Tunathubutu kusema hivyo kwa sababu tayari tumesikia mara kadhaa viongozi/wagombea mbalimbali wakijinadi kwamba wamefanya nini katika miaka mitano iliyopita na wanatarajia kufanya nini endapo wananchi watawapa tena dhamana ya kuongoza nchi kwa miaka mingine mitano.
Pia tumeshasikia tambo mbalimbali kutoka kwa wanaowania kuunda serikali mpya,wakijinadi kuhusu watakachokifanya tofauti endapo “ngekewa” ya kuwaongoza watanzania itawaangukia wao.Sasa kama tambo hizo sio sehemu ya kampeni,sijui Tume ya Uchaguzi ina tafsiri ipi kuhusu maana ya “kampeni”.
Bila shaka,baada ya kuwasikia wagombea mbalimbali wakijinadi na kutokana na uzoefu wako na jinsi unavyofuatilia shughuli mbalimbali za kisiasa,umeshafanya maamuzi(japo katika fikra tu) kwamba pindi itakapofika mwezi Octoba,kura yako utampa mgombea fulani.Ndio maana tunauliza;Uchaguzi Ungefanyika Leo,Ungemchagua Nani?Kwanini? Wanaogombea nafasi ya Urais kutoka vyama mbalimbali,hawa hapa:
Civic United Front(CUF): Professor Ibrahim Haruna Lipumba(kulia) na mgombea mwenza,Juma Duni Haji.
Chama Cha Mapinduzi(CCM):Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea Mwenza,Dr.Gharib Bilal.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) r.Wilbrod Slaa akisalimiana na Mgombea Mwenza,Hamisi Mzee Hamisi.
National Convention for Construction and Reform-Mageuzi(NCCR-Mageuzi)-Hashim Rungwe(kushoto) na Mgombea Mwenza,Ali Juma
No comments:
Post a Comment