Mimi kama mwenyekiti wa kamati ya ushindi kwa timu yetu ya Taifa (Taifa Stars) ninayofuraha kubwa kuwapa pongezi uongozi mzima wa timu yetu ya Taifa pamoja na wachezaji wetu kwa ushujaa waliouonyesha katika mechi yao dhidi ya Timu ya Taifa ya Algeria iliyochezwa siku ya Ijumaa tarehe 3/9/2010 ikawa ni kampeni za kuelekea katika kombe la mataifa ya Afrika.
Kwa nini nasema ni ushujaa? Ni kwa sababu ya kuweza kuonyesha mchezo safi ile hali kukiwa na uonevu ulioonekana wazi ukiwa na lengo la kukandamiza timu yetu isipate ushindi. Hakuna mtu yoyote ambaye aliyeshuhudia mechi hiyo atapingana nami eti kulikwa hakuna uonevu! Lakini matokeo tuliyoyapa yamedhihirisha ukomavu wetu katika soka la kimataifa, Pongezi zangu za dhati zimfikie kocha mkuu wa Jean Paulsen kwa kuweza kuwataarisha wachezaji kiakili ili kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya uonevu na pia nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitampa pongezi nyingi Abdi Kassim (Babi) kwa goli zuri alilolifunga katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Vilevile tukumbuke haya yote ni matunda ya mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuamua kuweka nguvu kubwa katika mchezo wa soka nchini naye pia nampa pongezi kubwa na ninafahamu naye anasheherekea pamoja nasi matokeo haya popote pale alipo.
No comments:
Post a Comment