Masela walioenguliwa ndani ya kundi la TMK Wanaume Halisi na kiongozi wa kundi la TMK Wanaume Halisi, Juma Kassim ‘Sir Nature’ wameibuka na kuunda kundi lao jipya.
Kampuni ya Mpo Afrika imetangaza kusaini mkataba na kundi jipya litakalokuwa likiitwa Wanaume, likiundwa na wanamuziki walioachwa katika kundi la TMK Wanaume Halisi.
Akizungumza jana bosi wa kundi hilo,Hassan Umande alisema lengo la kuunda kundi hilo jipya ni kwa ajili ya kuendeleza sanaa na kuleta mabadiliko katika anga ya muziki wa kizazi kipya aka bongofleva hapa nchini.
"Unajua kiukweli kuna vikwazo vingi vilitokea mpaka tukaamua kujitenga ,yote hiyo kuepuka migongano ambayo kimsingi si ya lazima kwa sababu sote ni vijana na tunatafuta maisha,kwa hiyo kwa sababu tumetengwa basi tumeamua kuunda kundi la watu sita"'amebainisha Hassani Umande.
Hassani amewataja wasanii watakaounda kundi hilo kuwa ni Athuman Yahya (A.Man), Juma Mbelwa (Juma Jazz), Karim Kaiman (Kakaman), Abdul Ally (Mzimu), Richard Shauri (Rich One) pamoja na David Mpangile (Daz-p).
Alisema mpaka sasa wamesharekodi nyimbo tatu ikiwemo, mapenzi kitu gani?, Poa tu pamoja na Mukide.
No comments:
Post a Comment