Kiungo
wa Yanga, Haruna Niyonzima, akimtoka beki wa Coast Union, wakati wa
mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam, jioni ya leo.
Katika
mchezo huo Yanga imeshinda 2-1, ambapo Coast Union ndiyo walikuwa wa
kwanza kuandika bao katika kipindi cha kwanza, ambalo lilidumu hadi
kumalizika kwa kipindi cha kwanza na kufanya timu hizo kwenda mapumzi
huku Coast ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi
cha pili Yanga ilianza kucheza kwa presha na kasi iliyowachanganya
zaidi Coast na kukosa mabao ya wazo na mipira mingine kigonga miamba.
Alikuwa
ni Ally Shamte aliyepiga krosi matata iliyounganishwa moja kwa moja na
beki wa Cost, Phillip Kaila, aliyeruka na kuuweka kimiani katika lango
lake. bao la pili liliwekwa kimiani na Said Bahanuzi, bao lililodumu
hadi kumalizika kwa kipute hicho.
Niyonzima, akikwepa kwanja la beki wa Coast Union.
Joshua (kulia) akimdhibiti Nsa Job wa Coast.
Kavumbangu, akimiliki mpira mbele ya beki wa Coast.
Mbuyu Twite, akijiandaa kumimina krosi mbele ya Nsa Job.
Jerry Tegete, akiruka tiktak na kukosa bao...... PICHA na http://sufianimafoto.blogspot.com/
No comments:
Post a Comment