Oct 1, 2010

Rais Kikwete awasili Singida akitokea Tabora ,maelfu wampokea Shelui!!

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Igunga Rostam Aziz, mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni uliohudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Igunga leo tarehe 1.10.2010.(Picha Freddy Maro na Kikosi Kazi)
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimnadi mgombea ubunge jimbo la Igunga Rostam Aziz wakati wa mkutano uliofanyika mjini Igunga, mkoani Tabora leo mchana(Picha na Freddy Maro)
Maelfu ya wakazi wa kata ya Shelui,wilayani Komboi mkoa wa Singida wakimsikiliza mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete wakati aliposimama kwasalimia leo jioni.Rais Kikwete amewasili mkoani Singida akitokea mkoani Tabora.
Mikono ya Mheshimiwa Kikwete akisalimiana na wananchi wa Igunga mara alipowasili kwa mkutano mkubwa wa kampeni Wilayani Igunga Mkoa wa Tabora leo tarehe 1.10.2010.
Wananchi wa Uyui wakimshangilia Mheshimiwa Jakaya Kikwete mara alipowasili kwa ajili ya mkutano wa kampeni.

anachuo wa IFM wamuomba Kikwete kuingia kati kupanda ada ghafla!!

Na Mary Kweka-Maelezo-Dar-Es-Salaam

WANAFUNZI wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wamemwomba Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuingilia kati tatizo la ongezeko la gharama za masomo chuoni hapo ambazo hazitambuliwi na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu

Kauli hiyo imetolewa jana Jijini Dar-Es-Salaam na Msemaji wa anafuzi hao Bw. Frank Fundi wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO).

Alisema ongezeko hilo la gharama za masomo limetokana na wao kurudia masomo kwa mwaka 2008/09 waliodahiliwa hapo awali ambapo walikuwa wakilipa ada ya Tsh. Milioni 1 kwa mwaka ikingalisha na Tsh. 1.8, ambalo ni ongezeko la Tsh. 800,000 kwa mwaka wa masomo 2009/10.

Kwa mujibu wa Fundi, kutokana na kushindwa kulipa ada hiyo, Chuo hicho kimeamua kuyazuia matokeo yao ya mihula yao yote miwili ya mwaka wa masomo 2009/10 na kuwafanya kushindwa kufahamu kama wanatakiwa kufanya mitihani ya marudio ambayo tayari imekwishaanza Chuoni hapo.

Alifafanua kuwa kwa mujibu wa Sheria za Chuo hicho, zinasema kuwa iwapo mwanafunzi atakuwa ameshindwa mitihani ya mwisho wa muhula na akashindwa kufanya mitihani ya marudio kanuni zinasema mwanafunzi huyo atatakiwa kurudia mwaka wa masomo.

“Tunamwomba Rais Kikwete kupitia ahadi yake aliyoitoa mwaka 2005 kuwa hakuna mtoto masikini atakayeshindwa kusoma sababu ya umaskini wake, itugeukie sisi na hatimaye kupata ufumbuzi wa suala hili kwani majibu ya Uongozi wa chuo hayatupi matumaini badala yake yanatukatisha tamaa”alisema Fundi .

Aliongeza kuwa ni ukweli usiopingika kuwa maendeleo ya Taifa siku zote yanaletwa na wasomi, hivyo ni jambo la ajabu kuona vyanzo vya elimu vinakuwa vigumu na hivyo kuifanya nchi kukosa wataalamu wanatakaopanga na kutekeleza mipango ya maendeleo au Uchumi.

Idadi ya wanafunzi waliokumbwa na tatizo hilo la kuzuiliwa matokeo kutokana na kushindwa kulipa ongezeko la ada ni 100 kutoka katika vitivo vya mifumo ya mawasiliano ya kompyuta na sayansi ya kompyuta, ambao wote kwa pamoja walidahiliwa katika mwaka wa masomo 2008/09.

MKUTANO WA WADAU WA MAJI WAMALIZIKA UBUNGO PLAZA!!

Waziri wa maji na umwagiliaji Mhe.Prof. Mark Mwandosya akifurahia machapisho ya shirika la kimataifa la WaterAid katika mkutano wa wadau wa maji uliomalizika jana jioni jijini Dar es salaam, anaetoa maelezo ni Afisa Mawasiliano wa Shirika hilo Bi. Sekela Mwambuli kushoto kwa Sekela ni Richard Lucas wa Taasisi ya Daraja.
Wadau wa maji nchini katika picha ya pamoja na waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Mark Mwandosya mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano wa mwaka wa wadau hao juzi, ubungo plaza jjijini Dar es salaam

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AKUTANA NA AKINA MAMA WAVUVI!!

Mama Mwananmwema Shein, mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mgombea U-Rais wa Zanzibar kupitia Chama cha mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na Mama Asha Nahodha,mke wa Waziri Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar,muda mfupi baada ya Mama Shein kuzungumza na kikundi cha akina mama wa uvuvi wa chaza hapa Zanzibar .
Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni mgombea U- Rais wa Zanzzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein akijadilina jambo na Mwakilishi mstaafu wa baraza la wawakilishi Bi Mvita Musa Kibendera,wakati Mama Shein alipofanya mkutano na kikundi cha akina mama wavuvi wa chaza mjini Zanzibar.

Picha/Clarence Nanyaro

Kampeni za Mheshimiwa Jakaya Kikwete Uyowa Wilayani Urambo mkoa wa Tabora!!

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapindzi CCM Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mkutano wa kampeni katika mji wa Uyowa Wilayani Urambo leo tarehe 30.09.2010, Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani unatarajiwa kufanyiaka Oktoba 31 mwaka huu nchini kote.
Umati mkubwa wa watu wakimshangilia Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiingia Uyowa, Ulyankulu Wilayani Urambo.
Wananchi wa Uyowa wakiwa na nyuso za furaha wakati wakifuatilia hotuba ya Mheshimiwa Kikwete kwenye mkutano wa kampeni Uyowa leo tarehe 30.09.2010

KCB Tanzania kulea watoto yatima 11 kutoka kituo cha amani orphanage


Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa K CB Tanzania ,Christina Manyenye akikabidhi vifaa vya kufundishia vyenye tahamni ya milioni 2/- kwa watoto wa kituo cha Amani Orphanage Center cha Boko kinachohudumia watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu wakati wa hafla liyofanyika shuleni hapo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center Margareth Mwegalawa akipokea msaada wa vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/- kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania ,Christina Manyenye wakati wa hafla iliyofanyika kwenye kituo hicho kinachohudumia watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dasr es Salaam leo.
Meneja Uhusiano wa KCB Tanzania , Austin Makani akigawa vinywaji kwa wanafunzi wa kituo cha Amani Orphanage Center wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa msaada vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya shilingi milioni 2/- jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania, Christina Manyenye (kushoto) na Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center , Margareth Mwegalawa wakiwasaidia kufungua maboksi yenye vitabu vilivyotolewa na benki hiyo wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni2/- jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wfanyakazi wa KCB Tanzania wakiwa wamewabeba watoto wa kituo cha yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Amani Orphanage Center cha Boko wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/-kwenyer hafla iliyofanyika shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya KCB Tanzania imeamua kubeba jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kwa kukikisaidia na kukihudumia kwa mahitaji ya vifaa muhimu vya shule kwa watoto hao kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45 wa shule hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Christina Manyenye alisema kwa kuanzia wametoa vifaa hivyo ili viwasaidie kwanza yatima.

Akifafanua alisema kutokana na kuguswa na watoto wa kituo hicho kilicho chini ya Shirika la Empowering Children and Community Organization kilichoanzishwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wameona wakisaidie kutokana na kuona kwamba ndoto za watoto hao ni sawa na za wanaotoka katika familia zinazojimudu kimaisha.

“Hivyo basi hatuna budi kuwasaidia watoto hawa na tunaahidi kuendelea kuwasaidia ili kukipunguzia mzigo kituo cha Amani jukumu la kuwalea watoto kituo hiki cha Amani ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kusoma. Ni wachache sana wanaoweza kufanya ubinadamu huu,” alisema Manyeye.

Hata hivyo aliongeza kwamba msaada huo umefuatia KCB Tanzania kutambua umuhimu wa jamii na kufahamu ukweli kuwa maendeleo ya jamii ni maendeleo ya taifa zima. Aidha alisema bila jamii yenye maendeleo uwepo wao kama benki utakuwa na mashaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Margareth Mwegalawa alisema kuwa licha kuhudumia watoto yatima 11 wanaoishi bweni, pia wanahudumia watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule na mahitaji mengine.

Hata hivyo wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kulala watoto, vitanda, uchakavu milango na madirisha ya jengo la kituo hicho jambo linalochangia kituo kuchukua watoto wachache wanaoendelea kuishi kwenye mazingira magumu.

Kutokana na hilo waliiomba KCB Tanzania na taasisi zingine kujitokeza kukisaidia kituo hicho kwa kukipa misaada mingine ikiwemo magodoro, vitanda, vifaa vya kusomea watoto, vyakula, madawati ya kukalia na vifaa vya kufundishia.

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Bunju, Syzgo Alexander aliiopongeza benki hiyo kwa kuwa na moyo huo wa kujitolea na kusema kutokana na mahali kilipo kituo imeonesha imejitoa kuihudumia jamii kwa hali na mali jambo alilotaka liiungwe mkon o na Watanzania.

KCB Tanzania ni benki kubwa Afrika Mashariki ikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo matawi zaidi ya 200 na mashine zaidi ya 400 za kutolea fedha (ATM) zilizotawanywa kote Afrika Mashariki na mtandao unaofikia nchi za Rwanda na Sudan Kusini.

Jeshi la polisi lawatunuku vyeti askari waliofanya vyema


Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha akimtunukia Cheo Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri katika mafunzo uafisa wa Polisi PC Happines Temu wakati wahitimu hao walipotunukiwa vyeti vya kumaliza mafunzo hayo leo kwenye Chuo cha maafisa wa polisi (Dar es salaam Police Academy) yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Wahitimu hao pia walionyesha uwezo wao wa kukabiliana na wahalifu wakati zinapotokea ghasia katika maeneo mbalimbali ya nchi na kuonyesha uwezo mkubwa katika kutumia vifaa mbalimbali ambavyo ni vya kisasa kabisa Hongera Serikali kwa kuboresha vitendea kazi kwa jeshi hilo ambalo lina kazi kubwa ya kuhakikisha raia wote wanaishi kwa amani nchini ikiwa ni pamoja na kuwaongezea mbinu mpya askari kitu kitakachowaongezea ufanisi wawapo kazini.
Mmoja wa wahitimu wa kozi hiyo ambaye pia ni mwanahabari wa Jeshi la Polisi Insp. Mohammed R. Mhina akiwa ameshikila Camera yake ya video huku akiendelea kunasa matukio mbalimbali katika mahafali hayo ya maafisa wa Jeshi la Polisi yaliyofanyika kwenye Chuo cha Dar es salaam Police Academy kilichopo Kurasini jijini Dar es salaam.
Polisi wa Kikosi Cha kuzuia Fujo FFU waliovalia mavazi ya kisasa kabisa na yenye usalama zaidi kwa askari hao wawapo kazini wakionyesha jinsi ya kukabiliana na ghasia mara zinapotokea.
Wahitimu wa mafunzo hayo wakipita kwa gwarede la Heshima mbele ya mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrence Masha hayupo pichani.
Magari Maalum papya yatakayokuwa yakitumiwa na jeshi la polisi Kikosi maalum cha kutuliza fujo FFU likionyesha uwezo wake wa kuzuia ghasia kwa kurusha maji leo mbele ya wageni na waalikwa mbalimbali.
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi Lawrence Masha akikagua gwaride wakati wa gwaride maalum lililofanywa na wahitimu wa Chuo cha Maafisa wa Polisi Dar es salaam Police Academy kilichopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar es salaam.
Baadi ya wahitimu wakionyesha uwezo wao wa kujihami kwa kucheza Karatee wakati walipohitimu mafunzo hayo.
Picha na mwanahabari wa Jeshi la Polisi Insp. Mohammed R. Mhina.

Sep 29, 2010

WANAMUZIKI WA FERRE GOLA WAWASILI JIJINI DAR TAYARI KWA MAKAMUZI, FERRE KUTUA KESHO SAA TANO!!

Mwimbaji na rapa wa Mwanamuziki Ferre Gola kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo anayejulikana kama (Shikitu) akihojiwa na wanahabari kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K,Nyerere, hata hivyo Kiongozi wao mwanamuziki Ferre Gola anatarajiwa kuwasili kesho saa tano za asubuhi na anatarajia kufanya onyesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee siku ya Ijumaa akishirikiana na bendi ya Mashujaa inayoongozwa na Mwanamuziki Jado Field Force
Mwanamuziki mpiga gitaa la Sollo kutoka kundi la Ferre Gola anayejulikana kama Chally Sollo akihojiwa na vyombo vya habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K. Nyerere mara baada ya kuwasili kwa ajili ya onyesho lao linalotarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee keshokutwa Ijumaa.
Mnenguaji wa bendi ya Mashujaa Frola Bamboocha akipozi kwa picha huku akiwa amevaa bango kubwa linaloonyesha picha za mwanamuziki Ferre Gola na wanamuziki wake kwenye uwanja wa ndege wa J.K.Nyerere usiku huu.
Wanamuziki wa Bendi ya Mashujaa wakiongozwa na kiongozi wa bendi hiyo Jado Field Force katika kutia hamasa ya ujio wa mwanamuziki Ferre Gola (Shetani) mbele ya Camera ya Clouds Televisheni wakati walipokuwa wakimsubiri mwanamuziki huyo kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nrerere usiku huu, hata hivyo mwanamuziki huyo atawasili kesho saa tano za asubuhi na waliotangulia ni wanamuziki wake.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHUTUBIA BARAZA LA UMOJA WA MATAIFA!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akilihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York alikomwakilisha Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Aiowa nchini Marekani wakti alipotembelea Chuo hicho Septemba 25, 2010.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe baada ya kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Mjini New York Rais Jakaya Kikwete Septemba 27, 2010. Katikati ni mkewe Tunu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana huku akipiga picha na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon kabla ya mazungumzo yao kwenye Ofisi za Umoja huo jijiniNew York Septemba 27, 2010. Mheshimiwa Pinda alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye umoja wa Mataifa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kushoto) wakiwa katika Mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa Ban Ki Moon (watatu kulia ) na Nibu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Dr. Asha Rose Migiro (wanne kulia) kwenye Ofisi za Umoja huo Mjini New York Septemba 27, 2010.

MISS PROGRESS INTERNATIONAL JULIETH WILLY AREJEA NYUMBANI NA MAFANIKIO MAKUBWA!!

Miss Progress International Juliet Willy akipozi kwa picha mara alipowasili akitokea nchini Italia alikoshiriki shindano la urembo katika taji hilo na kufanikiwa kutwaa taji hilo la Dunia ambalo ndiyo kwanza limeanzishwa mwaka huu, hivyo kuwatoa kimasomaso watanzania katika nyanja ya Urembo. Juliet amekwa mrembo wa kwanza Tanzania kutwaa taji la dunia katika masuala ya urembo na warembo wengi wameshiriki katika mashindano tofauti tofauti ya dunia lakini bado hawajafanikiwa kufikia katika kutwaa taji la dunia.
Rosemary Momburi Mama mzazi wa Miss Progress International Juliet Willy akimkabidhi ua kama ishara ya kumkaribisha nyumbani Tanzania mara baada ya kufanya vyema na kutwaa taji la dunia linalojulikana kama Miss Progress International.
Miss Progress International Juliet Willy katikati akipungia mashabiki ndugu na jamaa waliokuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili akitokea nchini Italia, kulia ni Caroline Sanga Mwandaaji wa Mashindano hayo Tanzania na kushoto ni Rosemary Momburi mama mzazi wa Juliet Willy.

TBL yazindua mashindano ya mitumbwi leo jijini dar


Meneja wa bia ya Balimi Extra,Fimbo Butallah akiongea na waandishi wa habari namna masindano ya mitumbwi yatakavyofanyika katika mikoa ya Mwanza,Kigoma,Mara,Kagera pamoja na Ukerewe katika mkutano na waandishi hao ulifanyika leo makao makuu ya kampuni ya bia Tanzania (TBL).Kushoto ni Meneja msaidizi wa bia hiyo,Edith Bebwa.
Meneja wa bia ya Balimi,Fimbo Butallah (pili shoto),Meneja msaidizi wa bia ya Balimi,Edith Bebwa (shoto) wakiwa na wadau wa Inter grated mara baada ya mkutano huo.
Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo leo.

****** ******* ********

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2010.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, ambayo yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah alisema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.

Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa. Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 4 Decemba.

Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Kigoma tarehe 9 Octoba, Kagera 23 Octoba, Mwanza 13 Novemba, Mara na Ukerewe 27 Octoba. Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu mbili za wanaume na moja ya wanawake zitakazoshika nafasi za juu katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Msaidizi wa Bia ya Balimi Edith Bebwa alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo: Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake

Mshindi wa kwanza 700,000 500,000 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 550,000 400,000 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 350,000 250,000 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 300,000 200,000 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 200,000 100,000 400,000 200,000

Tuna imani kubwa kuwa zawadi hizi zitaongeza chachu ya ushindani kwa washiriki na hivyo kuleta burudani ya aina yake kwa mashabiki.

Tunawaomba wakazi wa kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kujitokeza kwa wingi kushuhudia mashindano haya ya aina yake.

Sep 28, 2010

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI!!

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kisalimiana na Sister Davita Lumanzi wa Shirika la Wafrancisco wakati alipozungumza na watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania, kwenye Umoja wa Maifa New York ,Septemba 26,2010. Sister Davita Msomi wa fani ya Utawala katika Hospitali na anafanya kazi nchini Marekani.(Picha na Ofisi ya Wziri MKuu)
.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na baadhi ya watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York, Septemba 26, 2010
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tuni Pinda akisalimiana na Meja Ibuge wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipokutana na watanzania Waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, New York Septemba 26, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mzee, Omar Juma Mwilima katika Mkutano wake na Watanzania waishio Marekani kwenye makazi ya Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Matifa, New York, Septemba 26, 2010. Mzee Mwilima wa Mbezi, Dar es salaam,yuko Malekani kwa mwaliko wa wanae wanoishi huko. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

JAKAYA KIKWETE ALI POISISIMUA SHINYANGA

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dr.Jakaya Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Shinyanga jana jioni (Picha na Freddy Maro na Muhidin Michuzi)
Jakaya Kikwete mara baada ya kutua kwa helikopta nje ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo Jumatatu na kuamua kutembea kwa miguu hadi uwanjani
Mwanachama Mkongwe wa CCM Bi.Fatma Ndugulile akimuonesha Mwenyekiti wa CCM Dr.Jakaya Mrisho Kikwete kadi yake ya uanachama na risiti za malipo ya mwanachama tangu mwaka 1977 wakati Bibi huyo alipokutana na Mgombea huyo wa Urais kwa kupitia CCM mjini Shinyanga jana jioni. Dr.Kikwete alimsifu Bibi huyo kwa uaminifu wake kwa CCM na umahiri wake wa kutunza risiti zake za malipo.
Ze original Comedy wakiburudisha uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga jana Jumatatu
Kinamama waliokuwa wakimsubiri kwa hamu JK katika uwanja wa Kambarage mjini shinyanga wakirukaruka kwa furaha mara helikopta ya JK ilipokuwa ikitua nje ya uwanja huo.
Helikopta iliyombemba JK ikitua nje ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga leo Jumatatu

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA