SIKU moja
baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo
Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama
cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha
disco, katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa ameibua tuhuma nzito
dhidi ya Waziri Sitta na kumwita ni msaliti .
Amesema waziri Sitta alikuwa
katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti
pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM kama
alivyoahidi wakati alipokutana na viongozi wa Chadema may 2010.
Amesema katika mazungumzo hayo
yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti
lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa
alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa
wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia
chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.
Dr Slaa anasema ameamua kutoa
siri hiyo baada ya Sitta kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi
akisema kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio
kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho
Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.
Amekaririwa akisema “wenzake
wametapatapa yeye sasa ameingia na amejiingiza kichwakichwa mahali
asipopajua kwamba hatoki kwenye matope aliyoingia, kama Mbowe ni
mchezesha disco Samwel Sitta anataka kuliambia nini taifa hili kwamba
wacheza Disco ni wadhambi? ni wahalifu katika nchi hii? wacheza disco
katika nchi hii ni wapiga kura, ni vijana.. nenda pale Bilicanas! kwa
bahati mbaya kuna wazee ambao bado wanabehave kama vijana, kuna mawaziri
wanakesha pale Bilicanas, Sitta haelewi na hana uzoefu”
Kwenye line nyingine Dkt Slaa
amesema wakati Sitta akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema
na kupewa nafasi ya kuwania urais, alidai ana kundi la wabunge zaidi ya
55 waadilifu kutoka CCM ambao angehamia nao Chadema kabla ya bunge
kuvunjwa lakini pamoja na kwamba Chadema iliahidi kuyafanyia kazi maombi
yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa katika mazingira ya kushangaza
aliwatelekeza.
Katika mazingira ya kushangaza
badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake
ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza Chadema akidai hatojiunga na chama
hicho mpaka atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi
kujiondoa CCM.
Kuhusu uongozi na namna ya
kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta
akuwapangia utaratibu huku akikaririwa akitiririka zaidi kwa kusema
“Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu
mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati
akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake
nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka,”
Alisema Sitta ni kiongozi
mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na
wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi na alizizima, ambapo kuzimwa kwa hoja
hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi kunadhihirisha
jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya
Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimboni kwake Urambo.
Alisema wakati serikali
imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh
Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo
ilijengwa kwa Sh Milioni 350.
Dk Slaa na viongozi mbalimbali
wa chama hicho wako mkoani Iringa wakisubiri kuanza mikutano yao ya
vugugugu la mabadiliko waliyoipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi
la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.
Wakati huo huo Dkt Slaa
ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa
ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchini huku akiishia
kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya
serikali na michango ya wananchi. (stori imeandikwa na mwandishi Francis
Godwin wa Iringa, support kazi yake pia kupitia
francisgodwin.blogspot.com)
Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment