
























Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.

























Vodacom Miss Tanzania Geneviva Mpangala akiwa na washindi wenzie mara baada ya kutangazwa mshindi kwenye shindano hilo lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu kulia ni mshindi wa tatu Consolata Msofe na kulia ni mshindi wa pili Groly Mwanga, Geneviva ataiwakilisha nchi katika shindano kubwa la Dunia Miss World litakalofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Katika shindano hilo wanamuziki mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya wamefanya vitu vyao wakiwemo Temba na Chege kutoka TMK Family, Ambwene Yessaya (AY) Mataluma, Mwasiti na kundi la THT kutoka jijini Dar es salaam na wengine wengi.
Hii ni Tano Bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa ambapo waliulizwa maswali na kuyajibu kabla ya kutangaza mshindi wa shindano hilo kwa mwaka huu wa 2010.
Hii ndiyo kumi bora ya Vodacom Miss Tanzania mara baada ya kutangazwa kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam usiku huu.
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania wakipita jukwaani na vazi la ufukweni ilikuwa si mchezo.
Wakuu wa Kampuni ya MUZASHA TOURS wakishuhudia shindano hilo kulia ni Benedictor Mulokozi Mkurugenzi wa CM Co. Limited Charles Mtawali Mkurugenzi wa MUZASHA TOURS Muzamir Katunzi pamoja na Pamela ambaye ni maiwaifu wa Charles Mtawali.
Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam William Lukuvi aliyekaa chini pamoja na Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk Ladslaus Komba akiingia na ujumbe wake kutoka Bodi ya Utalii na Mamlaka ya hifadhi za Ngorongoro kabla ya kuanza kwa shindano hilo huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Kamti ya Miss Tanzania Hashim Lundenga. Ile safari ya mwisho ya kila binadamu katika duniani hii kwa Perfect kasiga 'P. Diddy' imehitimishwa jioni ya leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam huku warembo kibao wakipoteza fahamu wakati wa kuaga mwili wake. Ibada ya kumuombea marehemu, ambaye alikuwa mchumba wa mtangazaji wa TBC1, Maimartha Jesse, ilifanyika nyumbani kwake Kinondoni kwa Mwanamboka. P. Diddy, alifariki dunia ghafla barabarani mtaa wa Lumumba jana jijini Dar es salaam na kifo chake kushitua wadau wengi wa burudani jijini Dar es salaam.
Mtangazaji wa wa kipindi cha B&M, Ben Kinyaiya, ambaye anafanyakazi pamoja na Maimartha, mchumba wa marehemu, akitoa salamu zake za mwisho mbele ya jeneza huku akilia.
..hakika ni wakati wa majonzi na kilio kwa Ben Kimyaiya.
...warembo waliofanyakazi pamoja na marehemu katika masuala ya burudani walishindwa kujizuia kulia kwa uchungu
'Kimwana wa Manywele' (kati) ambaye anashikilia taji hilo lililoandaliwa na marehemu enzi za uhai wake, alikuwa miongoni mwa warembo waliopoteza fahamu (pichani chini) baada ya kumuaga marehemu.
Judith Mosha akisaidiwa kutembea baada ya kumuaga marehemu. Judith ndiye Mkurugenzi wa bendi ya Diamond Musica ambayo marehemu alikuwa mkurugenzi msaidizi wake ambaye alipanga bendi yake ifanye shoo kabambe wakati wa sikukuu ya Idd leo.
baadhi ya wanamuziki wa bendi waliohudhuria maziko....akiwemo Ali Choki (shoto), Kalala junior (wa pili kulia)
Maimartha Jesse akibebwa kuingia makaburini baada ya kushindwa kutembea.
MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA MJA WAKE, AILAZE ROHO YA MAREHEMU PEPONI-AMEEN!
(msaada toka global publisher)
Mkurugenzi wa Mabibo Heineken Beer Benedicta Rugemalila kulia akipunga mikono mara baada ya kuizindua albama ya sita "Vuta Nikuvute" ya Bendi ya muziki wa dansi FM Academia kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu akishirikiana kwa pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa Zain Kelvin Twisa wa pili kutoka kulia na Felician Mutta katikati, anayeonekana kuzungumza ni MC wa shughuli hiyo Benny Kinyaiya.
Rais wa Bendi ya FM Academia Nyoshi El Sadaat wa pili kutoka kushoto akiongoza wanenguaji wa kiume kutoka bendi hiyo wakati walipopanda jukwaani kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, FM Academia wanazindua albam yao ya sita inayoitwa "Vuta Nikuvute" usiku huu. Kumekuwepo na burudani mbalimbali kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee unaojumuisha wanamuziki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania, ambapo mwanamuziki Nameless kutoka nchini Kenya amefanya mambo makubwa huku akishangiliwa na mashabiki waliohudhuria kwenye uzinduzi huo.
Watotowazuri kutoka Bendi ya FM Academia waliendelrea kukonga nyoyo za mashabiki kwa staili mbalimbali wakati walipokuwa walionmyesha Makeke yao jukwaani.
MC wa shughuli hiyo Benny Kinyaiya ambaye ni mtangazaji wa TBC1 akizungumza wakati alipokuwa akiendesha utaratibu wa onesho hilo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mwanamuziki Nameless akimbembeleza kwa sauti nzuri huku akiwa amepiga magoti mmoja wa mashabiki wakati alipokuwa akiimba kwenyer ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mwanamuziki Nameless kutokam Kenya akimchukua mmoja wa mashabiki wa muziki waliohudhuria kwenye uzinduzi wa albam ya Bendi aya FM Academia ili wacheze wakati mwanamuziki huyo alipokuwa akitumbuiza kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mmiliki wa Bendi ya FM Academia Martin Kasyanju katikati akimtambulisha Felician Mutta kushoto kwa Mkurugenzi Masoko wa Zain Kelvini Twissa. | Mgombea Ubunge (CCM)jimbo la Kawe Angela Kizigha (kulia) akiomba kura mbele ya mama Salma Kikwete kwa wapiga kura wake jijini jana uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika oktoba 31 mwaka huu nchini kote. |
Baadhi ya Madiwani Wanawake jimbo la Kinondoni na Ubungo Mkoa wa DSM wakitambulishwa na kuombewa kura katika uchaguzi Mkuu ujao. | Kijana ambaye kura zake hazikutosha katika kura za maoni Nape Mnauye (kulia) akiongea katika mkutano wa umuhimu wa kupika kura. |
Kinamama wa UWT wa Jimbo la Kinondoni na Ubungo wakishangilia wakati wa utambulisho wa wagombea ubunge wa Ubungo na Kinondoni