Suma Mnazaleti na aliyekuwa meneja wa Mtanashati
Entertainent, Maneno wamefukuzwa Mtanashati Entertainment kutokana na kuonesha
utovu wa nidhamu.
Akiongea na Clouds FM kwenye 255 ya XXL leo, mkurugenzi wa
kampuni hiyo Ustaadh Juma amesema meneja huyo amekuwa akitumia cheo chake
vibaya na pia kuwa na tabia ya kutoa siri za kampuni.
Amesema zaidi ni jana kwenye fainali za kipindi cha Bibi
Bomba baada ya meneja huyo kushindwa kufanya kazi yake inavyotakiwa ya
kuwaangalia wasanii wake ambao jana walilewa kiasi cha kuiabisha kampuni yake.
Amesema Suma
Mnazaleti amekuwa na tabia chafu kiasi cha kuwaharibu wasanii wake
ambapo PNC alikuwa ameacha kunywa pombe lakini tangu Suma ajiunge nao, PNC
amerudia kunywa pombe.
Hata hivyo Meneja Maneno ambaye naye amehojiwa amedai kuwa
yeye ndiye ameacha kazi baada ya kuona ubabaishaji mwingi kwenye kampuni hiyo.
"Baada ya party ya Bibi Bomba, wasanii wote wametembea kwa
mguu wengine mpaka Mwenge, yeye keshachomoka, alichokifanya ni kumchukilia tu
Taxi Dogo Janja, halafu leo hii unaondoka unasema wewe ni mtanashati," alisema.
No comments:
Post a Comment