Sep 3, 2010

mamlaka ya mawasiliano nchini yatoa tamko kuhusu uzushi wa simu zenye madhara


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

UZUSHI KUHUSU MADHARA YA MAWASILIANO YA SIMU

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepata malalamiko kutoka kwa watumiaji wa simu za mkononi kwamba kuna ujumbe unaosambazwa kwamba ukipokea simu utapata madhara.

Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuwahakikishia wananchi kwa ujum;a kwamba taarifa zinazoenezwa ni za uzushi na sio za kweli. Wananchi wanaombwa kupuuza uzushi huo kwa kua hauna ukweli wowote.

Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna tafiti nyingi zimefanyika sehemu nyingi duniani, ambazo zimeonyesha kwamba kiwango cha mawimbi ya mawasiliano hakina madhara kwa afya ya binadamu.

Mamlaka inashauri watumiaji wa huduma na wananchi wote kwa ujumla, kuendelea kuwa na imani na teknolojia mpya zikiwemo za mawasiliano ya simu, utangazaji na utumiaji wa kompyuta, ambazo hutumiwa ulimwenguni kote bila kuleta madhara yoyote.
Madhumuni ya Mamlaka ya Mawasiliano na watoa huduma za mawasiliano kwa ujumla ni kuwaletea wananchi wa Tanzania mawasiliano bora kwa kujenga miundombinu, kutoa huduma bora na matumizi mema.

Uzushi unaoenea upuuzwe kwa kuwa hauna ukweli wowote.

Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Sep 2, 2010

MWINGINE ALAMBA MKOKO WAKE KUTOKA VODACOM "SHINDA MKOKO"

: Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akimkabidhi Torino Edward Pechaga mkazi wa Dodoma na mtumishi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) funguo za gari aina ya Hyumdai i10 alilojishindia katika promosheni ya Shinda Mkoko inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, zaidi ya magari 100 yanashindaniwa katika Promosheni hiyo na tayari washindi 30 wameshapatikana,(katikati)Mtaalamu wa mambo ya bidhaa na mahusiano ya wateja Yvonne Maruma.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru (kulia)akimuangalia mshindi wa gari la Shinda Mkoko Torino Edward na ndugu zake wakiangalia gari hilo mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi huyo wa Vodacom leo, zaidi ya magari 100 yanashindaniwa katika Promosheni hiyo na tayari washindi 30 wameshapatikana
Mshindi wa gari la Promosheni ya Shinda Mkoko inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania B w. Torino Edward akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Vodacom Tanzania katika hafla iliyofanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo leo. Kushoto kwake ni Meneja wa Kitengo cha Mahusiano ya wateja Deus Ntukamazina

TIMU YA TAIFA YA POOL YAJIFUA THE POOL TABLE VILLAGE TANDIKA!!

Kocha wa Timu ya Taifa ya Pool Dennis Lunguakifundisha wachezaji hao kwa vitendo jinsi ya kupiga mpita wa Pool wakati wa mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Kijiji cha Poll Table Village kilichopo Tandika Devis Coner jijini Dar es salaam, wachezaji hao wanajiandaa kwa michezo0 ya mikoa itakayofanyika Arusha. Kocha Lungu ameongeza kuwa mazoezi wanayofanya kwa sasa ni mepesi kutokana na wachezaji wengi kuwa kwenye mfungo wa Ramadhan lakini mfungo utakapopita na mashindano ya mikoa jijini Arusha ataanza rasmi programu ya kukiandaa kikosi hicho kwa ajili ya mashindano ya Poll Table World Championship yanayotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa mwezi Novemba mwaka huu. Ameongeza kwamba katika kuongeza uwezo wa wachezaji katika mbinu za kiuchezaji pia kuna uwezekana wa kuwa na mchezo wa kirafiki na taifa ya Zambia kwa ajili ya kujiweka sawa kabla ya kwenda kwenye mashindano ya dunia. Naye Mmiliki wa kijiji hicho cha mchezo wa Pool Mponjoli Mwakabana amesema anafurahia timu ya taifa kufanya mazoezi katika kijiji Chake kwani ni sehemu nzuri na tulivu kwa kwa wachezaji kuzingatia kile wanachoelezwa na mwalimu wao lakini pia ni sehemu ya ndani ambayo mipira inapopigwa upepo hauwezi kusukuma kama vile kwenye maeneo ya wazi.
Hapa akiwapa mbinu mbalimbali jinsi ya kufungua njia ya kucheza na kumfunga adui. Hili ndilo bango linaloonyesha kijiji cha Pool Table kikilchopo Tandika Devis Conner jijini Dar es salaam

MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WAPIGA KURA KUTOWAJARIBU WAGOMBEA!!

NA MWANDISHI MAALUM, SINGIDA
MWENYEKITI wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Salma Kikwete, amewataka wapigakura
katika uchaguzi mkuu ujao kuwachagua wagombea kwa kuzingatia masilahi ya taifa na sio
kufanya majaribio.
Alisema hayo leo (Agosti 2, 2010), alipozungumza na wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania
(UWT) mkoani hapa.
Mwenyekiti huyo alisema uchaguzi mkuu ni tukio kubwa katika kuamua mustakabali wa taifa, na
wapiga kura hawapaswi kupiga kura kwa majaribio.
Alisema wagombea wa Chama Cha Mapinduzi wanastahili kuchaguliwa kwa sababu katika kipindi
cha miaka mitano iliyopita, cha hicho kimeweza kutekeleza iliyoahidi katika ilani kwa
asilimia kubwa.
"Usiseme ngoja nimchague huyo kwa majaribio tuone naye atafanya nini, katika masuala ya
maendeleo ya taifa letu, hakuna kufanya majaribio. Majaribio hufanyika katika maabara na
siyo katika uongozi wa nchi," alisema.
Akianisha baadhi ya yaliyoahidiwa na CCM katika ilani ya uchaguzi na yametekelezwa, alisema
ni pamoja na ujenzi wa barabara, ambapo kwa sasa usafiri wa kutoka Singida kwenda Dar es
Salaam uliokuwa ukichukua zaidi ya siku nne, sasa unachukua saa kadhaa mtu anakuwa amefika.
Mama salma alisema, kuongezeka kwa shule za sekondari,kumesababisha wanafunzi wanaomaliza
elimu ya msingi kuendelea na masomo, na kuondokana na vilio vilivyodumu kwa muda mrefu vya
wanafunzi kukosa nafasi za sekondari licha ya kufaulu.
Alitoa mfano mwingine wa mafanikio ya utekelezaji wa ilani ni ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya
Ufundi Stadi (VETA), katika mkoa wa Dodoma, pamoja na ujenzi wa hospitali ya rufaa.
Naye mlezi wa mkoa wa Singida kielimu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Stadi, Mwantumu Mahiza, alisema kuongezeka kwa shule za sekondari kumeufanya mkoa wa
Singida kuondokana na wasichana kwenda mijini kufanya kazi za ndani.
Aliwataka wananchi wa singida kutohadaiwa kwani katika miaka mitano iliyopita serikali ya
Chama Cha Mapinduzi imetekeleza kwa vitendo yote iliyo ahidi.
Mwantumu alisema kwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya
2005, CCM inastahili kurejeshwa madarakani ili iendelee kuwatumikia Watanzania katika
kuwaletea maendeleo.
Mama Salma na Mwantumu kwa nyakati tofauti, walisema kwamba, licha ya CCM kuwa na uhakika wa
kushinda katika uchaguzi mkuu ujao, kinachotakiwa ni ushindi wa kishindo utakaowezesha
kupatikana kwa nafasi nyingi za wabunge na madiwani wa viti maalumu.
"Tunahitaji kura nyingi hadi zimwagige," alisema Mwantumu na kupigiwa kofi na kina mama hao.
Leo (Septemba 2, 2010), Mama Salma ataanza ziara ya mkoani Manyara ambapo atafanya mikutano
ya ndani na wanachama wa UWT akiwasihi kufanya kampeni za nguvu ili CCM iibuke na ushindi wa
kishindo pamoja na kuwanadi wagombea wa udiwani na ubunge wa chama hicho.

Jeshi la Ulinzi JWTZ laonyesha ufanisi wake kwa wananchi!!

Benjamin Sawe

Maelezo

Dar es Salaam

Serikali imesema kuwa itaendeleza ushirikiano wa kijeshi na nchi za Jumuiya ya Madola ili kuimarisha Jeshi la Wananchi la Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dr.Hessein Mwinyi katika maadhimisho ya miaka 46 ya Jeshi hilo.

Kwa mujibu wa Dr.Mwinyi tayari kuna mafunzo ambayo yamesaidia kukabiliana na uhalifu ambao unahitaji utaalamu wa hali ya juu.

Aidha Dr. Mwinyi alisema kwa kushirikiana na nchi nyingine Jeshi la Tanzania limejitaidi kupambana na Biashara haramu ya madawa ya kulevya,usafirishaji haramu wa binadamu ikiwa ni pamoja na vitendo vya ugaidi.

Kwa upande wake Mkuu wa Majeshi nchini Jenerali Davis Mwamunyange alisema kutimiza miaka 46 kwa Jeshi hilo kumeendana na maboresho mbalimbali yenye lengo la kuleta tija katika katika suala zima la ulinzi wa amani mipaka ya nchi.

Pamoja na hayo Jenerali Mwamunyange aliongeza kuwa kwa muda wa karibuni Jeshi la Tanzania limekuwa likifanya maonesho mbalimbali yanayosaidia kuonesha wananchi masuala yanayohusu Jeshi lao.

Akielezea historia ya Jeshi hilo Jenerali Mwamunyange alisema kuwa awali maadhimisho hayo yalifanyika baada ya miaka 10 ambapo kwa sasa yanafanyika kila baada ya miaka 5 yenye kushirikisha Jeshi lote nchini.

Kila mwaka JWTZ huadhimisha wiki ya majeshi ambapo kwa kawaida huanza tarehe 26/8/2010 hadi tarehe 1/9/2010 ambapo mwaka huu sherehe hizo ziliadhimishwa katika kambi ya wanajeshi wa majini kituo cha kigamboni ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dokta Hussein Mwinyi

WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WATEMBELEA KIWANDA CHA BIA TBL!!

Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakipata mafunzo ya namna ya uzimaji moto toka kwa Meneja usalama kazini,Renatus Nyanda. wakati warembo hao walipotembelea kiwanda hicho leo, Shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu jijini Dar es salaam Picha kwa hisani ya www.issamichuzi.blog
Afisa usalama wa TBL,Ismail Kalema (pili kulia) akiwaelekeza Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakati wa mafunzo ya uzimaji moto waliyokuwa wakiyapata leo katika kampuni ya bia Tanzania,TBL.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja.

Sep 1, 2010

GAZETI LA MWANASPORT LIMEPEWA SIKU KUMI NA NNE KUOMBA RADHI KLABU YA SIMBA

mwenyekiti wa simba rage akizungumza na vyombo vya habari
ndani ya ukumbi wa simba waandishi wakiwa wamebanana kutokana na udogo wa ofisi
waandishi wa habari wakiwa katika ofisi za simba hatari hii.

Mwenyekiti wa klabu ya simba ISMAIL ADEN RAGE amelitaka gazeti la mwanasport kumuamba radha ndani ya siku kumi na nne kutoka na gaziti hilo kuandika makala ambayo si yakweli iliyoandikwa
"SIKU 110 ZA RAGE NA POROJO ZAKE SIMBA ", "RAGE NI YULE YULE HAJABADILIKA".

RAGE amesema kuna mambo mengi ambayo yameandikwa na si ya ukweli

Lakini kwa upande wake mhariri wa gazeti la MWANASPORT FRANK SANGA amesema tayari amepokea barua kutoka kwa mwenyekiti wa simba inayomtaka aombe radhi ndani ya siku kumi na nne, lakini mhariri huyo amesema anamwanasherea wake ambaye anafuatilia suala hilo kwa umakini zaidi ili haki iweze kutendeka

KIKOSI CHA TWIGA STARS HADHARANI ,KAMBI YA NJE KUANZA KESHO

KOCHA W TWIGA STARS CHARLES MKWASA..

Kocha wa timu ya taifa ya wanawake twiga stars ametangaza kikosi cha wachezaji ishirini na nne watakaoingia kambini kwa ajili ya kuanza mazoezi ya kujiandaa na michuano ya kimatifa nchini AFRIKA KUSINI mwezi wa kumi.

Kocha amesema wachezaji watakaokwenda nchini AFRIKA KUSINI ni ishirini lakini pia wamemuongeza mchezaji mmoja beki ambaye atasaidia kuhakikisha timu inafanya vizuri.

SOPHIA MWASIKILI
FATUMA OMARY
MWANAIDI TAMBA
FATUMA BASHIR
MWAJUMA ABDALLAH
ASHA RASHID
ESTER CHABRUMA
HELLEN PETER
MARY MASATU
ZANA RASHID
PU;KERIA CHARAJI
MWANAHAMIS OMARY
ETTOE MLENZI
FATUMA SALUM
FADHILA KIGALAWA
NEEMA KUGA
MWASITI RAMADHANI
FATUMA MUSTAPHA
ELIZABETH KOMBA
EVELIN SENKUBO
MARIAM AZIZI
ZUHURA KABULULE
MAIMUNA SAID
FRIDIAN DAUDI

MAMA SALMA KIKWETE AWANADI WAGOMBEA ITIGI SINGIDA!!

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akikagua gwaride Agosti 31,2010 mara alipowasili Itigi Mkoani Singida katika shughuli zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete akiwa amewabeba watoto mapacha Agost 31,20101 alipowasili katika kijiji cha Kinya Mshindi Mkoani Singida kuanza ziara yake ya kuwahamasisha wanawake kuhusu uchaguzi mkuu.
Mgombea Ubunge Viti Maalumu Wanawake Mkoani Singida Martha Mlata akiwaomba wanawake wa Mkoa huo wampigie kura katika Uchaguzi Mkuu ujao. Pichani nyuma ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete .

VODACOM YAANZA KUMWAGA MAGARI YA SHINDA MKOKO!!

Mkurugezi wa Uhusiano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi funguo za gari Aprina George Chuma mshindi wa moja ya magari 100 katika promosheni ya Shinda Mkoko inayoendeshwa na Kampuni ya simu za Mkononi Vodacom Tanzania, katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwenye duka la Vodashop Mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam leo. Tayari washindi 30 wameshajishindia magari na kuna magari mengine 70 yanaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo, Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Ephraim Mafuru ameongeza kwamba leo wamekabidhi magari matatu kwa washindi na wanaendelea kutoa magari mengine kadiri washindi wanavyokuja kuchukua magari hayo ikiwa ni pamoja na kukamilisha nyaraka muhimu za magari hayo. Wengine wanaoshuhudia tukio hilo kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na anayefuatia ni Aika Makidara Matiku Mkuu wa Idara Mahusiano na Huduma kwa wateja.
Mshindi wa promosheni ya Shinda Mkoko inayoendeshwa na Vodacom Tanzania akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa gari lake aina ya Hyundai i10 katika hafla iliyofanyika jijini Dare salaam leo .
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru akiongea na Mwamvita Makamba Mkurugenzi wa Uhusiano Vodacom Tanzania kulia na Mkuu wa Idara ya Mahusiano na Huduma Kwa wateja Aika Makidara Matiku wakati wa kukabidhi magari kwa washindi wa Promosheni ya Shinda Mkoko katika hafla iliyofanyika kwenye duka la Vodashop Mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam leo.
Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru wa pili kulia akionekana kumwambia maneno ya kumpongeza Aprina George Chuma kushoto,mshindi wa Shinda Mkoko aliyejishindia moja ya Hyundai i10 30 wakati alipokuwa akikabidhiwa usafiri wake leo kwenye duka la Vodashop mtaa wa Ohio, wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusiano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba na kulia ni Rukia Mtingwa Meneja na Udhamnini.
Hii ndiyo mikoko mitatu iliyokabidhiwa kwa washindi na Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Scangroup tawi la Tanzania Barnabas Lugwisha kulia akiongea kwa msisitizo huku George Rwehumbiza,Mkuu wa Idara ya Udhamini wa Vodacom Tanzania, akimsikiliza wakati wa hafla ya kukabidhi magari kwa washindi watatu wa Shinda Mkoko katika hafla iliyofanyika kwenye duka la Vodashop Mtaa wa Ohio jijini Dar es salaam leo.

Kikwete Anguruma Mkoani Mbeya

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Dr. Harisson Mwakwembe katika mkutano wa kampeni uliofanyika wilayani humo jana.

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika vazi la uchifu mara baada ya kusimikwa na chifu mkuu wa Mbeya akishirikiana na machifu wa wilaya zote za mkoani humo.

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisimikwa uchimu

Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM,Mh. Dr. Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na machifu wa Mbeya waliongozwa na Chifu mkuu,chifu Mweshenga mara baada ya kusimikwa uchifu.

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na mmoja wa wazee wa Kyela ambaye ni mlemavu pindi alipokuwa katika wilaya hiyo kwa ajili ya kunadi sera ya CCM na kumnadi mgombea Ubunge wa jimbo hilo,Dr. Harisson Mwakyembe (katikati).

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wakazi wa Tukuyu wilayani Rungwe jana.

Mh. Dr. Jakaya Kikwete akisalimiana na wakazi wa Mbeya mjini pindi alipofika katika uwanja wa Sokoine kuwahutubia.

msafara wa pikipiki

Msanii wa Bongo Freva,Marlow akiwaburudisha wana Mbeya mjini katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mh. Dr. Jakaya Kikwete

Umati mkubwa ulifurika kuja kumsikiliza Mh. Dr. Jakaya Kikwete wakati alipohutubia Mbeya mjini jana.

Aug 31, 2010

INTERVIEW MAN X,O TEN NA JANEROSE STUDIO ZA MLIMANI RADIO LEO

KUTOKA JUKWAA LA SANAA,BASATA-FILAMU NA MAADILI YETU

Katibu Mtendaji wa BASATA,Ghonche Marerego (Kushoto) akisisitiza jambo wakati akichangia mada kwenye Jukwaa la Sanaa kuhusu Filamu na Maadili ya Mtanzania. Kulia ni Mwasilishaji wa Mada Richard Kallling, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Video Library.

Mwongozaji chipukizi wa Filamu nchini, Christian Kauzeni ambaye pia ni msanii kutoka Kundi la Kidedea akitoa mchango wake kwenye Jukwaa.

Mtaalamu na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayefanya masters yake kwenye masuala ya sanaa, Issa Mbura akifafanua juu ya utafiti wake alioufanya kuhusu filamu za kibongo.

Mwalimu Rashidi Masimbi akichangia kwa hisia kali juu ya Maadili katika Filamu zetu.Kulia kwake Ni Mkongwe wa Muziki wa Dansi, Kassim Mapili.

Sehemu ya umati wa wadau wa sanaa waliohudhuria kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu hii.

FILAMU ZA KIBONGO MAADILI YAKE NI KIFO KWETU?
Wadau,kama kawaida leo hapa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwenye Jukwaa la Sanaa kulikuwa na Mjadala Mkali kuhusu Filamu za Kibongo na maadili yake kwa jamii za kitanzania.

Mjadala huo uliohudhuliwa na zaidi watu 100 na kuchokozwa na Rais wa Chama Cha Wamiliki wa Video Library,Richard Kallinga, ulijikita kwenye haja ya waandaaji wa filamu za kibongo kutengeneza filamu zenye ubora, zenye kubeba maadili ya mtanzania, zilizo na uhalisia wa maisha yetu ya kila siku,zisizokuwa za kuiga kutona Nollywood (Nigeria), zenye ujumbe unaoeleweka na kwa ujumla zenye mvuto.

Katika mjadala wake, wadau wengi walisema kwamba, Industry ya Filamu hapa Bongo imeajiri vijana wengi na inafanya vizuri ila hawakusita kutaja matatizo sugu ambayo lazima yafanyiwe kazi ili kubadili industry hii ambayo hapana shaka imekuwa kimbilio la wengi.Matatizo yaliyoainishwa ni pamoja na:

1. Wizi wa kazi za wasanii (Piracy) ambapo ilishauriwa kwamba Cosota lazima ibadilike, ipewe meno na iweze kupambana vilivyo na tatizo hili ambalo limekuwa likiwakwamisha wasanii wengi.


2.
Kunakiri (copying) kazi za wasanii wa Nigeria na kutumia muziki (Sound Tracks) za wasanii wa muziki bila idhini yao.Katika haya wasanii wa Filamu wameshauriwa kuwa makini kwani sheria ya Hakimiliki inaweza kuwafunga.Kwa ujumla wasanii walishauriwa kuwekeza ubunifu binafsi na kubeba uhalisia wa sanaa yetu badala ya ilivyo sasa ambapo filamu zetu zimekuwa zikifanana fanana na zile za Nigeria.


3.
Uchafu wa Filamu-Wadau wengi wamesema kwamba, filamu za kibongo zimekuwa na maadili mabovu yanayotokana uvaazi wa vichupi kwa wasanii wa kike, uoneshaji wa matendo ya faragha (mapenzi) mara kwa mara, script zenye kushabikia matendo maovu na yasiyofaa kwa jamii nk.Wadau walishauri Bodi ya Filamu, vituo vya TV na wasanii wenyewe kuhakikisha wanadhibiti filamu zisizo na maadili kwani zimekuwa zikitia aibu/kichefuchefu.Ilielezwa kwamba, baadhi ya filamu hazibebi uhusika wenye ufanano na maisha/maadili ya kitanzania.

4. Wasanii kuact maisha ya juu mara kwa mara tofauti na uhalisia wao.Mtaalamu wa Filamu kutoka Chuo Kikuu,Bw.Ndunguru alieleza kwamba,filamu nzuri ni ile inayobeba uhalisia.Aliongeza kwamba, wasanii wanapenda kutumia magari ya gharama kama Hammer, majumba ya thamani, maisha ya anasa nk. kwenye filamu zao kueleza uhalisia usiokuwepo katika maisha yetu.

5. Ubunifu mdogo wa waongozaji, watengenezaji na mameneja wa Filamu ambao umekuwa ukiwafanya muda mwingi wautumie kunakiri (copying) kazi za kigeni.Ilishauriwa kwamba, wataalamu hawa wafikirie walau kupata elimu,semina na mafunzo ya muda mfupi kwenye taaluma zao badala ya ilivyo sasa.

6. Kutokuzingatia mikataba kwenye kazi zao.Ilielezwa kwamba, wasanii wengi wamekuwa wakiwalalamikia wasambazaji wa kazi (Distributors) huku wakiwa wamesainiana mikataba.Kumbe tatizo lililopo ni wasanii wenyewe kusaini mikataba kwa pupa, uroho wa fedha, bila kuisoma mikataba husika na wakati mwingine bila kuandikiana bali kwa mazungumzo tu.Ilishauriwa kwamba, wasanii lazima wasimamie mikataba na kuhakikisha inawanufaisha.Wasilalame tu, wachukue hatua pia.
JUMATATU IJAYO KWENYE JUKWAA LA SANAA

Mchango wa Kituo cha Utamaduni cha Kimataifa cha Ufaransa na Ubalozi wa Ufaransa Katika Ukuzaji wa Sanaa na Utamaduni Wetu.Tutakuwa na Wataalam kutoka Ubalozi wa Ufaransa.USIKOSEKANE.

Picha/Habari na Afisa Habari wa BASATA,

Alistide Kwizela

TENDWA KUTOA MAAMUZI PINGAMIZI LA CHADEMA BAADA YA SIKU TANO!

Msajili wa Vyama Vya Siasa Nchini John Tendwa amesema atatoa uamuzi wake dhidi ya malalamiko yaliyowasilishwa ofisini kwake jana na Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA)kuhusu mgombea wa urais kupitia chama cha mapinduzi(CCM) baada ya siku tano.

Bwana Tendwa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari hayo ofisini kwake jijini Dar es salaam baada ya kupokea malalamiko hayo rasmi leo.

‘’Nitatoa maamuzi hayo baada ya kupokea maelezo kutoka kwa mlalamikiwa dhidi ya malalamikaji yaliyowasilishwa,na nitatoa nakala ya maamuzi kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi,Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na Katibu Mkuu wa chama cha CHADEMA’’,Alisema Tendwa.

Akifafanua suala hilo Tendwa amesema baada ya maamuzi yake mlalamikaji na mlalamikiwa kama hawataridhika na uamuzi wake wanayo haki ya kwenda kutafuta haki yao kwenye vyombo vya sheria.

Aidha Msajili huyo Vyama ameongeza kuwa amepokea malalamiko hayo kwa mujibu wa sheria ya gharama za uchaguzi inachomkataza mgombea yeyote ambaye yeye mwenyewe, wakala wake au Chama chake kitafanya kitendo ambacho kimekatazwa kama ilivyoelekezwa kwenye sheria hiyo atakuwa au kitakuwa kimepoteza sifa za kushiriki mchakato wa uteuzi au uchaguzi.

Pingamizi hilo liliwasilishwa jana ofisi ya masajili huyo na Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika wakimlalamikia Mgombea urais wa chama cha mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete kutumia madaraka yake kutoa ahadi kwenye kampeni na kutangaza nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wakati wa kampeni.

WAREMBO VODACOM MISS TANZANIA WAELEZWA FAIDA ZINAZOTOKANA NA BIDHAA ZA VODACOM!!

Afisa Bidhaa wa Vodacom Tanzania Elihuruma Ngowi akiweka sawa picha kwenye Projekta wakati alipokuwa akiwasilisha mada kwa warembo wanaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania juu ya umuhimu wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kutolewa na kampuni ya Vodacom katika semina ambayo imefanyika kwenye kambi ya warembo hao Hoteli ya Giraffe Ocen View Mbezi Beach jijini Dar es salaam leo.
Meneja Mauzo wa M-PESA Jerome Munishi akitoa ufafanuzi juu ya huduma za hizo zinazotolewa na kampuni ya Vadacom Tanzania wakati wa semina ya warembo wanaoshiriki kwenye shindano la Vodacom Miss Tanzania katika Hoteli ya Giraffe Ocean View Mbezi Beach leo hii shindano hilo linatarajiwa kufanyika Septemba 11 mwaka huu.

JARIDA NUMBER 10 LIMETOKA JIPATIE COPY YAKO.


PRECISION AIR YAZINDUA NDEGE MPYA !!

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mh.Mohammed Babu akikata utepe kama ishara ya kuzindua ndege mpya ya Precision ART 42- 500 iliyopewa jina la "Bukuoba" yenye uwezo wa kubeba abiria 48 ambayo itafanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba na kurudi Dar es salaam, ndege hiyo iliruka kutoka Dar es salaam kwenda Zanziar na kurudi kwa majaribio na inatarajia kuanza safari zake mwezi ujao, wanaoshuhudia katika picha kutoka kulia ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank, Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air na kushoto ni Rubani wa Ndege hiyo Chohan Mbarouk

Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi Mh. Mohamed Babu katikati akisubiri ndege itue ili kufanya uzinduzi rasmi kwa kukata utepe kulia ni Allan Sharra Kaimu Mkurugenzi Mtendaji na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air kushoto ni Jamal Hussein Afisa Mtendaji Mkuu Citi Bank na mwisho kushoto ni Lucy Malu Meneja Mkazi Kenya Airways.
Hii ndiyo ndege mpya ya Precision Air ATR 42- 500 yenye uwezo wa kubeba abilia 48 itakayofanya safari zake kati ya Dar es salaam na Bukoba.
baadhi wa Marubani wa Precisiano Air wakiwa katika uzinduzi huo leo.
Meneja wa Uhusiano wa Kampuni ya SCANAD Barnabas Lugwisha akiwa na mmoja wa waalikwa katika ndege hiyo mpya ilifanya safari kati ya Zanzibar na Dar es salaam leo kwa ajili ya uzinduzi rasmi

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA