Sep 4, 2010

TAIFA STARS YAWIKA MBELE YA WAARABU WA ALGERIA NA KUTOKA SARE 1-1!!

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imetoka kifua mbele nyumbani kwa waarabu wa Algeria baada ya kutoka suluhu ya magoli 1-1 mjini Argels na kugawana pointi moja ya kwanza katika kundi lake usiku huu katika kipute kigumu na cha kusisimua ambacho ndiyo kwanza kimemalizika. Ulikuwa ni mpira mgumu lakini pia ulikuwa ni mchezo mgumu katika maamuzi ya refa yaliyokuwa yakikatisha tamaa wakati wote wakati mpira ukiendelea hasa katika kipindi cha pili, Hata hivyo mungu alisimama upande wa Taifa Stars na kulazimisha suluhu hiyo. Shujaa wa mchezo wa leo kwa timu ya Tifa Stars na watazania ni Mchezaji Abdi Kassim "Babi" aliyefunga goli katika kipindi cha kwanza kwa mpira wa mbali na kuifanya Taifa Stars kuongoza kabla ya timu hiyo ya Algeria kusawazisha goli hilo. Kazi kubwa inabaki kwa kocha mkongwe Jean Paulsen, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na watanzania kwa ujumla kujipanga katika mchezo mwingine dhidi ya Moroco m mwanzoni mwa mwezi Oktoba utakaofanyika kwenye uwanja wa Taifa Tunatakiwa kujipanga na kuhakikisha tunasonga mbele katika michuano hii ili nasi tuweze kunusa fainali za kombe la Mataifa ya Afrika miaka miwili ijayo ambazo zimetutupa mkono kwa muda mrefu ukiachilia mbali kumbukumbu iliyoachwa na Kocha Joel Bendera ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo.

WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA KULAMBA MILIONI 46.6

Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza akitangaza rasmi zawadi za zitakazotolewa kwa washindi katika shindano la Vodacom Miss Tanzania litakalofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam septemba 11 jumamosi. Akizungumzia zawadi hizo amesema jumla ya shilingi milioni 46.6 na gari aina ya Hyundai i10 lenye thamani ya shilingi milioni 12, Amesema mrembo huyo pia atajipatia shilingi milioni 10 fedha taslimu pamoja na kujishindia zawadi ya gari. Mshindi wa pili atajipatia shinilingi milioni 6.2 wakati mshindi wa tatu atajipatia shilingi milioni 4, mshindi wa tatu atajipatia shilingi milioni 3, mshindi wa nne atapata shilingi milioni 2.4 na wa tano atapata shilingi milioni 1.4 huku washiriki wengine wakipata kifuta jasho cha shilingi laki 700.000
Mkuu wa Udhamini wa Voodacom Miss Tanzania George Rwehumbiza akisaidiana na warembo kufunua gari la zawadi ya mshindi wa shindano hilo wakati wa kutangaza zawadi za zitakazotolewa na Kampuni hiyo katika hafla iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View iliyoko ufukweni wa bahari ya Hindi huko Mbezi Beach.
Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania wakifurahia gari litakalotolewa kama zawadi katika shindano hilo.
Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza mwenye kofia Mkuu wa Itifaki Miss Tanzania Albert Makoye wakipiga picha pamoja na warembo mara baada ya kuonyeshwa gari aina ya Hyundai i10 litakalotolewa kama zawadi kwa mshindi wa shindano mhilo.

Warembo wakiwa katika ushiriki wa kutafutwa balozi wa redd's


Baadhi ya Warembo watakaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,ambao pia usiku wa kuamkia leo walikua katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Balozi wa Redd's 2o1o katika fukwe za Mbalamwezi Beach Mikocheni jijini Dar,Wageni waalikwa mbalimbali walihudhulia tukio hilo.mshidi atatangazwa siku ya Mashindano ya Miss Tanzania tarehe 11/09/2010 na atakabidhiwa zawadi zake siku hiyo.



Meneja wa Kinywaji cha Redd's Primaim Cold, Kabula Nshimo akiwakalibisha wageni waalikwa kwenye shindano la kumsaka mrembo atakaeibuka na taji la Miss Redd's 2010 usiku wa kuamkia leo ndani ya Mbalamwezi Beach,Mikocheni jijini Dar.
Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania,Pattel (kati) akiwa na wadau wengine wakifuatilia kwa makini mashindano hayo.
Madizaina wakifuatilia kwa makini tukio hilo
Wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia tukio hili usiku wa kuamkia leo.
kushoto pichani ni Meneja Mawasiliano wa TBL,Edith Mushi akiwa na wageni waalikwa wkifuatilia kwa makini shindano la kumsaka Miss Redds usiku huu
Wageni waalikwa mbalimbali ndani ya tukio la kumsaka mlimbwende atakaeibuka na taji la miss redd's usiku wa kuamkia leo katika fukwe za Mbalamwezi,Mikocheni jijini Dar.

Mh. Kikwete Aiteka Kawe, Ubungo na Mbagala leo

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete akihutubia wana CCM wa jimbo la Ubungo,katika ukumbi wa Ubungo plaza,jijini dar leo.

wana CCM wa jimbo la kawe wakimsikiliza Mh. Dr. Jakaya Kikwete ukumbi wa Ubungo plaza

Mwana CCM akitoa hoja ukumbi wa Nakiete, Mbezi Beach, wakati Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete alipokutana na wanachama wa jimbo la Kawe na kuwahutubia leo.

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akihutubia uwanja wa wana CCM na wapenzi wa chama hicho katika viwanja vya Zakheem, Mbagala jijini dar leo

Kadi za chama cha CUF zikionyeshwa kwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM mara baada ya wenye nazo kiasi cha 80 hivi kuamua kurejea CCM.

Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kutoka CUF uwanja wa Zakheem, Mbagala leo.

Shamrashamra za kumkaribisha Mh. Jakaya Kikwete katika viwanja vya Zakheem,Mbagala alipokwenda kwa ajili ya kuinadi ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) na kuwahutubia leo.

Umati wa wana CCM na wapenzi wa chama hicho wakiwa wamefutika katika uwanja wa Zakheem Mbagala leo kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kwa tikweti ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete.

wana CCM wengi walijitoteza katika viwanja vya Zakheem,Mbagala leo.

Sep 3, 2010

MKURUGENZI WA MAENDELEO WIZARA YA HABARI AWAFUNDA WAREMBO VODACOM MISS TZ!!

Mkurugenzi wa Maendeleo wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo nchini Hermas MwasoKo akiwapa hamasa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe ambapo viongozi wa Wizara hiyo walitembelea kambi ya Miss Tanzania kwa nia ya kujionea na kutoa ushauri kwa warembo hao.(kulia) Mkurugenzi Msaidizi anayesaidia Sanaa katika Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Anna Ngoi,(kushoto) Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashimu Lundenga.
Mkurugenzi wa Kamati ya mashindano ya Vodacom Miss Tanzania Hashimu Lundega (kushoto) akiwatambulisha Viongozi wa Wizara ya Habari michezo na Utamaduni wakati walipotembelea kambi ya miss Tanzania iliyopo katika Hoteli ya Giraffe wapili kutoka kushoto Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo Tanzania Hermas MwasoKo, Mkurugenzi msaidizi anayesaidia Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo ANNA NGOI.Afisa Utamaduni Mkuu wa Wizara hiyo Chiku Shomari.Viongozi hao walitembelea kambi hiyo ili kuwapa ushauri mablimbali ikiwemo na kuwahamasisha kujiamini katika shindano la miss Tanzania litakalofanyika Septemba 11 mwaka huu.
Mkurugenzi Msaidizi anaye saidia Sanaa Anna Ngoi (kulia) akisalimiana na baadhi ya Warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania Septemba 11 mwaka huu, baada ya kumalizika kwa kuwapa ushauri katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Giraffe,
Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM.

Baadhi ya Warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni wa Wizara ya Habari utamaduni na Michezo Hermas Mwasoko. wakati alipowatembelea kambini kwao katika Hoteli ya giraffe DAR ES sALAAM.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHUDHURIA MKUTANO WA MAPINDUZI YA KILIMO GHANA!!

Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akifurahia jambo na Rais wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuendeleza Kilimo (IFAD) Bw. Kanayo Nwanze (kushoto), kabla ya ufunguzi wa Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika (African Green Revolution Forum - AGRF) jijini Accra, Ghana leo asubuhi Septemba 2, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama wakati wa mjadala uliohusu Njia za Kufanukisha Mapinduzi ya Kilimo kwenye Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika jijini Accra, Ghana leo asubuhi Septemba 2, 2010. Kushoto ni Bw. Kofi Annan ambaye ni Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa.
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda na Mwenyekiti wa Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA), Bw. Kofi Annan (kushoto) wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama wakati akitoa hotuba ya ukaribisho kwenye Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika jijini Accra, Ghana leo asubuhi
Rais wa zamani wa Nigeria, Mhe. Olesegun Obasanjo (kulia) akijibu swali wakati wa mjadala maalum kwenye Mkutano wenye lengo la kuleta Mapinduzi ya Kilimo Barani Afrika uliofunguliwa leo asubuhi (Septemba 2, 2010) jijini Accra, Ghana. Kushoto ni Makamu wa Rais wa Ghana, Mhe. John Dramani Mahama na kulia ni Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda wakimsikiliza.

AY achaguliwa kushiriki tuzo nchini ufaranza,watanzania tumpigie kura ili aweze kushinda


Ambwene Yessaya a.k.a AY

Kwa mwaka huu AY alianza kunyakua tuzo ya Chaguo la Teneez ya Kenya,Kili Awards ya Tanzania na Museke Awards ya Ghana.Mwaka huu ni moto chini sidhani kama kuna artists wa bongo aliyekuwa nominee kwa awards za nchi tofauti na kushinda Tuzo..

Sasa amechaguliwa katika final za Tuzo za Ufaransa za RADIO FRANCE INTERNATIONALE DISCOVERIES AWARD 2010 {Rfi Prix Découvertes 2010} zitazofanyika September,ndani ya Paris.

AY anawaomba watanzania wote kumpigia kura za kutosha aweze/tuweze kushinda tuzo hizo.Unaweza kuvote kupitia

www.rfimusique.com

PAMOJA SANA

Dr. Bilal Akiwa Mjini Songea

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia vazi la asili ya kabila la Wangoni na silaha ya Kinjenje, baada ya kukabidhiwa na wazee wa kabila hilo, Aidan Mbano (kushoto) na Joachim Silo, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Bombambili mjini Songea jana.

Mgombea Mwenza wa Urais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi Mgombea wa ubunge wa jimbo la Songea mjini, John Nchimbi, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Bombambili mjini Songea

Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akishuka jukwaani na vazi la asili la kabila la Wangoni na silaha ya Kinjenje aliyokabidhiwa na Wazee wa Kabila hilo ili kujilinda na wabaya wake wakati wa mapigaino, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Bombambili mjini Songea jana

Dk. Mohamed Gharib Bilal, akivishwa vazi la asili la kabila la Wangoni na wazee wa kabila hilo, Aidan Mbano (katikati) na Joachim Silo, wakati wa mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Bombambili mjini Songea

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Songea Mjini, John Nchimbi, (wapili kushoto) akimkaribisha mgombea Mwenza wa Urais kwenye jimbo lake katika Uwanja wa Bombambili wakati alipofika kufanya mkutano wa kampeni. Kushoto ni mgombea ubunge wa Viti maalum wa Mkoa wa Ruvuma, Devotha Likokola.

Dk Mohamed Gharib Bilal na mkewe Bi. Asha Bilal, wakiangalia ngoma ya Ligambuza ya kabila la Wangoni, baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Bombambili mjini Songea kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni na kuinadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi

Mgombea Mwenza wa Urais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Shina la wakereketwa la CCM Stand Mpya lililopo katika Jimbo la Peramiho Wilaya ya Songea Mjini. Kulia ni Mgombea ubunge wa jimbo hilo,Jenista Mhagama.

Wananchi wa Wilaya ya Songea mjini,wakiimba na kumshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiingia kwenye Uwanja wa Bombambili kuhutubia wananchi katika mkutano wa kampeni, ikiwa ni pamoja na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo hilo John Nchimbi.Picha na Muhidin Sufiani.

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA