(Picha na Aron Msigwa)
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 31, 2010
Designers visiting the Textile Sector Development Unit
Dr. Bilal Aendelea na ziara ya kampeni masasi na nayumbu!!!
Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Bilal akizungumza na wanachi wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Masasi leo
Kamanda wa Chipukizi wa Wilaya ya Masasi, Fatuma Rajab akimvisha skafu Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal alipokuwa akiingia mpakani mwa Wilaya ya Masasi akitokea Wilaya ya Newala leo mchana
Mgobea Mwenza wa urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na wananchi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Masasi, baada ya kuingia mpakani mwa wilaya hiyo na Newala, leo
Baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi wa Wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara, wakiwa katika magari kwenye msafara wa kumsindikiza Mgombea Mwenza wa nafsi ya urais, Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akitoka Wilaya hiyo kuelekea Wilaya ya Masasi leo asubuhi
wananchi wa Kijiji cha Lukuledi Wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara, waliojitokeza kumsikiliza mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwahutubia na kuwanadi wagombea Ubunge wa Jimbo la Lulindi,Bwanausi Dismas na Mariam Kasembe wa Jimbo la Masasi leotano Wa Marais Wastaafu Wafanyika Jijini Dar
(Picha na Aron Msigwa)
Aug 29, 2010
Chama cha NCCR Mageuzi chazindua ilani yake ya uchaguzi
Pichani ni mgombea urais kwa Chama cha NNCR Mageuzi, Hashim Rungwe akionyesha ilani ya uchaguzi ya chama hicho wakati wa uzinduzi wa kampeni ya chama hicho leo jijini Dar. CHAMA cha NCCR Mageuzi leo kimezindua ilani yake ya Uchaguzi huku kikitaja mambo 12 ambayo chama hicho kitaelekeza nguvu iwapo kitapewa ridhaa ya kuongoza nchi.Wakati wa uzinduzi huo Mwenyekiti wa chama hicho taifa James Mbatia alisema chama chake kitazindua kampeni zake kitaifa Septemba 11 baada ya mfungo wa ramadhani ili kutowakwaza Waislam ambao wako kwenye mfungo wa mwezi mtukufu.“Ajenda yetu kuu itakuwa ni katiba, tumeainisha mambo yatakayokuwemo kwenye katiba hiyo, hili ndilo nataka wagombea wetu mlizungumzie kwa kina,” alisema Mbatia. VODACOM YAFUTURISHA PANGANI NA KUGAWA MISAADA YA CHAKULA KWENYE MADRASA!!

Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.
: wakazi wa mji wa Pangani waliojitokeza katika futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation wakisubiri muda ufike ili waweze kufuturu Vodacom Foundation pia iligawa misaada ya Mchele, Mafuta ya kula, maharage na vifaa vya shule kwa watoto wa Dadrasa mbalimbali na vituo vya watoto yatima mjini Pangani CUF wazindua kampeni zaao


Rais Kikwete Awasili Mkoani Mbeya
Dr.Bilal aendeleaa kuinadi ilani ya CCM mkoani mtwara
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika Kijiji cha Ntiniko Wilaya ya Mtwara Vijijini Mkoa wa Mtwara.
Mgombea Mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal akipita katikati ya chipukizi baada ya kupokelewa katika mpaka wa Wilaya ya Mtwara Mjini na Tandahimba Mkoa wa Mtwara wakati akiwa kwenye ziara yake ya mikutano ya kampeni leo mchana.
Mgombea Mwenza wa nafasi ya urais, Dk. Mohamed Gharib Bilal akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Nanguruwe Wilaya ya Mtwara Vijijini baada ya kusimama eneo hilo wakati akielekea Kijiji cha Ntiniko katika mkutano wa kunadi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) leo.
Wananchi wa Kijiji cha Nahyanga Wilaya ya Tandahimba Mkoa wa Mtwara, wakimsikiliza Mgombea mwenza Dk. Mohamed Gharib Bilal wakati wa mkutano wa kampeni.
Rais Kikwete apokelewa kwa shangwe sumbawanga na mpanda
Wanachi wa mji wa Sumbawanga wakiwa wamefurika ndani ya Uwanja wa Mandela kumsikiliza Rais Jakaya Kikwete wakati akiwahutubia.
Warembo wa Miss Tanzania watembele mapango ya amboni tanga
Aug 28, 2010
RAIS JAKAYA AWASILI MPANDA TAYARI KWA KAMPENI!!
Mwenyekiti wa Taasisi ya WAMA mama Salma Kikwete ziarani mkoani Mbeya!!
Kikundi cha ngoma ya asili cha wakina mama mkoani Mbeya kikimtumbuiza Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) Mama Salma Kikwete (hayupo pichani) alipowasili (Agosti 28.2010) katika uwanja wa ndege wa Mkoani Mbeya katika muendelezo wa ziara zake za kuwahamasisha wanawake wa UWT kuhusu Uchaguzi Mkuu mwaka huu.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.

















