Nov 9, 2010

MAALIM SEIF ATINGA SUTI NA KUSHIKA HATAMU YA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS RASMI ZNZ

Salma Said, Zanzibar
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein amemteua Maalim Seif Shariff Hamad kuwa Makamu wa Kwanza wa rais na Seif Iddi kuwa Makamu wa Pili.

Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Rais Shein amemteu Maalim kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na kifungu 39(1).(2) na (3)cha Katiba ya Zanzibar.

Vilevile Dk Shein alimteua Balozi Seif Ali Idd Makamu wa Pili wa rais kwa mujibu mamlaka aliyopewa chini ya kifungu 39 (1),(2) na (6) cha katiba ya Zanzibar.

Viongozi hao wawili waliapishwa jana saa 10 jioni wakitanguliwa na shamrashamra zilizofanyika katika maeneo mbalimbali ya katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Utuezi wa Maalim Seif ambaye ni Katibu Kkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwa makamu wa kwanza wa rais unafuatia mwafaka uliofikiwa baina na CUF na CCM Zanzibar kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kulingana na matokeo ya uchaguzi mkuu.

Katika makubuliano hayo, mshindi wa kwanza kwenye kinyang’anyiro hicho ndiye anakuwa rais na mshindi wa pili anakuwa makamu wa kwanza wa rais. Chini ya maridhiano hayo makamu wa pili ambaye ndiye kiongozi wa shughuli za serikali huchaguliwa kutoka katika chama cha rais.

Matokeo ya uchaguzi wa rais wa Zanzibar yalimpa ushindi Dk. Shein wa CCM akifuatiwa na Maalim Seif wa CUF, hivyo kwa mujibu wa maridhiano hayona marekebisho ya Katiba ya Zanzibar, Maalim anakuwa makamu wa pili na Seif Iddi kutoka CCM anakuwa makamu wa pili na mkuu wa shughuli za serikali.

Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar kifungu cha 20 (6), Makamu wa Pili wa Rais anateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka katika chama anachotoka Rais.

Marekebisho hayo ya katiba yanaeleza kuwa Makamu wa Pili wa Rais ndiye atakuwa mshauri wa Rais katika kutekeleza majukumu yake na pia atakuwa mkuu wa shughuli za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).

Dk Shein ambaye anakuwa rais wa saba tangu visiwa hivyo viuondoe utawala wa kisultani mwaka 1964 alimshinda kwa tofauti ya kura chache mgombea wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad.

Katika hotuba yake baada ya kuapishwa kuwa Rais SMZ wiki iliyopita, Dk Shein alisema licha ya urais kuwa jukumu kubwa na gumu, atatumia nguvu na uwezo wake wote kutekeleza wajibu wake kwa maslahi ya taifa na watu wake bila ubaguzi ili kudumisha umoja wa kitaifa visiwani humo.

Sherehe za kumwapisha Dk Shein zilizofanyika Jumatano wiki mjini Zanzibar iliyopita zilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Jakaya Mrisho Kikwete, marais wastaafu wa Serikali ya Muungano, Benjamin Mkapa, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais SMZ anayemaliza muda muda wake, Aman Karume, aliyekuwa Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha Rais wa Awamu ya Tano wa SMZ, Dk Salmin Amour na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.

Wakati huo huo, Wajumbe wateule wa Baraza la wawakilishi wamemrejesha Spika Pandu Ameir Kificho katika kiti chake uspika kwa ushinda wa kura 45 dhidi ya mpinzani wake Abass Juma Mhunzi aliyepata kura 32 kati 78 zilizopiwa na kura moja iliharibika.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA