Ni globu ya kijamii inayojihusisha na mambo yote ya kijamii,natumaini jamii yangu ya kitanzania itafaidika sana pindi ichukuapo fursa ya kuperuzi kwenye globu hii,dhamira yangu ni kufikisha ujumbe pamoja na kuiburudisha jamii yangu na furaha yangu ni kuona natimiza dhamira yangu kwako.natumaini kuwa wewe utaniunga mkono kwa kile ambacho nataka kukifanya kwa ajili ya jamii yangu ya kitanzania.NASHUKURU KWA KUNIELEWA.
Aug 16, 2012
KITU ALICHOKIFANYA RAIS MUSEVEN KWA MGANDA ALIESHINDA OLYMPIC, HII NDIO NYUMBA ALIYOKUA AKIISHI..
Baada ya kurudi home, Maelfu ya waganda wamempokea Stephen Kiprotich mshindi wa medali ya dhahabu kwenye riadha ya Olympic 2012 ambapo ameifanya Uganda itangazwe mshindi wa medali hiyo baada ya miaka 40.
Kiprotich ambae ni askari magereza alieshinda kwenye mbio za wanaume jumapili iliyopita ndani ya Olypic 2012, amezawadiwa cheki ya dola za kimarekani elfu 80 ambazo zimetolewa na Rais Yoweri Museveni ambae pia amempandisha cheo mara tisa kwenye kazi yake ya uaskari Magereza.
Standard Media wameripoti kwamba mzigo ulikua mzito manake watu walipanga foleni kumpokea Stephen huko Entebbe akiwa amebebwa kwenye gari ambalo lilikua na plate namba iliyoandikwa UG GOLD.
Watu walikua wengi mpaka waliziba njia ambapo magari yaliyokua kwenye msafara yalikosa pa kupita wakati yakielekea ikulukumpeleka Stephen kunywa chai asubuhi na Rais Museveni.
Baada ya Kiprotich kupewa cheki yake ya dola elfu 80, alimuomba rais Museveni kuwajengea wazazi wake nyumba kaskazini mashariki mwa Uganda ambapo rais Museveni amekubali kujenga hiyo nyumba ya vyumba vitatu.
Kwenye line nyingine ni kwamba rais Museven ameahidi kwamba katika muda ujao, mwanamichezo yoyote wa Uganda atakaeshinda medali ya kimataifa, atakua analipwa shilingi shilingi milioni moja za Uganda kila mwezi.(SOURCE:www.millardayo.com)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
ME MYSELF & I
THE DON HIMSELF
Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)
No comments:
Post a Comment