Jul 16, 2010

BEEF KATI YA TZ V/S KE


Baada ya video ya wimbo unaoitwa Nitafanya ambao ni ushirikiano wa Kidum(mwanamuziki kutoka Burundi) na Lady JayDee hapo jana,tumepokea maoni tofauti tofauti as a presenter wa radio. Maoni hayo yamekuja kutokana na ukweli kwamba kuna tofauti katika wimbo uliopo katika video na ule wa Audio ambao siku za nyuma tuliuweka baada ya kuupata kutoka kwa Producer Hermy B kama sehemu ya promotion ya wimbo huo.
Waliopata kuusikiliza wimbo huo katika Audio walielezea kukerwa kwao na jinsi wimbo huo ulivyobadilishwa au kuwa tofauti na ule wanaousikia katika video.Wengi waliupenda zaidi ule wa Audio.Kwanini nyimbo hizo zikawa tofauti? Je Producer wa nyimbo zote mbili ni mmoja?
Jibu kwa swali la kwanza nitakuachia wewe msomaji/msikilizaji.Ila jibu la swali la pili ni Hapana. Producer wa wimbo wa kwanza ni Hermy B akishirikiana kwa karibu na Kidum mwenyewe wakati ule wa video umetengenezwa na RKay Kamanzi,producer/videographer kutoka nchini Kenya. Huyu ndio pia producer wa nyimbo za msanii Wahu kama vile Sweet Love na Runnin’ Low.
Nini kilitokea? Kwa mujibu wa “Insider” kutoka B’Hitz Studio,kilichotokea ni kwamba,Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy ambae siku za nyuma walikutana wakati wa Project Fame kule Nairobi.
Wakakutana na kufanya kazi pamoja huku Hermy B akiwa na jukumu la recording,engineering,adding instruments, mixing and mastering na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern yote ikiwa ni ya Hermy B. Raundi ya kwanza ikawa imeisha.
kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na RKay.Dhumuni likiwa ni kutengeneza Video ya wimbo huu kwani RKay anayo pia kampuni ya kutengeneza video inayoitwa Maramoja Films. Cha ajabu RKay akamshawishi Kidum mpaka akakubali kurekodi au “kuutengeneza” upya wimbo huo. RKay akakopi karibuni kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, kama ambavyo inasikika katika video tofauti na inavyosikika katika audio.Kimsingi idea ya kisanii ya Hermy B ikawa imetupwa nje(kwa kiasi fulani) bila yeye mwenyewe kuambiwa au kushirikishwa kama ambavyo sheria za kazi za kisanii zinavyokwenda.


Bila kujua kwa undani kinachoendelea, Hermy B aliutoa wimbo katika Radio Stations mbalimbali na pia blogs kama JIWE THE DJ na nyinginezo. Hapo ndipo mambo yalipokwenda mrama kwani Kidum alizi-approach radio kadhaa ambazo tayari zilikuwa zimeshaanza kupiga original version ya wimbo akiwataka kuacha kuupiga. Alipoulizwa kwanini hakuwa tayari kuelezea kwa kina kilichotokea. Lakini stesheni kadhaa zikaendelea kuucheza ule ule wa kwanza ambao umetengenezewa Tanzania na sio Kenya. Kwa kifupi “Beef” likaanzia hapo!
Wakati yote hayo yanatokea, Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa RKay ukichezwa na upo katika video iliyopigwa au kuongozwa na RKay JE hammy anazungumza nini juu ya hilo?soon ntawawekea clip yake wacha nimtafute aseme kwa kina zaidi.

No comments:

THE DON HIMSELF

Karibuni sana kwenye blog hii ya kijamii iliyosheheni makila kitu kuanzia siasa uchumi afya na burudani kwa ujumla wake.uingiapo kwenye blog hii ni mengi ambayo utapata nafasi ya kukutana nayo,kumbuka mawazo yako ndo hasa yanayojenga na kunifanya niwe na ufanisi zaidi.kariiiiiiibuuuuuuuuuuuu saaaaaaaaaaaaaaanaaaaaaaaaa.(THE DJ HIMSELF-JIWE)

Followers

BLOG ZA MARAFIKI

Search This Blog

ZILIZOPITA

DUNIA MUZIMA