasnia hii.

Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,
Alistide Kwizela

MGOMBEA MWENZA DK GHALIB BILAL AINGIA MKOANI TANGA!!

Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dk. Mohamed Gharib akifurahia jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Handeni Abdallah Kigoda baada ya kupokelewa mpakani mwa Wilaya ya Bagamoyo na Handeni leo
Mgombea Mwenza wa Urais kupitia CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na wazee wa Kijiji cha Manga Wilaya ya Bagamoyo wakati aliposimama njiani kuwasalimia na kuzumngumza na wananchi wa kijiji hicho alipokuwa njiani kuelekea mkoani Tanga leo
Mgombea Mwenza wa Uraiskupitia CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kwa Msisi Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga, wakati akiwa safarini kelekea Mkoani Tanga leo

MAPOKEZI YA DK. GHALIB BILAL BAGAMOYO JANA

Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal kulia akimnadi mgombea ubungea wa Jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana jioni. (Picha na Muhidin Sufiani)
Katibu wa CCM Mkoa wa Pwani, Sauda Mpambaliyoto na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Bagamoyo, Shukuru Kawambwa, wakisakata ngoma na msanii wa kikundi cha Sprendid wakati wa hafla ya mkutano huo jana
Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia ngoma ya asili ya Kikundi cha Sanaa cha Sprendid cha Bagamoyo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Shule ya Msingi ya Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana Okt 4, alipofika kufanya mkutano wa kampeni n kuanadi wagombea ubunge Shukuru Kawambwa waJimbo la Bagamoyomo na Amour Abuu Jumaa wa Jimbo la Kibaha Vijijini.
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM Dk. Mohamed Gharib Bilal na mkewe Asha Bilal, wakiingia kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni Wilaya ya Bagamoyo jana Okt 4, kufanya mkutano wa kampeni.
Dk Ghalib Bilal akiwapungia mkono kuwasalimia wananchi waliojitokezza kwenye mapokezi hayo mjini Bagamoyo jana.
Msafafa wa waendesha Pikipiki ukimpokea Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwasili Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana Sept 4 kwa ajili ya kufanya mkutano wa uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Majengo Kata ya Magomeni.

RAIS JAKAYA AMTEUA PROFESA WANGWE KUWA MWENYEKITI WA BODI


















Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Profesa Samwel Wangwe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.

Taarifa iliyotumwa Kwa vyombo vya habari kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali za Mitaa Bibi Maimuna Tarishi imesema Profesa Wangwe ameteuliwa kutokana na Sheria aliyopewa Rais Kikwete katika Sheria ya Mashirika ya umma namba 17 ya mwaka 1969

Sambamba na uteuzi wa Profesa Wangwe,Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda pia amewateua Wakurugenzi wa Bodi ya Shirika la Elimu Kibaha.

Kutokana na Mamlaka aliyopewa Waziri Mkuu katika Sheria ya Umma namba 17 ya mwaka 1969 wakurugenzi wa bodi walioteuliwa ni pamoja na Bibi Fatma Kiongosya ambaye ni Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Uchumi,Dr Magreth Mhando,Mwakilishi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.

Wengine ni Bibi Salock Musese kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Bwana Apenda William Mrinji,kutoka Wizara ya Kilimo,Chakula na Ushirika na Bibi Halima Kihemba ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha.

Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi pamoja na Wakurugenzi hao umeanza rasmi tarehe 1/9/2010 na itamaliza muda wake tarehe 31/08/2013

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHUDHURIA MKUTANO WA MILLENIA KAMPALA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakati Rais huyo alipofungua Mkutano wa Kimataifa wa Kujadili Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia kwenye Serikali za Mitaa uliofanyika kwenye hoteli ya Serena Mjini Kampala Oktoba 6, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda baada ya Rais huyo kufungua Mkutano wa Kimataifa wa kujadili Utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia kupitia Serrikali za Mitaa kwenye Hoteli ya Serena Kampala Oktoba 6, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizunguza na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mamlaka za Serikali za Mitaa la Kenya (Local Government Authorities of Kenya), Bw. Tarayia Ole Kores katika Mkutano wa kimataifa wa Kujadili utekelezaji wa malengo ya Maendeleo ya Millenia kupitia Seriklai za Mitaa, Ulipofunguliwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwenye Hoteli ya Serena Kampala, Oktoba 5, 2010.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Kikwete katika maadhimnisho ya siku ya mwalimu mjini Songea,Afungua jengo la kitega uchumi la Chama Cha Waalimu!!

Rais Jakaya mrisho kikwete akikata utepe kufungua rasmi jingo la Chama Cha waalimu Tanzania Mkoa wa Ruvuma leo asubuhi mjini Songea.Wapili kushoto ni Rais wa Chama Cha waalimu Tanzania Bwana Gratian mkoba na watatu kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Maghembe.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watoto waliomlaki muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa songea ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimnisho ya sherehe ya siku ya mwalimu duniani.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Samora mjini Songea mkoani Ruvuma akimkaribisha Rais Dr.Jakaya Kikwete kwa saluti maalumu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufungua rasmi jingo la Chama Cha waalimu mkoa wa Ruvuma leo asubuhi(picha na Freddy Maro)

Baadhi ya waalimu waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani wakiingia kwa maandamano katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea ambapo Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete alikuwa mgeni rasmi na kuwahutubia.
Baadhi ya waalimu waliohudhuria sherehe za siku ya mwalimu duniani wakimsikiliza Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete alipowahutubia katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea.Rais Dr.Kikwete alikuwa mgeni ramsi katika maadhimisho hayo kwa mwaliko wa Chama cha Waalimu Tanzania(picha na Freddy Maro)


Mgombea Ubunge Jimbo la Hanang Kupitia CHADEMA-Rose Kamili Sukum

Rose Kamili Sukum, Mgombea wa Ubunge Jimbo la Hanang kupitia CHADEMA akiwa katika mkutano wake wa kuomba ridhaa kwa wananchi Kata ya Endagaw.
Baadi ya wananchi wakimsikiliza Mgombea ubunge wa Jimbo la Hanang Rose Kamili Sukum anayegombea kupitia kupitia Chama Cha CHADEMA wakati alipokuwa akiwahutubia.

Ridhiwani Kikwete akiwa katika mji wa Rufiji!!

Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani
Kikwete,akivishwa skafu chipukizi baada ya kuwasili wilayani
Rufiji jana, kuanza kampeni mkoani Pwani ya kuweka mikakati
ya ushindi wa kishindo kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba 31, Mwaka huu nchini. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Mzee Kada wa CCM,Salum Mwegio akiwaombea dua wagombea ubunge
na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wanaowania nafasi
hizo, baada ya Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu
la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,
Ridhiwani Kikwete, kuwanadi mjini Uteta, Rufiji juzi, wakati
wa kampeni za ndani za kuweka mikakati ya ushindi wa Align Center
kishindo kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, Mwaka
huu nchini
Wazee makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakimlaki Mjumbe
wa Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Ridhiwani
Kikwete,alipowasili mjini Utete, Rufiji jana, kufanya
kampeni ya kuweka mikakati ya ushindi wa kishindo kwa CCM
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, Mwaka huu nchini.
Sehemu ya umati wa wanaCCM, ukiwa katika mkutano wa kampeni
uliohutubiwa na Mjumbe a Kamati ya utekelezaji ya Baraza Kuu
la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa,
Ridhiwani Kikwete,mjini Utete, Wilaya ya Rufiji juzi.

Oct 4, 2010

WASANII WATAKIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU YA KAZI ZAO!!

Wasanii wametakiwa kutunza kumbukumbu ya kazi zote wanazozifanya ikiwa ni pamoja na kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za kazi za sanaa za kale ili kuchota ujuzi wa kale na kuboresha sanaa wanazozifanya.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa,Dkt Paul Msemwa wakati akiwasilisha mada yake kuhusu ‘Uhifadhi wa Sanaa za Asili na Changamoto Zake’ kwenye Jukwaa la Sanaa, linalofanyika kila Jumatatu kwenye Ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kukutanisha wadau wengi wa sanaa.

Alisema kwamba uhifadhi wa kazi za sanaa ni muhimu sana kwani ndiyo chanzo kikubwa cha kujua ni kwa kiwango gani sanaa imebadilika na ni kwa jinsi gani wasanii wataweza kutumia kazi za kale za sanaa katika kuboresha zile wanazozizalisha sasa.

Aliongeza kwamba, sanaa haiwezi kukua kama wasanii watakuwa ni wa kujifungia ndani ya boksi na kubuni vitu vyao bila kutaka kutafiti na kujifunza sanaa za kale zilivyokuwa ili nao waweze kuboresha na kuongeza vionjo kulingana na nyakati tulizonazo sana.

“Ukuzaji wa Sanaa huanza na kujua wengine wanafanya nini halafu ukishajua sasa unaweza kuongeza vionjo na ubunifu kulingana na nyakati zilizopo lakini pia uhitaji wa soko la kazi za sanaa” Alisisitiza Dkt.Msemwa.

Aliyataja matatizo ambayo yanasababishwa na wasanii kutokutunza kumbukumbu ya kazi zao kuwa ni pamoja na kazi zao kutokuthaminiwa,kuuzwa kwa bei za chini,kuibiwa hakimiliki, kuharibiwa, kutoroshwa nje ya nchi pasi na mtu kujali na wasanii kushindwa kujua tarehe na muda kazi zao ziliozalishwa.

Sakata la wasanii hususan wa muziki kupuuzia kutunza kumbukumbu ya kazi zao liliibuka Kwenye Jukwa la Sanaa mwezi mmoja uliopita wakati Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akiwasilisha mada yake Kuhusu ‘Mwelekeo wa Tunzo za Muziki Tanzania na Changamoto Zake’ ambapo alisema kwamba, wasanii wamekuwa hawatunzi kumbukumbu za kazi zao hali ambayo imekuwa ni changamoto katika uingizaji wa nyimbo zao kwenye tunzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Music Awards).

Mbali na kuwashauri wasanii kujenga utamaduni wa kuhifadhi kazi zao, aliwashauri kutembela hifadhi za sanaa za kale na kazi zingine za utamaduni ili kujijenga kisanii na kupata kujifunza sanaa za kale zilivyokuwa zinaendeshwa ili sasa waweze kupata pa kuanzia.

Kwa uapande wake Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Materego alisema kwamba, utunzaji wa kazi za sanaa ni muhimu sana kwani ndiyo njia pekee ya kuirithisha sanaa kwa vizazi vijavyo.Aliongeza kwamba, lazima kuwepo na utaratibu wa wasanii kuhifadhi kazi zao ili kuhakikisha hazipotei na kusahaulika.

Wadau wengi waliochangia kwenye Jukwa la Sanaa waliishauri serikali kuanzisha Hifadhi za Kazi za Sanaa na Utamaduni katika ngazi mbalimbali za wilaya na mikoa badala ya ilivyo sasa ambapo hupatikana katika maeneo machache.Walisema kwamba, maafisa utamaduni wapewe kazi ya kuratibu zoezi hili ili kufufua utamaduni.

Jukwaa la Sanaa litaendelea tena wiki ijayo na wadau wa sanaa kama kawaida watakuwepo kujadili masuala mbalimbali yahusuyo tasnia hii.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA