

Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.



Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga akitoa shukrani mara baada ya kukabidhiwa cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi
Mkurugenzi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta akishukuru mara baada ya kukabidhiwa Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Breweries Limited Bw. Ajay Mehta.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw. Joseph Kusaga ambaye aliambatana na Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mtahaba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinazotambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru katikati ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi. Mwamvita Makamba.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Msaidizi wa Kampuni ya Azam Bw. Yusuph Kamau katikati ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo ya Azam Bw. Daniel Hill aliyembatana nae.
Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki Miradi ya Superbrands Bwana Jawad Jaffer, akimkabidhi Cheti cha Superbrands inayothaminisha nembo ambazo zinatambulika na zenye viwango vya ubora wa juu zaidi Mkurugenzi wa Kampuni ya Chemi&Cotex Industies LTD, Bw. Lakshmi Narayan, Katikati ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Chemi&Cotex Industries LTD, Bw. Riyan Dewji. (Picha kwa hisani ya www.michuzijr.blogspot.com).· Ni kwa Face Book na nyinginezo
Dar es Salaam, 26 Septemba, 2010. Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania, imezindua huduma mpya ya Intaneti ambayo itawawezesha wateja wake kuchati kwa intaneti bure.
Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Bi Mwamvita Makamba alisema jana kwamba wateja wa Vodacom sasa wanaweza kuchati bure kwenye tovuti za Face Book, the Grid na Vodamail.
Alisema Vodacom Tanzania inatoa huduma hiyo kwa lengo la kuwawezesha wateja wake kupata muda wa kuchati zaidi.
Alifafanua kwamba hayo yote yatawezekana kwa kutumia mtandao wa 3G ambao una kasi na nguvu kubwa.
“Tunapenda wateja wetu watumie mtandao wetu kwa kuwasiliana bure na hivyo kukata kiu yao ya mawasiliano”.
Alitoa wito kwa wateja wa Vodacom na Watanzania kwa ujumla kutumia huduma hiyo ya mtandao wa Intaneti.
Aliwaomba Watanzania kujiunga na Vodacom ili kupata huduma hiyo bure na hivyo kuwasiliana zaidi.
Alisema huduma hiyo itapatikana kwa simu za mkononi na pia kwa Laptop zilizounganishwa na USB Moderm.
Tangu kuanzishwa kwake miaka kumi iliyopita Vodacom imekuwa ikizindua huduma mpya kila mara kwa lengo la kurahisha huduma za mawasiliano kwa wateja wake.
Hivi sasa kampuni hiyo inawateja zaidi ya milioni saba ambao wanaunganishwa na huduma mbalimbali zenye lengo la kuboresha maisha yao, baadhi ya huduma hizo ni kama M-Pesa, ambayo ni njia ya haraka na uhakika ya utumaji wa pesa hapa nchini.
Vodacom ndiyo wa kwanza kuanzisha huduma hiyo hapa nchini.
| Wanachama Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Lindi mjini wakimsikiliza Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati alipokuwa akiwahutubia.Picha na Mwanakombo Jumaa |


P-Funk aka Majani ameizungumzia issue yake na Afande (Live kwenye Powerjamz Show - East Africa Radio) na kusema kuwa ni kweli Afande Sele alikua ana ngoma kwake lakini alikua hajamalizia kuilipia na jana ndio alikuja ghafla tena usiku na kuilipia but Afande alikua anaitaka fasta ili akai-release kwenye radio ila Majani alikua ana ratiba zake nyingine....So alikua hajambonji almost wiki nzima na alikua amekunywa dawa na kupumzika kidogo na ndipo Afande alipotinga na kutaka track yake ili akaiachie kwenye show. ......Kwa mujibu wa P-Funk sababu ya kumpiga "tena kibao tu" Afande ni kuwa alipotoka nje alimkuta Simba Dume akila "Cha Arusha" nje ya geti lake...na Majani ametamka kuwa hana noma wakae pamoja then wayamalize wala si lazima yafike "kwa kova"! KINACHOONEKANA HAPA NI KUWA HAKUNA BEEF,BALI NI LUGHA GONGANA TU BAINA YAO!
Kuna mtafaruku umetokea kati ya Afande Sele na Producer P-Funk wa Bongo Records mida hii ya mchana (Ijumaa) na Afande kupigwa na kwa mida hii amechukua RB kwa ajili ya kumfikisha Majani kwenye kwenye vyombo vya sheria. ......Ishu kwa mujibu wa Afande Sele ni hivi Afande alitoka Moro jana usiku akiwa na Ferooz na kumpatia Majani mkwanja kwa ajili ya kumalizia ngoma na kuambiwa aje leo (Ijumaa) kuchukua ngoma yake na alipofika kuchukua singo kwa mujibu wa Afande,Majani alimwambia yuko bize na kuanza kumpa kipondo!!!!(kwa hisani ya chini ya carpet blogspot.) MAGRETH KINABO NA ARON MSIGWA- MAELEZO
SERIKALI imeagiza kuwa kila halimashuri ya wilaya,miji, manispaa na majiji iwe na Mratibu wa Tiba Asili ambaye atakuwa msimamizi wa masuala ya hayo, ikiwa ni hatua ya kuwadhibiti watoa huduma wa tiba hiyo watakaokiuka sheria.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni kwa niaba yake wakati uzinduzi wa usajili wa waganga wa tiba asili nchini.
“Mratibu huyu awe ni mfanyakazi katika idara ya afya aliyechini ya Mganga Mkuu wa Halimashauri husika,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Waziri Mkuu alisema hayo huku akiagiza kuwa waganga wanaofanya matendo yanayohatarisha uhai wa watu yanayohusisha waganga wa tiba asili ambayoni uuaji wa vikongwe, albino, watoto wadogo na uchunaji wa ngozi za binadamu kuwa hawatakuwa sehemu ya wizara hiyo.
“Yeyote atakayebanika kujihusisha na vitendo hivyo, wizara haitamtambua kuwa ni mganga na hivyo hatasajiliwa na kuruhusiwa kutoa huduma ya asili,” alisisitiza huku akisema waganga na wakunga na hasa waganga wa tiba asili nchini wanatakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo yakiwemo maelekezo mbalimbali ya wizara hiyo.
Aliongeza kuwa waganga hao wanatakiwa kuanzisha vituo rasmi, kutoa huduma kwa mfumo wa kitaasisi na si mtu mmojammoja , kutayarisha dawa katika mazingira safi kujiendeleza kielimu na kuanzisha vitalu na mashamba ya miti dawa ili kuhifadhi dawa na mazingira ikiwemo kutunza kumbukumbu.
Akizungumzia kuhusu usajili huo, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mutasiwa alisema waganga na wakunga wa tiba asili wataruhusiwa kusajiliwa kwa mujibu wa sheria namba 23 ya mwaka 2002 na kanuni zake. Hivyo watakaokiuka wataadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Dk. Mutasiwa aliongeza suala la usalama wa dawa za tiba hizo litasimamiwa na Serikali chini , Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA), lakini la kuhusu jukumu la dawa na jinsi inavyofanya kazi litakuwa na mwenyewe dawa .
Na Mwakilishi Shirika la Afya Duniani Tanzania (WHO) Dk. Rufaro Chatora, alishauri wanasayansi kufanya utafiti wa dawa za asilia ili kuboresha huduma hiyo. Pia utafiti wa dawa hizo ukishirikisha na ule dawa za kisasa ufanyanyike ili kuimarisha na kuendeleza huduma hizo kwa kisasa.
MO akihutubia wananchi wa Kata ya Unyambwa.
*******************
Na Hillary Shoo.
Singida. Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM, Mohamed Gulam Dewji, amesema endapo wananchi watampa ridhaa ya kuendelea kuwawakilisha tena bungeni, atatekeleza Ilani ya CCM kwa kasi zaidi ikiwemo kutafuta ufumbuzi wa namna ya kupunguza upungufu wa ajira kwa vijana.
Dewji alisema katika ilani uchaguzi, CCM imeainisha wazi kwamba inatambua tatizo la ajira na hasa ajira ya vijana wanaomaliza elimu ya msingi, sekondari na vyuo vikuu kila mwaka kuwa, ni kubwa mno.
“Vijana hawa wote ni nguvu kazi ya taifa ambayo inaweza kutumika katika kazi na shughuli halali za ujenzi wa nchi yetu na ikapiga hatua kubwa ya kimaendeleo”,alisema Dewji.
Mgombea huyo,alisema ili kukabiliana na tatizo hilo, CCM ina mpango wa kupanua mafunzo ya VETA yaweze kuchukua vijana wengi zaidi, ili waandaliwe kujiajiri wenyewe.
Aidha, alisema vijana watahamasishwa kuanzisha miradi ya kiuchumi na kujiunga katika vikundi vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOS) ili waweze kupata mikopo kwa masharti nafuu.
“Katika miaka mitano iliyopita, nimewatafutia kazi vijana kutoka jimboni kwetu kwenye kiwanda changu cha nguo cha Afritex kilichopo mkoani Tanga., Kuajiri vijana hao, nimefanikiwa kwa kiasi fulani kupunguza idadi ya vijana wetu wanaomaliza elimu ya sekondari, kukaa vijiweni”,alisisitiza huku akishangiliwa na mamia ya wananchi.
Dewji aliyasema hayo jana katika mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Unyambwa.
Wakati huo huo,Dewji alitumia fursa hiyo kumwombea kura mgombea urais Jakaya Kikwete kwa madai kwamba ameonyesha uwezo mkubwa wa kusimamia utekelezaji wa ilani za uchaguzi. Aidha, alimnadi mgombea wa udiwani wa kata hiyo, ya Unyambwa Salum Satu na kuomba apewe kura za kutosha kumwezesha kushika nafasi hiyo.
MO, akisistiza kuwa Katika kipindi cha miaka saba michezo imeweza kupaa katika mkoa wa Singida ambapio Kindai Shooting Stars, timu ya mkoa ilibeba kombe la kilimanjaro Taifa Cup kwa mara ya kwanza katika historia ya mkoa huo.
MO akizcheza ngoma ya Kinyaturu ya kutikisa mabega, maarufu kwa jina la tikisa mabega tingisha kiuno.
Wanafunzi wa shule ya msingi Unyambwa wakimpokea MO kwenye viwanja vya shule hiyo wakati alipokwenda kweye mkutano wa kampeni wa Kata hiyo.
Wanafunzi wakiwa na mabango yanayomnadi MO huko KatikaKata ya Unyambwa.
Mwanzilishi na muandaaji wa jukwaa la wanawake wajasiriamali Tanzania (TWENDE ) na Jukwaa la kukuza vipaji vya wabunifu chipukizi Swahili Fashion Week, ambae pia ni mbunifu maarufu wa mavazi, Mustafa Hassanali amealikwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mavazi yanayofanyika jijini Arusha kwa muda wa siku mbili tarehe 23 na 24 ya mwezi huu katika hoteli ya New Arusha.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Maridadi. Maridadi ni kikundi kinachojumisha wanawake watatu kutoka mataifa tofauti ya Tanzania, Austarialia na Uholanzi ambao wanaishi nchini katika jiji la Aruha na kujishughulisha na masuala mbalimbali yanayohusiana na mendeleo ya mwanamke..
Akielezea lengo la kuandaa maonyesho hayo, mmoja wa wanawake hao, Lilian Bulengo
amesema kuwa “dhumuni kuu la kuandaa tukio hili linalojulikana kwa jina la “Maridadi Women Show” ni kuwakutanisha pamoja wanawake kutoka maeneo tofauti ya Arusha na Moshi katika Fashion Show, maonyesho ya biashara pamoja na kupata fursa ya kuzungumza mambo mbalimbali yanayowakabili wanawake katika maisha ya kila siku hapaTanzania ikiwemo suala la unyanyasaji wa kijinsia na ubakaji, wanawake na kuondokana na utegemezi na masuala ya uchumi na biashara kwa ujumla”.
Mustafa Hassanali, pamoja na kuwa mgeni rasmi, pia ataonyesha mavazi ambayo kwa mara ya kwanza alionyesha nchini Cameroon mezi wa 2 mwaka huu katika show iliyojulikana kama PARFUM D’AMOUR, na mavazi yanayojulikana kwa jina la Karafuu collection aliyoyaonyesha julai 2010 Zanzibar.
Jumla ya visura 10, kati yao nane kutoka Dar es salaam na wawili kutoka Arusha watapita jukwaani na kuonyesha mavazi hayo ya Mustafa Hassanali, ambayo yanawavutia wengi kutoka na ubunifu wa hali ya juu.
“Nimefurahi sana kupata fursa ya kuwa mgeni rasmi katika tukio hili, pia kuonyesha nguo zangu ambazo zilipendwa sana Cameroon, naamini pia wakaazi wa Arusha watafurahia kazi yangu” . Alisema Hassanali.
Katika maonyesho haya Mustafa ataonyesha na wabunifu wengine kutoka Arusha ambao ni Shwari Collectables,Hanifa Hash na Woolworth.
Mbali na maonyesha hayo pia siku ya jumamosi kutakuwa na manyesho ya kibiashara yatakayojumuisha kazi mbalimbali za sanaa za mikono. Benki nazo zitapata fursa ya kuonyesha na kuelezea shughuli zao mbalimbali wanazozifanya hasa katika kuchangia maendeleo ya wanawake Tanzania.