Oct 4, 2010

KAMPENI YA SHANGILIA TAIFA STARS YAZINDULIWA LEO!!

Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu nchini Rodger Tenga akizungumza katika uzinduzi wa kampeni ya Shangilia taifa Stars iliyozinduliwa leo kwenye soko la Karume jijini Dar es salaam kulia ni Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano Mh Mohammed Seif Khatib na kushoto ni Meneja Mkuu Mwasiliano na Uhusiano wa Serengeti Breweriers Limited. Timu ya taifa inatarajiwa kucheza na timu ya taifa ya Moroco siku ya jumamosi kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, na mchezo huo utaonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha SuperSport.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano Bw. Mohamed Seif Khatib akibandika Stika kwenye bendera ya taifa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Shangilia timu ya taifa Taifa Stars uliofanyika kwenye soko la Karume leo.
Kocha wa timu ya Taifa Jean Paulsen naye akibandika stika kwenye bendera ya taifa kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni hiyo.
Wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars wakibandika Stika na kusaini saini zao kwenye bendera ya taifa.
Meneja Mkuu Mwasiliano na Uhusiano wa Jamii Serengeti Breweriers Teddy Mapunda kulia na Meneja Bidhaa wa Serengeti Breweriers Nandi Mwiyombea Kushoto wakifurahia jambo kwa kupiga makofi mara baada ya kuzindua kampeni ya Shangilia Taifa Stars leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Rodger Tenga wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu Mawasiliano na Uhusiano wa Jamii wa Serengeti Breweriers Teddy Mapunda katikati mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya Shangilia Taifa Stars kwenye soko la Karume leo kushoto ni Kocha Mkuu wa timu ya Taifa Jean Paulsen na kulia ni Meneja bidhaa wa FRerengeti Breweriers Nandi Mwiyombela.
Wachezaji wa timu ya Taifa wakiwa jukwaani katika uzinduzi huo.
Mmoja wa maafisa wa kampuni ya bia ya Serengeti Lutufyo Mwalusamba akitafuta taswra ya picha ya wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars katika uzinduzi huo wa kampeni ya kushangilia timu ya taifa.
Mashabiki mbalimbali wa mpira wa miguu wakiwa katika soko la Karume mahali ambapo leo Kampuni ya Bia ya Serengeti imezindua kampeni ya kuishangilia timu ya Taifa Taifa Stars kwa ajili ya kuishagilia mara itakapocheza na timu ya Moroco Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa.

taarifa ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto 2009/10 yazinduliwa leo


Mtakwimu kutoka Banki ya Dunia Bw. Thomas Danielewitz akipokea taarifa za awali za utafiti wa Afya ya uzazi na mtoto ya mwaka 2010 kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi. Blandina Nyoni akiongea na wadau mbalimbali wa takwimu na sekta ya Afya wakati wa kufunga shughuli za uzinduzi wa taarifa za awali za utafiti wa Afya ya uzazi na mtoto ya mwaka 2010 leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya ya uzazi ili kutimiza lengo la 4 la milenia na kupunguza vifo vya watoto wadogo.Picha na Aron Msigwa.

***** ****** **********

Na Mary Kweka,Dar Es Salaam.

TAARIFA ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa 2009/10 imebaini kuwa vifo vya akina Mama vitokanavyo na uzazi na watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua kwa kiwango kikubwa.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi Blandina Nyoni wakati alipokuwa akizindua taarifa za awali za utafiti wa afya ya uzazi na mtoto Jijini Da Es Salaam.

Bi Nyoni alisema takwimu zinaonyesha kuwa katikati ya miaka ya tisini vifo vya watoto wadogo chini ya miaka mitano vimepungua kwa asilimia 40 kutoka vifo 137 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai hadi vifo 81 kwa kila watoto 1000 waliozaliwa hai kwenye kipindi cha miaka ya 2006-2010.

Aidha alisema kwa upande wa vifo vya akina Mama vinavyotokana na matatizo ya uzazi vimepunua kwa asilimia 21, hii ni kutoka vifo 578 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa hai kwa kipindi cha mwaka 2004-05 hadi vifo 454 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa hai kwa mwaka 2009-2010.

“Katika hatua hii pamoja na kuonekana kuwa Tanzania tumepunguza vifo vya watoto ambavyo ni lengo la nne la maendeleo ya milenia jitihada zinahitajiaka zaidi kufikia lengo namba tano la milenia ambalo linasisitiza kuboresha afya ya uzazi”alisema Bi Nyoni.

Pamoja na mafanikio hayo, Bi. Nyoni alisema mfumo wa ukasanyaji takwimu za Afya bado unakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo jinsi ya kupunguza vifo vya akina mama vinavyotokana na uzazi kwa kuboresha huduma kwa akina Mama wajawazito na huduma ya afya.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, changamoto nyingine ni pamoja na kupunguza vifo vya watoto wadogo, mijini na vijijini ili kuhakikisha kuwa watotowote hawapotezi maisha utotoni.

Alitoa wito kwa kuwaomba wadau wote hasa wale wanaoisaidia sekta ya afya kutumia kwa ukamilifu taarifa zinazotokana na utafiti huu wa Afya ya uzazi na mtoto kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini.

Pia Bi. Nyoni ameihimiza jamii kutumia takwimu hizo kwa ajili ya mipango bora na utekelezaji wa programu mbalimbali za afya katika ngazi zote za utawala kwa ajili ya mipango ya maendeleo ili kuboresha maisha ya watanzania wote.

Utafiti huu umefanywa na kuandaliwa na kikundi cha wataalamu wakiwemo Tanzania and Demographic and Health Survey Technical Working Group, wakishirikiana na Wizara ya Afya, Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wafanyakazi wa Serikali katika ngazi mbalimbali.

haya ndio mambo ya KILI BSS 2010


Mkoko wa maana unaotumiwa na washiriki wa BSS 2010 ukiwa umepaki nje ya mjengo wao uliopo maeneo ya Mikocheni,jijini Dar
Hivi ndivyo lionekanavyo jumba linalotumiwa na washiriki wa Kili Bongo Star Search 2010 chini ya udhamini mkuwa wa kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager, ambapo mpaka sasa washiriki ishirini wapo ndani ya mjengo huu na watakaa mpaka mashindano BSS yatakapo malizika kwa mwaka huu.

MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA AFUNGUA SEMINA YA SHERIA YA GHARAMA ZA UCHAGUZI!!

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa akifungua rasmi semina ya vyombo vya habari juu ya Sheria ya Gharama za Uchaguzi inayofanyika kwenye Hotel ya Markham iliyoko Msasani jijini Dar es salaam ambayo inashirikisha vyombo mbalimbali vya habari. Msajiri amesema vyombo vya habari visione kama ofisi yake imechelewa sana kutoka semina hiyo hapana hii inatokana na kwamba ofisi yake iliona ni vyema iawapa semina kwamba wale ambao ndiyo wachezaji wa mchezo huo yaani vyama vya Siasa na wagombea wazijue kwanza sheria hizo ndipo sasa wadau wengine waendelee kuzifahamu. Uchaguzi Mkuu waRais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini kote, wengine katika picha kulia ni Zakia Stefano mwanasheria ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na kushoto ni Abraham Nyantori Afisa Mwandamizi Idara ya Habari Maelezo Dar es salaam.
Mwanasheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Zakia Stefano akitoa maelekezo kwa maafisa wengine wa ofisi hiyo wakati wa semina ya sheria ya gharama za uchaguzi kwa vyama vya Siasa inayotolewa leo kwa vyombo vya habari.
Kutoka kushoto ni Haika Belinda Macha, Joyce J. Msofe na Nyangi G. Wambwa wanasheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa wakiwa katika Semina hiyo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia semina hiyo inayoendelea sasa kwenye hoteli ya Markham jijini Dar es salaam.
Waratibu wa Semina hiyo kutoka kulia ni Ibrahim Muwawa Msaidizi wa Msajili wa Vyama vya Siasa na Martin Mung'ong'o Mratibu wa Semina hiyo
Mratibu wa Semina hiyo Bw. Martin Mg'ongo akigawa vipeperushi vya sheria ya gharama za uchaguzi kwa vyama vya siasa.
Wanahabari waliohudhuria katika semina hiyo kutoka kulia ni Louis Kolumbia Hits FM Zanzibar, Gresimo Bambaza Pride FM Mtwara, Winfrida Emmanuel Mzalendo, Peter Orwa kutoka Uhuru na Mzalendo.
Kutoka kulia Manka Mnuo kutoka Upendo Radiao Herieth Ben Mtanzania na Winfrida Ngonyani kutoka Mtanzania.

Chama Cha Mapinduzi Msisiri B watamba ushindi wa kishindo!!









CHAMA cha Mapinduzi (CCM) tawi la Msisiri B, ngome ya Chama cha Wananchi CUF, kimetamba kuibuka na ushindi wa kishindo kuanzia urais, ubunge na udiwani.

Tambo hizo zilitolewa jana katika uwanja wa Msisiri B, kwa Igumila wakati wa mkutano wa kampeni ya kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge, ambapo alihutubia wakazi wa maeneo hayo na kuwaomba wampatie ushindi yeye pamoja na wagombea wa CCM ili wapate maendeleo waliyoyakosa kwa kipindi kirefu.

Songoro alisema mwaka huu wagombea wa vyama vya upinzani wasahau kupata uongozi katika mtaaa huo kwa sababu katika kipindi walichoongoza hawajaweza kuleta maendeleo yaliyokuwa yakihitajika na wananchi ambao sasa wameonyesha dhamira ya kuichagua CCM.

Songoro aliwataka wana CCM kuachana na uvumi wa wapinzani juu ya machafuko ya kimapinduzi na badala yake wajitume zaidi ili kuhakikisha wanawang’oa wapinzani kwenye maeneo machache wanayoyashikilia ili uongozi uendelee kubaki mikononi mwa CCM, ambayo ndiyo iliyofanikisha kuiletea nchi uhuru hivyo aliwataka kumpigia kura za kutosha za udiwani, pamoja na kuwachagua Kikwete na Idd Azan ili kuongoza nchi kuendeleza yale waliyoanza..

“Mapinduzi si kupindua, bali ni maendeleo hivyo hata maendeleo ya nchi hii yameweza kuletwa na CCM ambayo iko madarakani mpaka sasa na wapinzani wanalijua hilo kwani falsafa zao wanazitoa hukohuko ikiwemo Baba wa Taifa Julius Nyerere, hakuna mpinzani atakayejisifia kama amefanya hiki ama kile,” alisema Songoro.

Naye Kaimu Katibu wa Tawi la Msisiri B, Vumilia Idd, aliwataka Wanamsisiri kwa pamoja kujitokeza kwa wingi na kumpigia kura Songoro ili kuendeleza yale yote aliyoyaanza pamoja na kuendeleza umoja ili kuhakikisha wanaupoteza upinzani katika maeneo hayo.

“Wana CCM wa Msisiri kazi ni moja tu, kuhakikisha Songoro anapata kura za kishindo na ili kuongoza kata hii vivyo hivyo na kwa mgombea urais Jakaya Kikwete pamoja na Mbunge Idd Azan,” alisema Vumilia.

Kampeni hiyo pia ilihudhuriwa na mshindi wa nafasi ya pili katika kura za maoni, Mustapha Muro, ambapo aliwataka wana CCM kuendeleza umoja na mshikamano ili kuhakikisha chama hicho kinatawala kipindi chote.

Upinzani ndani ya kata hiyo ni mkubwa kufuatia CUF kuwa na wenyeviti wa serikali watatu kwenye maeneo yote kuanzia Msisiri A na B, pamoja na baadhi ya maeneo ya kata hiyo na kufanya kuwa tishio kwa CCM.

"KALUNDE BAND IMFUNIKA MSUMBIJI " DEO MWANAMBILIMBI

Rais wa Bendi ya Kalunde Deo Mwanambilimbi au Mzee wa Goba akitoka nje ya uwanja huo huku mwimbaji mwingine wa bendi hiyo Debora Nyange akionekana kwa nyuma mara walipowasili leo mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Msumbiji ambako walikwenda kwa ajili ya kufanya onesho moja lililofanyika jana Oktoba 2 jijini Maputoa. Deo amesema bendi yake ilikonga nyoyo za mashabiki wa msumbiji kiasi kwamba hali ilikuwa ni ya furaha na kumfanya mmoja wa wageni waalikwa katika hafla hiyo Rais Mstaafu wa Msumbiji JoachimChisano kucheza muziki huo tena kwa furaha na hisia kali, "Hii kweli ilikuwa ni furaha kwetu na ilikuwa ni changamoto pia tumefurahia sana ziara hiyo". Anasema Deo Mwanambilimbi.
Baba yake Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel Mzee Emmanuel Mpangala naye aliwapokea wanamzuki wa Kalunde Bandi kwenye uwanja huo kama unavyomuona akiongea na wanamuziki hao, hata hivyo alisema alikuwa akimsubiri mke wake mama Maria Mpangala aliyekuwa akitokea Shinyanga.
Mwanamuziki Sarafina Mshindo akitoka nje
Remmy naye hakukosa kuwepo uwanja wa ndege J.K.
Mpiga gitaa la bezi ktoka bendi ya Kalunde Band Othman Majuto akitoka kwenye uwanja wa ndege wa Malimu J.K.Nyerere leo mchana mara baada ya bendi hiyo kuwasili kwenye uwanja huo ikitokea jijini Maputo Msumbiji.

DK. GHALIB BILAL AUNGURUMA KISIWA CHA MAFIA

Wananchi Wilaya ya Mafia eneo la Kilindoni Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Visiwani humo leo Okt 3. (Picha na Muhidin Sufiani)
Wananchi Wilaya ya Mafia eneo la Kilindoni Mkoa wa Pwani wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Visiwani humo leo Okt 3.

VODACOM TANZANIA YATIMIZA MIAKA KUMI YA HUDUMA BORA ZA MAWASILIANO NCHINI!

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania,Dietlof Mare akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa hafla ya Vodacom Tanzania kwa kutoa huduma ya miaka kumi nchini Tanzania.hafla hii imefanyika asubuhi ya leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akitoa ufafanuzi katika mkutano na waandishi wa habari juu ya mtandao wa Vodacom utakavyoboreshwa baada ya kutoa huduma zake kwa muda wa miaka kumi hapa nchini.
Mkurugenzi wa uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akikaribisha maswali mbalimbali kutoka kwa waandishi wa habari waliofikam leo katika hoteli ya Kilimanjaro Kempiski wakati wa mkutano wa Vodacom kusherehekea miaka kumi kwa kutoa huduma zake hapa nchini.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Vodacom wakiangalia picha mbalimbali tangia Vodacom ilipoanzishwa hapa nchini.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru(kushoto)akipozi kwa picha na Mkurugenzi wa Mauzo Exaud Kiwali.
Mkurugenzi wa Radio Times Rehure Nyaulawa wa pili kutoka kushoto akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Busness Time Aga Mbuguni wakati wa hafla ya kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania kutimiza miaka kumi ya utendaji wakazi nchini leo kwenye hoteli ya Kilimanjaro Kempinski kulia ni Mtangazaji wa redio hiyo Masoud Kipanya na kushoto mwisho ni Mwandishi wa gazeti la Dar Leo Eckland Mwafisi.
Mkurugenzi wa Uhusiano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Radio Times ya jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Busness Times Aga Mbuguni.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na ziara yake mkoani Kagera!!

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiendelea na zaiara yake Mkoani Kagera, kuhamasisha wanachama wa UWT pamoja na wakinamama wakereketwa kuhusu umuhimu wa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Uchaguzi Mkuu,Oktoba 31,mwaka huu.Upigaji kura ni haki kwa mwananchi wote wa Tanzania.
Hapa katika picha anaonekana akimnadi Mgombea ubunge jimbo la Nkenge Bukoba Vijijini mama Assumpta Mshana
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwanadi wagombea udwani ,viti maalumu na mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba Mjini Khamis Kagasheki.
Kikundi cha watoto wa shule ya awali ya Kitobo Misenyi Bukoba vijijini wakimkaribisha Mke wa Rais Mama SALMA Kikwete
Palikuwa hapatoshi Bukoba vijijini kwani ngoma ya asili ya Kihaya ilikuwepo na ikatumbuizwa katika mkutano huo.
Wanawake wa jimbo la Bukoba Vijijini wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete 2-10-2010

JANUARI MAKAMBA AWATAKA WANANCHI KUJITOLEA KUSAIDIA WATOTO WENYE MATATIZO!!

Mgreni rasmi katika harambee ya kuchangia Juhudi za CCBRT katikakusaidia watoto wenye matatizo Bw. Januari Makamba akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika harambee hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Double Tree maeneo ya Masaki jijini Dar es salaam ambayo inaendelea usiku huu. Januari Makamba amewataka watanzania kusaidia watoto wenye matatizo ili nao waweze kupata mahitaji muhimu kama watoto wengine na kuwapunguzia matatizo watoto hao.
Mkurugenzi wa Shear Illution Shekha Nasser akisoma hotuba yake mbele ya wageni waalikwa mbalimbali katika harambee ya kuchangia juhudi za CCBRT katika kusaidia watoto wenye matatizo.
Shekha Nasswer Mkurugenzi wa Shear Illution akiwa katika picha ya pamoja na Khadija Khalili kulia.
Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda akipata picha na Mbunge mtarajiwa wa jimbo la Bumbuli mkoani Tanga Januari Makamba.
Fiderin Ilanga yeye alikuwa akicheka tu sijui nini kimemfurahisha sana leo.
Mboni Masimba akila pozi la kiuchokozi katikaeneo la kupigia picha hebu cheki mdau
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Ilala akiwa na maiwaifu wake wakipata picha ya pamoja.
Mwanaharakati Mama Sadako kushoto akiangalia ratiba ya harambee hiyo.
Kissa na rafiki zake walikuwepo katika harambee hiyo.
Mboni Masimba kushoto, Fiderin Iranga katikatio pamoja na rafiki yao nao walipenda kuchangia harambee hiyo.
Mgeni rasmi January Makiamba akiwa katika mpicha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shear Illution Shekha Nasser ambaye ndiye aliyeandaa harambee hiyo.
Mbunge Mtarajiwa wa Jimbo la Bumbuli Januari Makamba wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba kulia kushoto ni Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa na katikati ni Lissa Jensen aliyewahi kuwa Miss Tanzania.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Vodacom Tanzania Mwavita Makamba kushoto akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Meta wa Wilaya ya Ilala Jerry Silaa kulia na mrembo Lissa Jensen katikati.
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa tayari kwa kushiriki katika harambee ya Shear Illution Ball iliyokuwa maalum kwa ajili ya kuchangia harakati za CCBRT katika kiusaidia watoto wenye matatizo.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA