|
Mwenyekiti
wa bodi ya wadhamini wa klabu ya Young Africans, Mama Fatma Karume
akiwaongoza viongozi na wachezaji wa yanga kwenda kuweka mashada ya maua
katika makaburi ya mauaji ya Kimbari katika eneo la gisozi jijini
kigali |
Timu ya Young Africans iliyoko Kigali
nchini Rwanda imetembelea eneo la makumbusho ya mauaji ya kimbari
yaliyotokea mwaka 1994 na kusababisha wanyarwanda wengi kupoteza maisha
katika vita iliyohusisha makabila mawili tofauti.
Young Africans iliyoko nchini Rwanda kwa
ziara ya mafunzo ya wiki moja, jana jioni ilifanya mazoezi katika
uwanja wa Nyamahoro kujiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kirafiki dhidi
ya Rayon Sports, mchezo utakaochezwa hapo kesho majira ya jioni.
viongozi wa yanga wakisubiri kuzuru na kuweka mashada ya maua katika makaburi ya mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Young Africans wakiwasili katika makaburi ya mauaji ya kimbari mjini kigali
Wachezaji na Viongozi wa yanga wakipata maelezo kabla ya kuingia kutembelea nyumba ya makumbusho ya mauaji ya kimbari
Jeryson Tegete akimtoka Godfrey Taita, wakati wa mazoezi katika uwanja wa Nyamirambo
Saimon Msuva (kulia) akichuana na Jeryson Tegete (kushoto) wakati wa mazoezi
Wachezaji
wa Young Africans wakiwa wamejipumzisha katika hoteli ya kisasa ya La
pallais mjini kigali (picha zote na PICHA NA SALEH ALLY WA CHAMPIONI
No comments:
Post a Comment